Tofauti ya nyimbo " chura"(Snura) na "ninasema nae" (Diamond & Hadija Kopa)

Ndiho

JF-Expert Member
Feb 23, 2013
2,306
1,532
Wana Jf, salaam kwenu.
Binafsi napenda kukubaliana na kitendo cha Serikali kupiga marufuku wimbo wa CHURA. Lakini labda ningependa wadau mnisaidie kunifahamisha kama kimaadili kuna tofauti gani kati ya wimbo huo na ule wa Diamond akiwa na Hadija Kopa uitwao NASEMA NAE?
 
Ha ha haaaa. Mleta Uzi umenfurahisha sana Leo, ni kama umeyasemea mawazo yangu na ninaamini kabisa umeona nlichokiona usiku huu.

Mda si mrefu nlikua naangalia wimbo wa Nasema nawe wa Diamond EATV, nkajiuliza mwenyewe the same question.. Ngoja waje wachambuzi wa BASATA watujuze
 
Ha ha haaaa. Mleta Uzi umenfurahisha sana Leo, ni kama umeyasemea mawazo yangu na ninaamini kabisa umeona nlichokiona usiku huu.

Mda si mrefu nlikua naangalia wimbo wa Nasema nawe wa Diamond EATV, nkajiuliza mwenyewe the same question.. Ngoja waje wachambuzi wa Basata watujuze
Hiyo nyimbo ya akina Diamond na Hadija Kopa, director wake ni mwanangu, nilishajiuliza maswali mengi sana juu ya kazi ya mwanangu na vipi anakabiliana na changàmoto za kazi hiyo. Kimantiki hii nyimbo haitakiwi kuwa hewani kwenye jamii yetu
 
Nimeghairi nilichotaka kuandika na nimejikuta.
Next time.
 
Hata Mimi nimeuliza swali hilo hilo muda si mrefu wakati video inachezwa eatv,..nikafikia conclusion kwamba may be ni kwa sababu vyura wanaonekana kwa mbali kidogo na ikiwa close shot haikai sana kulinganisha na snura
 
Tatizo kubwa la chura ya snura ni video yake.Maungo ya kike yaliwekwa mno nje nje!
 
Nsamehe tu ila nakumbuka Siku ile kule stand ya ndege

Hahahahahahahaaaa yaani hadi sauti yako nimeisikia inajirudia tena masikioni mwangu......

Siku ingine nikikuona ntakurusha rusha mwendo wa kichura chura na push ups ndo nakuachia......:p:p
 
Cchura ya snura ni porno kabisaa na hivi sasa wimbo huo unaonekana kwenye website za porno,
 
Hata asanteni kwa kuja imevuka mipaka ya maadili ya tanzania
 
Chura zile inye zko na maji so zinahamasisha zaidi na ukija kwa nasema nawe inye ni kavu halafu hazionyeshwi kwa mda mrefu but zote hazina maadili
 
Back
Top Bottom