Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

JIPU lipo kwenye hizi bank ambazo ni wakala wa TRA kwenye ukusanyaji wa kodi na baadhi ya maafisa wa TRA.

Hili lipo sana hasa katika ulipaji wa PAYE (Income tax) kwa wafanyakazi hasa makampuni/taasisi binafsi.

Majuzi mtu kalipa kodi Tsh 10 million anapewa risiti ya Tsh 10.00 halafu wanasema ni system error, na wakati huo huo account wanayodeposit hizo kodi ni tofauti. Tunao ushahidi wa hili, lilitokea CRDB.

Naomba hili jipu litumbuliwe
 
Mtu unatoka chuoni na kupata ajira yako ya kwanza unalazimika kulipa mamilioni kuanga nyumba wakati ungeweza kulipa kila mwezi na ku-save kidogokidogo ili kujiimarisha, ndio maana watu wanakwiba mali ya umma au kura rushwa hili kumudu maisha, but why?

1. Kwanini wapangaji walipe kodi ya miezi sita/mwaka wakati NHC wanatoza kodi kwa mwezi na hata wenzetu kenya na uganda wanalipa monthly?
2. Je wapangishaji wanalipa kodi yeyote serikalini baada ya kupokea rent?
3. Je serikali haioni ingesimamia rent kulipwa kila mwezi ingeweza kukusanya kodi toka kwa wapangishaji kiurahisi?
 
JIPU NO. O1.
Sisi walimu tulosimamia mtihani wa form four 2015 wilaya ya MONDULI bado hatujalipwa haki yetu na hali kwingine wameshalipwa.Mimi ndo mhanga wa hili.

JIPU NO. O2.
Wilaya ya TEMEKE nako kuna kajipu maana walimu waloajiliwa mwaka mmoja na kwenda masomoni mwaka mmoja huku wote wakiwa na ruhusa. Wengine wanapandishwa madaraja na wachache wanaambiwa ukiwa masomoni hupandishwi daraja.

Hako nako ni kajipu.
 
Jipu lipo huku Mwanga barabara.

Miradi yote ya maji aliyoianzisha Maghembe kabla ya awamu ya JPM baada ya kuwa waziri ameiomba serikali pesa zote amegeuza kutoka barabara ya kiwango cha changarawe/lami wapi na kukwangua tuu tena alisema yeye ndo mwanaume tuuu Mwanga nzima hakuna wa kumfanya kitu.

Kampuni ni ya best wake wanagawana tuu mabilioni mzigooooooo huuuu
 
Hotel zinazomilikiwa na makampuni ya mabasi ya Dar - Arusha zina mauzo yanayozidi stahiki ya kusajiliwa na VAT lakini bado wanauza kwa kutumia "manual coupon" nadhani TRA Korogwe wana tatizo la kushindwa kuthibiti hiyo hali.

Kwa kuwa mteja hulipa kwanza ndio apewe huduma basi watoe risiti za mashine ya TRA moja kwa moja ili walipe kodi stahiki. Mbaya zaidi bei wanazotoza ni sawa na hotel za kitali....mtori 5000 wapi na wapi
 
Jipu kubwa zaidi lipo kwa uhamiaji kuna wahamiaji haramu wanaofanya kazi bila vibali na hawana vibali vya kuishi nchini pia. Tumetoa sana ripoti kwa maafisa wa uhamiaji lakini tukageuziwa kibao tukaitwa na boss tueleze kwa nini tunataka kuua kampuni yake yeye hana pesa ya kulipia wageni maana wapo zaid ya 50 so serikali hapa imekosa zaidi ya million 100. Huyo afisa aliyetuchoma anaitwa John M jina la pili tumemstai kwa sasa tu natafuta namna ya kuakikisha tunafikisha hizi taarifa kwa Magufuli maana huyo Waziri Kitwanga nae ni mzigo tu hatumuamini.

Huu ni ujipu wa hali ya juu sisi tunatoa sapoti kwa taifa wao wanaenda kuchukua rushwa alafu wanatuchoma. Uhamiaji ni jipu jipu kubwa sana.

Nakubaliana kuwa KITWANGA NI MZIGO, madudu yaliyojazana Uhamiaji, Polisi, Idara ya Wakimbizi, na hata Mageraeza, yeye nasikia anatumiwa na wakuu wa idara hizo kujenga hoja za kutetea madhaifu kibao ya huko, eti kwa sababu walisoma naye!!
 
Mkuu: Bara Bara ya Goba; kuanzia masana hospital kuna kipande hakiishi kujengwa sijui kulikoni?

Magufuli tunakutegemea wakazi wa huku kipande hicho tu ndo bado wakati kuanzia mbezi mwisho mpaka hapo zaidi ya kilomita 10 ni lami tu.....hapa kuna nini???

Alafu hii hospital ya Masana wanafungulia maji ya chooni na maji taka wanayaelekeza barabarani yaani ni pananunuka na hapakaukagi

Tumbua hii Masana Hospital
 
SHIDA YA MAJI GOBA

Mh Magufuli; Huku kwetu Goba maji ni kilio ila tunachoamini ni kwamba kuna watu wachache wamekwamisha mradi wa maji kwa muda mrefu sasa ilihali wananchi tunaatabika
Kuna watu wenye miradi ya KUUZA MAJI KWA MAGARI hawa ndio wanatukwamishia wananchi kupata maji....tumeetaabika kwa muda mrefu na sasa inatosha

Kuna Diwani wa kata moja kati ya kata za huku ana mradi mkubwa ndo anakwamisha mradi wa maji huku kufikia wananchi

Rushwa na matumizi mabovu ya mamlaka sasa basi; Magufuli tumekuchagua tuna imani na wewe hata hili unaweza baba
 
Wale waliobeba fedha za Escrow kwenye sandarusi kana kwamba ni malipo ya korosho watumbuliwe,waliofungua akaunti nje ya nchi bila kufuata utaratibu watumbuliwe mwanawane.

Tanesco na bei zao za umeme ni maumivu tu pamoja na vyanzo kuongezeka bado ni shida tu,nako patumbuliwe pia, Richmond kama bado inalipwa naomba malipo yasitishwe na utumbuaji ufuate.

Yule aliyesafirisha wanyama pori, kugawa vitalu kama shamba lake la urithi atumbuliwe pia, na wanyama warudi.

Mikataba yote ya serikali iwekwe hadharani maana sisi wananchi ndio wanufaikaji ama wapata madhara patumbuliwe na huko.

Magufuli sisi wananchi tunakuombea kwa Mungu. Usiogope kitu, tumbua tumbua tu.
 
Jamani heshima ya Watanzania nje ya mipaka imeanza rudi taratibu ajili Magufuli!

Juzi kati nikiwa kwenye mizunguko Nairobi/Kenya! Nikawa naulizia aina flani ya kitu maeneo ya Weslands! Wakanambia we mTZ nkawambia ndio! Wakanambia wow muko na a very nice President! Ndo twataka such a leader hata kwetu!

MGANDA nae alikua hapo akapokea yap u guys are lucky! Wale Wakenya wakaanza nambia na twaskia anakwenda kwa public sectors and ana fire wazembe? Nkawajibu yeah! Ukweli walikua wako excited sana niwambie zaidi alafu MAGUFULI anafatiliwa kila tukio Kenya!

Mwishowe nikawambia haya naenda mja akasema okay ngoja tukupe ur item ikiwa inafanya kazi powah! Usifike usiende tusemea kwa Magufuli ha ha ha wakacheka wakaniaga HAPA KAZI TU!

Nikaondoka najiskia raha hadi mwenye duka alinipa discount ajili ya story za Tanzani na Magufuli!
 
Muhimbili kuna bonge la jipu. Kuna kipimo cha afya kupima ugonjwa wa Germany Rubella (siijui jobs mashine hiyo) ila wanacho.

Lakini ukienda kupima Germany Rubella unaambiwa hawapimi wao ni mpaka Aghakan au Hindu Mandal. Hivyo inabidi utoe hela 350,000/- au zaidi.

Lakini utafiti wangu unaonesha ni wao wanapima na si Aghakan wala Mandal. Wanakuchukua vipimo na kuambiwa urudi kesho maana vinapelekwa huko. Ukiwapa mgongo wanapima na kutoa majibu.

Hili ni jipu kubwa kwa kina mama wajawazito mimba changa.
 
Kuna dispensary ya serikali ya tegeta kwa ndevu karibu na kituo cha polisi wafanyakazi wanafika saa tatu na nusu wanakuta wagonjwa wako hoi na hata wakifika mpaka wanaanza kutoa hudumu saa nne na nusu ni jipu wazir wa afya tembelea hivi vituo vya afya hasa vya mkoa wa Dar es salaam
 
Hii Dstv chini ya Multi Choice ni ya nani?

Kuna tetesi zimezagaa mitaani kuwa mmiliki au mwenye majority share ni ............ na kwa mamlaka aliyojiwekea serikalini amezuia TV binafsi kuonyesha Premier League na hivyo kuongeza mapato ya serikali.

Natoa wito kwa mtumbua majipu namba moja nchini alimulike suala hili!

Gharama za Dstv zimekuwa kubwa kwa sababu ya urasimu usiokuwa na msingi wowote.

NAWASILISHA!
 
Hospitali ya wilaya Mbambabay Nyasa. Dawa huwa zinafikia hapo lakini ukienda wanasema hakuna dawa.

Cheti kinauzwa tsh elfu sita. Ila maduka ya dawa ya madoktari na manesi hakuna dawa utakayoikosa.
 
Mwanafunzi wa kidato cha nne kujifungulia bwenini ni jipu kwa mkuu wa shule na utawala wake. Angekufa?
 
Wakazi wa Mbagala.

Tunaumia na foleni ambazo kwa mtazamo wangu zinachangiwa na matumizi ya barabara 1 (mtongani).

Kuna haja ya kuwagawa watu wa kijichi kuanzia mtongani na watu wa mbande kuanzia kipati.

Kupunguza msururu wa magar njia moja na mbanano wa abiria kweny gari moja.

Viwango vya nauli.

(Nahisi Sumatra wanaegemea sana kwenye mabasi makubwa lakini viwango vya nauli vya mabasi ya jiji havieleweki hasa kwa wakazi wa Mbagala.

Makondakta wamekuwa wakijiongezea bei za nauli kwa hiari zao wenyewe na kwa shida ya usafiri abilia hawana budi kupanda.
 
Trafiki kuongoza magari ki mazabe..husababisha foleni makusudi ili watu wa bodaboda wapate abiria washukao katika mabasi.

Pia wenye malori hupewa kipaumbele kwani hutanguliza mlungula mbele(Fedha ya kufungua njia ili gari za upande wao zivutwe)...TAZARA kukaa foleni lisaa limoja au zaidi ni jambao la kawaida sana.

DAWA YAKE TAA ZIACHWE ZIFANYE KAZI YAKE KWANNI IMETIMIKA FEHDA NYINGI KUZIWEKA PALE......KAMA VP ZING'OENI TUJUE KIMOJA KWAMBA HAZINA MAANA KWETU.
 
Nakubaliana 100% na mtoa mada na thread hii ibaki ikiwezekana permanent.

Lakini nimesoma response chache hapa chini zipo general, naomba tutoe evidence based majipu.

Kwa mfano wa gari la tanroad ni sahihi kabisa ila angeenda mbali zaidi na kutuo namba. Majipu mengine si ya kutumbua hata mhusika akisoma tu atakuwa na wasisiwasi hajui nini kitafuata lini na ataacha hiyo tabia na hapo tutakuwa wananchi tumemtumbua. Sio lazima kila kitu hata rushwa ya traffic nyiani aitunbue rais.

Mwisho namshauri rais akaimu madaraka ya utumbuaji hata kwa wananchi kwa maana ushahidi akiwa nao mtu aukabidhi kwa boss wa mwenye jipu na copy ikulu. Ole wake sasa asitumbue!!! Anatumbuliwa yeye
 
58 Reactions
Reply
Back
Top Bottom