Tofauti ya kabila na kabila

Nsibwene

Senior Member
Mar 2, 2017
198
129
Mimi nikiwa nje ya Tanzania najitambulisha kama Mtanzania, maana ndiko baba zangu walitoka au kuzaliwa au kuishi au waliamua wenyewe au mimi mwenyewe kuwa ni nchi yangu. Ukiwa ndani ya Tanzania ni mara chache utaamuliza mtu wewe ni Mtanzania, labda awe wa rangi nyingine unaweza kushuku anatoka nchi nyingine utamuuliza unatoka wapi.

Ukiwa ndani ya Tanzania unauliza wewe ni wa wapi au wazazi wako asili ni wapi. Hospitali wanauliza kabila lako ni lipi.
Ikiwa kwenu mfano Kyela huweza kuuliza wewe ni Mnyakyusa, unauliza ukoo wako ni nani. Kwenye ukoo unaulizwa baba yako ni nani.

Huu ni utambulisho wa kawaida wa kujitambua asili yako. Mtu kujiita Mnyakyusa, Mhaya, Msukuma sio ukabila ni ndiyo asili yake au ya wazazi wake. Hata Nyerere alijijua ni Mzanaki mpaka akatupa maneno ya Kizanaki kama "kung'atuka" alitumia maneno aliyojifunza akiwa mdogo. Kuzungumza lugha ya kabila langu sio ukabila, ni kujivunia utajiri wa lugha niliyozaliwa nayo.

Ukabila ni nini - Ni kupendelea watu wa kabila yako kwenye kuajiri kazi, kutoa misaada. Kwa ufupi ni ubaguzi ambao ulifanyika sana Afrika Kusini. Nikizungumza na mke wangu kilugha changu mbele ya watu sio ukabila kama si msemi mtu ye yote, bali ni mawasiliano ya kuwekana sawa katika mambo fulani.

Hata nizikizungumza lugha ya mama na mtu mwingine mbele ya watu, huenda nataka kuwakilisha jambo fulani ili kumtahadharisha asifanye kosa. Wasomaji wa Biblia hupendelea kutumia lugha nyingi kusoma ilie aelewe nini kimeandikwa ili aweze kuwasilisha vizuri.

Usiache kujifunza lugha y akabila lako, hata kama uliacha ukiwa mdogo. Hakuna lugha bora kuliko nyingine, bali uwingi wa watu wanaozungumza hiyo lugha, ndio inafanya ionekane ya maana.

Sipendi Ukabila bali napenda Kabila ambalo Mungu ameniumba na kunileta kupitia watu hao. Sio aibu wala ushamba, naamini Nyerere hakuchukui Kabila hata mara moja bali alichukia Ukabila. Akafanya makosa kwa kufuta lugha zetu ili tusiongeze utajiri wa kujua lugha na Kiswahili (kina maneno mengi ya lugha zetu).

Kuna ukabila mwingine wa maeneo, kiongozi mkuu amesema hana kabila ni kweli ndivyo alivyokua, lakini ukabila mbaya wa kupendelea eneo.

Hata yeye akiwa bara anajiita Mzanzibari akienda Zanzibar atajitambulisha zaidi Mpemba au Muunguja. Atazidi kujitambulisha kuwa anatoka Tumbatu au Kojani.

Kwa sisi wenye Makabila tunajitambulisha kwa kabila, eneo halina mshiko mzuri kuliko kabila. Wasio na kabila wanajitambulisha kwa eneo. Kama utajiita Mtemeke, au Muilala ni juu yako.

Sina maana kwamba yeye anapendelea hivyo, ila viongozi wengine wengi ndivyo walivyo kupendelea maeneo yao. Angalia bajeti za serikali ni maeneo gani ambayo miundombinu inakimbizana kwa kasi bila kujali maeneo mengine.

Katika mkakati wa Tanroads ni kujenga "Trunk Roads" zote nchi nzima. Sasa wanawaza kujenga barabara mbili kwenye njia ambazo tayari zina barabara za lami wakati kwingine huko hawana hata barabara moja ya maana. Huo ni unini?

Umewahi kusikia barabara ya Ifakara - Malinyi - Songea iko kwenye mkakati wa kujengwa tangu lini, hakuna dalili za kujengwa.

Barabara ya kutoka Itigi -Rungwa - Makongolosi, na ile Tabora - Ipole-Rungwa- Makongolosi na Ile Tabora -Ipole -Mlele.

Ziko kwenye makakati wa kujengwa miaka zaidi ya 20, ila miradi mingine pesa inapatikana kiurahisi tu ya kujengea. Kulikoni. Nani atasimama kwa ajili ya maeneo hayo? Nani?

Hapo ukichukulia eneo lako na ukalipendelea kulika eneo lingine huo ni ukabila wa aina yake, nao ni mbaya ni sawa mtu anayependelea watu kabila lake pasipo sababu. Pia kuwepo kabila katika nchi hakutasha kesho ni baada ya miaka sana ijayo.

Mwisho nasema Kabila sio Ukabila ila mtu ye yote anaweza kuwa na ukabila wo wote anaoamua kufuata.
 
Basi sawa! Ila kwa sasa uvumilie kidogo maana kuna mtanange mkali unaendelea huko uwanjani kati ya Wakojani vs Sukuma Gang!

Na mchezo unakaribia kabisa kuisha, huku timu isiyo fungika kirahisi ya Sukuma Gang katika hali ya kushangaza kabisa, wako nyuma kwa goli 3 kwa 0 dhidi ya timu dhaifu ya Wakojani.
 
Back
Top Bottom