Tohara kwa Kabila la Wamasai

Tohara kwa Kabila la Wamasai

Mleta mada kuna sehemu umebugi, huenda wewe sio wa kabila hilo, au nikuulize, hayo maelezo umeyatoa ukirefere wamasai wa mikoa IPI?
 
Mleta mada kuna sehemu umebugi, huenda wewe sio wa kabila hilo, au nikuulize, hayo maelezo umeyatoa ukirefere wamasai wa mikoa IPI?
Sehemu gani Mkuu. Sema tu
 
Muendelezo:

Mtaalamu huyu baada ya kumpaka hiyo nduroto huanza kuchonga kwa utaalamu kabisa kwa kurudisha govi huko nyuma mpaka mahali atakapoona panafaa. Kisha huvuta kwa nguvu sana huelekea upande wa magotini. Kisha hupimia kwa kidole na kutoboa kishimo kidogo kwa juu kisha kupitisha dushelele juu yake hivyo kukifanya ile govi kuning'inia kwa chini. Ikishaning'inia kigovi kile hukatwa kwa mbele kidogo. Baada ya hapo hummwagia maziwa pale alipotahiriwa kisha huamshwa.


Baada ya hapo kijana huinuliwa na kuambia ateme mate kama ishara ya kuuaga uvulana na kuukaribisha uanaume. Hapo ndipo mvulana huzichanga karata zake na kuhimiza kutotema mate mpaka apewe ng'ombe.

Kwa mfano,kaka yake atamuambia tema mate nikupe ng'ombe jike,mwingine tema mate nikupe mbuzi,mjomba wake tema nikupe mbuzi jike,mwingine tema nikupe beberu. Baada ya hapo kijana hunyanyuka na kupelekwa ndani kwa mama yake.

Malipo ya Daktari mara nyingi huwa mbuzi au kama vijana wapo wengi hupewa ndama. Kwa siku hizi kwa sababu wamekuwa wa maeneo ya mbali huhitaji pesa taslimu na baada ya hapo huondoka zao. Gharama hutofautiana kutoka mmoja mpaka mwingine.

Daktari hawa huwa hawaishi maisha marefu sana. Hii ni kutokana kuwa wanaamini wanagusa damu nyingi za watu hivyo damu zile huwafatilia. Lakini endapo sehemu kubwa anaowafanyia tohara watashindwa kuhimili maumivu basi anaendelea kupata baraka. Pia malipo ya kijana aliyeshindwa kuhimili maumivu huwa na malipo ya ziada kuliko yule aliyehimili.
 
Duuuuuh hadi nimeogopa jamani!Sio kwa masharti hayo.
Eti hatakiwi kujitikisa...mhhhhh!
Nimewaza tu,hivi baba yangu nae alifanyiwa hivyo?
Ila yeye ni Maasai wa mjini..sidhani.
 
Alifanyiwa Kabisa Nifah. Kama wewe ni mkubwa kwa zaidi ya miaka 25 basi kwa namna yeyote ile atakuwa kapitia hatua hii muhimu sana.

Ukifanikiwa kuhudhuria ndipo utajua kweli hawa ni wanaume.
 
Alifanyiwa Kabisa Nifah. Kama wewe ni mkubwa kwa zaidi ya miaka 25 basi kwa namna yeyote ile atakuwa kapitia hatua hii muhimu sana.

Ukifanikiwa kuhudhuria ndipo utajua kweli hawa ni wanaume.
Miaka yangu ndio hiyo uliyoitaja...hata sijui umejuaje.

Kama atakuwa alifanyiwa jamani aliumia sana...
Ninavyompenda hadi nimeumia na mimi.
 
Miaka yangu ndio hiyo uliyoitaja...hata sijui umejuaje.

Kama atakuwa alifanyiwa jamani aliumia sana...
Ninavyompenda hadi nimeumia na mimi.
Hahaha! Pole sana kwa kuumia. Dingi aligugumia maumivu makali sana. Ila hata hivyo ndiyo maana kapata Mtoto Kisu Nifah...... Hahahahah
 
Ila mkuu c huwa inatokea mtu anatikisika au hata kuliaaa???
Wapo wanaotikisika na kuumia kwa maumivu. Hao hushikiliwa wakimalizwa hupelekwa ndani lakini hudharauliwa sana. Hakika ni fedheha kwa familia nzima.
 
Ni kweli kuwa tohara ya Masai hawatoi ngozi yote, huacha Kipande kining'inie kwa chini ili kuleta raha kwa ile kitu ina run dunia?
 
Back
Top Bottom