tofauti ya tobo na tundu

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,301
520
Wakuu nisaidieni kujua kuna tofauti gani kati ya tobo na tundu haya maneno yananchanganya kuelewa!
 
Hapa unatuyayusha tu,
Nenda jukwaa la Wakubwa ndio utapata majibu sahihi!!
 
Nadhani tundu ndiyo fasaha lakini tobo linaoneka la mitaani labda wali fupisha neno toboa, mfano huwezi sema toboa tobo bali utasema toboa tundu, lakini kwa uhakika zaidi wasiliana na BAKITA
 
"Tobo" linaasili moja na neno "toboa"

Maneno mengi yenye asili moja na "tobo" ni "tobwe", "kitobwe", " kitobo",

Yote hayo yanamaanisha tundu haijalishi kama kubwa au ndogo

Nb: tobwe wakati mwengine hutumika kumaanisha "mtu mjinga au mpumbavu"

"tundu" nayo ina maana ile ile kama "tobo", haijalishi kubwa au ndogo

Nb, neno "tundu" halina asili moja na neno "tundua"

Kwa matumizi ya kila siku watu wengi huita tobo ikiwa tundu ni kubwa na imekosa shape au uwiano,
 
hii inanchangaya sana kuna watu wanaposema kitundu cha ndege na tundu la ndege na pia kitobo je inamaanisha tobo aahhhhh nimestuck
 
Tundu (kitundu, ukiacha 'nyumba' za ndege) - hii sio lazima itokane na kutoboa, inaweza kuwapo kwa asili tu,
Tobo (kitobo) - hii inatokana na kutoboa, kutoboka nk,
Shimo (kishimo) - inaweza kuwa tobo au tundu lakini halitokei upande wa pili wa kitu (aghalabu huwa ni kwenye ardhi)
 
ni kweli tobo na tundu ni vitu viwili tofauti kutegemeana na mahali unapotaka kutoboa tundu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom