Update ya tukio la uonevu kwa kijana Emmanuel Mlimila

Update ya tukio la uonevu kwa kijana Emmanuel Mlimila

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,653
Reaction score
860,941
- Baada ya video ya jiko lile na wanafunzi kusambaa, viongozi wakamkamata, wakamlazimisha arekodi video ya "maelezo ya uongo" ili wamuachie, na video yenyewe ni hii chini

Unyanyasaji na upuuzi wa viongozi na polisi wa eneo hilo, unamuumiza kijana asiye na hatia aliyetaka shule yao isaidike

Soma zaidi...

Kijana baada ya kurekodi ile taarifa na kuisambaza, leo aliitwa ofisi ya kijiji na kuwekwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za kusambaza taarifa ya uongo.

Uongo upoje?
Maelezo ya Mkuu wa shule yanadai kuwa kijana aliwalazimisha wanafunzi wafanye kile kilichoonekana na kurekodiwa kwenye video.

Kijana akiwa katika ofisi ya kijiji cha Lilondo alirubuniwa kuwa akubali maelezo wa Mkuu wa shule ili asamehewe. Kijana kwa tamanio la kupewa msamaha akajirekodi kwa kukiri kuwa ni kweli aliwalazimisha wanafunzi kufanya yaliyofanyika kisha akaomba msamaha. Baada ya kujirekodi na kukiri makosa; Mkuu wa shule akamchukua kijana na kumpeleka polisi na kumfungulia kesi ya kuwalazimisha wanafunzi wafanye igizo la uongo na kusambaza taarifa hiyo ya uongo.

Nini kinaendelea?
Baada ya jitihada nyingi kijana amechukuliwa maelezo na kubaki ndani kwa madai kuwa taarifa zake zimefika mbali hivyo mamlaka ikiwauliza polisi watashindwa cha kujibu. Uzuri kule polisi ametoa maelezo ya kweli. Kwa hiyo dhamana yake imekataliwa.

Tunaomba wanaharakati watusaidie ili aweze kupata msaada wa kisheria kwa kuwa hana mtetezi kabisa...

OMBI
Rais wa TLS, Mheshimiwa Boniface Anyisile Mwabukusi tunaomba mawakili wa TLS walio huko kijana alipo, wamsaidie ili asiendelee kuumizwa isivyo haki!
 
Hii story kama imeanzia njiani. Tunaomba link ya tukio la kwanza.
 
Back
Top Bottom