TUSIKASIRIKIANE!
Rais wangu Magufuli:
Trump atakuwa alicheka kwanini Profesa Kabudi alipaita UDSM ni jalalani, chuo kikuu cha kitaaluma na mashuhuri kusini mwa jangwa la sahara. Trump lazima ashangazwe na hili.
Au labda Trump alishangaa ni kwa sababu gani mtu mwenye hadhi ya kuwa profesa anaimba nyimbo za kumpongeza Rais kuliko idadi ya neno 'Tanzania' katika kinywa chake.
Au labda Donald John Trumol alicheka kwa sababu una miaka minne hujawahi kukanyaga pale New York City kwenye UNGA, na mara zote umekuwa unatuma wawakilishi tu..
Au labda alishangaa kwanini Profesa Kabudi anaacha kazi chuo kikuu ya kufundisha waswahili ambao wanahitaji ukuzwaji wa maarifa kutoka kwake na kukubali kuitwa "mpumbavu" kulinda cheo cha 'uwaziri'
Marekani haina shirika la ndege linalomilikiwa na kuendeshwa na serikali (state owned). Nafikiri watu wetu watajifunza kidogo kuhusu uendeshwaji wa American Airlines Group
Rais wangu Magufui:
Sijui kwanini unadhani Trump alishangaa Tanzania kununua ndege Boeing, wakati hata Eritrea Airlines wanayo Boeing 737-300
Kwanini watushangae sisi kununua ndege kwao wakati hata Air Djibouti wanazo Boeing 737-400 na Boeing 767-200ER? Kwamba sisi ndio 'maajabu?'
Hata wasomali waliokuwa vitani waliweza kununua ndege hizo za Boeing, kwetu Tanzania haiwezi kuwa ni jambo jipya la kumshangaza Trump! Eeh! Kwanini ashangae?
Pesa ya pambano moja la Floyd Mayweather Jr keenye endorsement yote katika pambano lake vs Conor McGregor... Ndio thamani ya ndege yetu moja.. Imshangaze Trumoe? kweli?
Rais wangu Magufuli:
Kwani na mimi nikinunua Azam Malt au Mo Energy, nitakuwa daraja sawa na Said Salim Bakhresa na Mohammed Gullam Abbas Dewji?
Kwamba kwa sababu tumenunua ndege hizo (Boeing) kwa watu wa Marekani basi na sisi tumekuwa 'level' moja na hawa wamarekani? Sawa!
Kwamba, kwa sababu Trump katupongeza kununua ndege Marekani, basi sasa ni rasmi na sisi tunalingana na hao wamarekani?
Umaskini sio jambo jema. Sio jambo la kufurahia. Lakini kujimwambafai kwamba sisi ni matajiri na kutaka tutembee vifua mbele ni kutulisha chakula kizuri machoni, mdomoni hakipiti.
Rais wangu Magufuli:
Tumetumia zaidi ya bilioni 571 za kitanzania kununua ndege hii ya Boeing 787, fedha za kodi zetu.. Nani alikueleza tunahitaji ndege? Wananchi gani huko kwenye ziara wanalilia ndege?
Wanakijiji wa kijiji cha Shuka, halmashauri ya Mtama, Lindi wanalalamika hawana maji ya kutumia, wanatumia maji na wanyama, maji ni kero kwao.
Mimi na wenzangu, kwetu huko Tarime, zahanati, vituo vya afya na hospitali ni kero kubwa, kata hazina vituo vya afya, hospital ya wilaya hakuna Vifaa tiba.
Needs vs Wants.. Mahitaji makuu sidhani kama ni hayo madege,.. Hizo ni 'wants' tu. Wananchi wa Mtama wanataka visima vya maji safi na salama sio ndege hizi .
Hatuna scale of preference? Au ni lazima kununua Lamborghini ,Ferrari, Porsche, Buggati,Bentley, Aston Martin, Jaguar, Rolls-Royce, Audi, Maserati wakati wa njaa kali nyumbani?
Rais wangu Magufuli:
Kuna upungufu wa vyumba vya madarasa kwa zaidi ya asilimia 50 kwa shule za msingi na sekondari..
Kuna upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo mashuleni kwa zaidi ya asilimia 40 shule za msingi na sekondari
Kuna upungufu wa walimu wa shule za msingi na sekondari nchi nzima kwa zaidi ya asilimia 30.
Vipi upungufu wa vifaa tiba na dawa Katika hospitali za serikali kwa zaidi ya 65%?
Upungufu wa madaktari na wauguzi Katika hospitali za umma nchi nzima kwa zaidi ya asilimia 45?
Kuna kata hazina vituo vya afya, vijiji havina zahanati na baadhi ha hospitali za wilaya hazina vifaa tiba. Tumesahau?
Rais wangu Magufuli:
Umeme umefika kwa kiwango gani kwa wananchi vijijini? REA III inakuja, itamaliza vijiji vyote kwa Umeme?
Vipi nyongeza ya mishahara kwa watumishi? Mikopo elimu ya juu? Ajira? Wananchi Hawa wana uwezo wa kujiajiri wenyewe Katika sekta binafsi?
Rais wangu Magufuli:
Wapambe hawana jema. Hawatakueleza kweli, na ukweli tutakueleza sisi wengine ambao hatusubiri mrija wa mnunurisho wa asali na maziwa.
Wananchi wa Nachingwea, tunadai zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 3.4 za mazao yetu ya korosho ambayo serikali ilichukua kwetu. Mtulipe fedha zetu!
Wakulima wa mbaazi, dengu na choroko hatujui soko letu tena. Bidhaa zimeoza ndani. Naibu waziri wa viwanda na biashara alisema tule mbaazi kwa sababu ni nzuri kwa afya!
Rais wangu Magufuli:
Kwanini kila kiongozi ambaye anapata nafasi ya kupanda jukwaani mbele yako anasema ndege hizi ni zako, na yule wziri wa uchukuzi amesema hili ni wazo lako,
Ni kweli ni wazo lako? Sio matakwa ya wananchi? Hizi ndege zinaendeshwa kwa kodi ya nani kama sio hao wananchi? Zimenunuliwa na nani kama sio mwananchi?
Kiongozi wa serikali anapanda jukwaani anawananga wananchi wengine, hii ni kwamba kuna ambao hawakuchangia ununuzi wa ndege hizo? Kwamba
Rais wangu Magufuli:
Nimesikia ukisema utafuatilia faida iliyotengenezwa na ATCL. imetajwa na Kamwele kwamba ni USD14M yaani "dolari milioni 14 za kimarekani"
Kwa kweli uzifuatilie. Maana, The issue is endemic. Unfortunately. Anywhere in the world, political kleptomaniacs never put their people's interests ahead. Never. Saad
Kisha, utupe sisi "wanyonge wenzako" mrejesho, wa kimaandishi, ikikupendeza, na risiti za ununuaji ndege hizo, maana unasisitiza sana "Toa risiti: Dai risiti" ni vyema tukafanya hivyo.
Mheshimiwa Rais, nikutakie 'weekend' njema, afya tele! ni mimi mwananchi wa Tanzania, mtaani wananiita eti "jeshi" na hawataki kuacha, mimi nawaomba waendelee kuniita 'ninja' au wakishindwa 'Rambo'
Nakusalimu Tata!
#MMM, Martin Maranja Masese