Wale waliobeba fedha za Escrow kwenye sandarusi kana kwamba ni malipo ya korosho watumbuliwe,waliofungua akaunti nje ya nchi bila kufuata utaratibu watumbuliwe mwanawane.
Tanesco na bei zao za umeme ni maumivu tu pamoja na vyanzo kuongezeka bado ni shida tu,nako patumbuliwe pia, Richmond kama bado inalipwa naomba malipo yasitishwe na utumbuaji ufuate.
Yule aliyesafirisha wanyama pori, kugawa vitalu kama shamba lake la urithi atumbuliwe pia, na wanyama warudi.
Mikataba yote ya serikali iwekwe hadharani maana sisi wananchi ndio wanufaikaji ama wapata madhara patumbuliwe na huko.
Magufuli sisi wananchi tunakuombea kwa Mungu. Usiogope kitu, tumbua tumbua tu.