Utofauti wa watu wa Dar na wa mkoani huu hapa

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Umeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".

Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.

Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.

Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".

Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.

Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!

Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"

Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!

Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.

Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.
 
Yani huu ni ukweli mtupu, naongezea na hii. Mtu wa mkoani akiwa anakuja Dar akiwa njiani tu anaweza kukutaarifu bwana nakuja hukoo.. Jibu utakalo mpa .. aisee karibu bwana ila mi nmepata safari niko Mpanda narudi huko wiki ijayo utakuwepo bado?? Kumbe jamaa upo mjini tu hapa iila hutaki aje kwako. Hizi ni dhambi sana
 
Bro umeongea vitu muhimu, lakini sidhani tena Kama vitakuja kuwa sawa na kuishi maisha ya aina iyo tena ,

Moja ya sababu ni kukua kwa tekinolojia"

huko kijijini unaposema hakuna game, watoto hawana smartphone"

kiufupi havipo vitu vya kuwakeep busy ,

niamini nakwambia mambo haya yanavozidi kuwa hata huko kijijini unaposema ni wakarimu haitakuwa hivyo tena,
hivyo tujiandae tu kuendana na wakati ..
 
Aisee umenikumbusha mbali maisha ya kijijini... Ndugu anakuja kukutembelea karibia nyumba zote za jirani wanajali ujio wako.
 
ni suala la muda hata huko vijijini watabadirika tu, wanaoiendesha dunia wanataka iwe hivyo..

Miaka ijayo mbele hata ukifiwa, hakuna atakayekuja msibani kwako, wewe ni kupiga simu huduma za mazishi na wao wanakuja kuchukua mwili na kwenda kuuzika inakuwa imeisha hiyo, kuoa kuolewa itakuwa hakuna, mnachukuana tu mnakwenda kuishi na mitoto mkishazaa mnapeleka daycare huko, mambo ni mengi sana hakuna namna tukubali tu mabadiriko..
 
ni suala la muda hata huko vijijini watabadirika tu, wanaoiendesha dunia wanataka iwe hivyo..

Miaka ijayo mbele hata ukifiwa, hakuna atakayekuja msibani kwako, wewe ni kupiga simu huduma za mazishi na wao wanakuja kuchukua mwili na kwenda kuuzika inakuwa imeisha hiyo, kuoa kuolewa itakuwa hakuna, mnachukuana tu mnakwenda kuishi na mitoto mkishazaa mnapeleka daycare huko, mambo ni mengi sana hakuna namna tukubali tu mabadiriko..
acha ushamba wewe mambo mengi ndio usahau mpaka ndugu zako.

kama mambo mengi mbona aujawahi kuskip ratiba ya kwenda chooni
 
Back
Top Bottom