Ni ipi tofauti ya masikini na fukara?

Ni ipi tofauti ya masikini na fukara?

Una alufu kumi hapo ili walau ni pate chakula nipate nguvu ya kukueleza jinsi ufukara ulivyo.

Ila umaskini watakueleza walimu.
 
Fukara na maskini ni tofauti sana!!

Ni ipi tofauti?

Kwanza fukara hana pesa wala chakula na haelewi atakula nini.., hata kazi hana chakula labda akaombe kwa jirani kwa kifupi fukara ana hali ngumu

Ni yupi maskini?

maskini
Anaweza kua hana pesa ila ana akiba ndani hata chakula mwezi hata wiki mfano masiki anaweza kua kavuna gunia la mahindi ila akakosa nauli mboga bila mafuta n.k hiyo ndo tofauti

AMBAE ANA SWALI AULIZE?
 
Wakuu kichwa kinajieleza ni ipi tofauti ya masikini na fukara yani ni nani aliye chini zaidi kati ya hao wawili niliowataja hapo juu?

NAWASILISHA:
Fukala yeye hata kupata chakula ni issue ngumu mno
Lakini.
Maskini uwezo wa kula anao lakini kukizi mahitaji mengine ndiyo mtiani
 
Wakuu kichwa kinajieleza ni ipi tofauti ya masikini na fukara yani ni nani aliye chini zaidi kati ya hao wawili niliowataja hapo juu?

NAWASILISHA:
Masikini na Fukara ni watu wawili tofauti kabisa:
Fukara ni mtu ambaye kipato chake (Kiuchumi) hakimtoshelezi kujipatia yale mahitaji ya kimsingi na ya lazma kwa binadamu ili aweze kuishi maisha ya kawaida i.e. apate chakula cha kumtosha yy na familia yake. Hali hii inatokana na na mazingira anayoishi e.g. mazingira hayakumruhusu apate elimu ya kutosha, anashindwa kuyamudu mazingira ya ushindani yaliyopo hivyo maisha yanamwelemea. Ana maisha duni. Huyu akipata mazingira wezeshi anaweza kutoboa.
Masikini ni yule mtu ambaye ana mapungufu kimaumbile e.g. ulemavu; na mapungufu hayo yanakuwa ni changamoto au kikwazo katika kujiendeleza au kumudu kikamilifu mustakabali wa ustawi wa maisha yake. Huyu anakuwa hawezi kukabiliana kikamilifu na changamoto zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali ya kimaendeleo binafsi. e.g. Mlemavu wa ngozi a.k.a. Albino hawezi kumudu kikamilifu kazi zinazomhitaji akae juani kwa muda mrefu, kiwete hawezi kusimamia shughuli zitakazomlazimu kutembea umbali mreefu kwa au yule asiye na mikono kufanya kazi ya kusomba tofali n.k.
Kwa kifupi Masikini ni mtu mwenye limitations kutokana na maumbile yake -Amelazimika kuishi maisha duni aliyonayo e.g. anaomba misaada n.k.
Lakini anamudu kujipatia mahitaji yake ya kila siku - chakula, malazi n.k.
Hivi ndo nionavyo mm.
 
Back
Top Bottom