Tofauti ya watu wa Dar na watu wa mkoani ni hii

ukija mjini tutafutane, fika dar sasa anakuuliza upo wapi ukisema mbezi anakwambia nipo mbagala, siku ukiwa unaondoka utasikia leo ndo nlikua nataka tuonane .
 
Bro njoo kwangu ukija kufata mzigo hutajuta
Mm dar labda niende kufata mzigo wa biashara lkn kukaa kule ata wiki moja uwa naona masaa ayatembei. Uwa nashangaa mtu anakazi yake mkoani ila siku akipata uwamisho wakwenda dar anafurahi kweli wakati mm kama ningekuwa mfanyakazi siku niambiwe naamishiwa dar naweza kabisa kuonga nibaki mkoani.
 
We mdada ni shida sana hata usije mjini kaa hukohuko kwenu
Ni bora nikute vitoto viko bize na gemu kuliko kitoto kinakuja kinaanza kuniambia 'wewe, unaitwa nani?' 'Umekalia kochi letu' 'nenda kwenu'...namtwanga kofi mtoto wa mtu
 
Dar soda xipo kila siku hayo mambo yenu mikoani dar watoto wanakunywa juisi
Watoto wa wenye nyumba huko dar wakiona mgeni umeletewa soda wanaenda jikoni kuchukua kikombe then anakuja hapo mezani ulikoweka hio soda.

Kile kikombe chake anakifanya kama gari(toy) anakua anaendesha kuzunguka meza yenye kinywaji eti njiiiiiiiiiiiiiiiiiimu njiiiiiiiiiiiiiiiiiimu daah inabd umgawie soda tu maana hio ni gia ya kuombea soda.

Fundisheni watoto wenu maadili aiseee
 
kwanza kabisa umeongezea chumvi

hakuna wapiga magoti wakisalimia huko mikoani, labda wale wa vijijini ila wale wa mikoani nao wanaishi mijini hukohuko mikoani hawapigii watu magoti siku hizi

na watu wa dar nao sio malimbukeni kihiivyo kama unavyowasimulia
 
Katiba inasema kila mtu yupo huru ilimradi havunji sheria. Unaweza kusema culture, lakini mambo yanabadilika ila wengine hawabadiliki au wanachukua muda mrefu kubadilika.
Maana yangu ni kuwa kila familia ipo huru kuishi wanavyopenda bila kuingilia ilimradi hawapo evil.
Halafu quick adaptation ni muhimu sana, huyo wa Dar ali-adapt situation ya Dodoma, iweje wa Dodoma ashindwe? Zaidi wa Dar alimwambia wa Dodoma principles zao.
Huyu wa Dodoma ngazi yake ya juu ya elimu ni ipi? Na huyo wa Dar ni ipi?
 
___________________

Umeenda semina Dodoma, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Chamwino shukia St.Gaspar. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".

Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.

Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.

Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".

Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.

Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!

Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"

Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!

Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.

Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba - mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.
Story ya dodoma imenikumbusha nikienda kijijini.. anko analeta na jogooo achinjwe.
 
mnawatembelea vijana ambao hawajaoa
ukija mjini tutafutane, fika dar sasa anakuuliza upo wapi ukisema mbezi anakwambia nipo mbagala, siku ukiwa unaondoka utasikia leo ndo nlikua nataka tuonane .
 
Back
Top Bottom