Tofauti na mfanano wa kikazi na kimamlaka kati ya CIA na FBI

Habari chiefs,

Hope mko poa na mishemishe zinaenda. Niende kwenye topic moja Kwa moja, ningependa kufahamu nini tofauti iliyopo Kati ya hizo taasisi mbili za kiintelejensia zinazo operate ndani ya nchi moja. Utendaji, mamlaka na je zinawajibika kwenye idara au wizara tofauti?
No hayo tu karibuni wajuvi wa mambo..
FBI inaanza na herufi ya F na CIA inaanza na herufi ya C. Kwenye CIA herufi inayofuata ni I wakati FBI inafuata B. Halafu FBI inamaliza na I wakati CIA inamaliza na A.

Hiyo ndiyo tofauti MKuu.
 
CIA ni shirika la kijasusi la Marekani lenye jukumu kuu la kukusanya taarifa za kiusalama kimataifa kuhusu Taifa lao katika nyanja zote muhimu kama vile kiuchumi, kisiasa nk

Makao makuu ya CIA yapo katika jengo la The George Bush Centre of Intelligence huko katika viunga vya Langley, Virginia. Makao hayo makuu yamepewa jina la aliyekuwa Mkuregenzi Mkuu wa CIA aliyekaa madarakani kwa muda mfupi sana na ambaye baadae alikuja kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha muhula mmoja, George H.W. Bush (Bush Mkubwa)

FBI ni shirika la upelelezi la Marekani lenye jukumu kuu la kufanya upelelezi na kusimamia usalama katika nchi ya Marekani.
FBI huingia jimbo lolote bila kizuizi katika ufanyaji wao wa kazi tofauti na wale askari wa majimbo.

Makao makuu ya FBI yapo katika jengo la Edgar Hoover huko jijini Washington. Makao makuu hayo yamepewa jina la muasisi wa FBI na Mkurugenzi pekee aliyekaa madarakani kwa muda mrefu bwana John Edgar Hoover.
 
Ahaa kwa maana hyo CIA wana deal na international intelligence huku FBI waki operate ndani ya nchi pekee
CIA Hawaruhusiwi kisheria kufanya kazi ndani ya USA , FBI wanafanya kazi ndani ya USA tu au katika special occasion pale wanapoitwa ku provide utaalamu
 
Shukrani mkuu hyo ya ku operate kwenye balozi zote za USA naweza changia Kwani Kwa mujibu wa sheria za kimataifa za UN... ardhi majengo na mali za ubalozi wa nchi X zilizopo ndani ya nchi Y ni mali ya nchi X.. Hata eneo la bahari ambalo si eneo la bahari ya kimataifa ndani ya nchi Y linalokaliwa na meli inayopeperusha bendera ya nchi X ni eneo la bahari la nchi X.. Hivyo pale msasani US EMBASSY ni eneo ndani USA bado wako ndani ya USA naanza concept.
Ila practically CIA wanafanya kazi ndani ya Marekani pia
Kumbuka pia wako above FBI

FBI wanamandate ya Marekani nzima na kwenye balozi zote za Marekani dumiani utawakuta FBI hata Dar walikuja 98
 
Secret service ni kikosi cha ulinzi wa viongozi wakuu wa serikali ya Marekani.
Mpaka 1997, marais wote wa zamani, na familia zao, walikuwa wanalindwa na Secret Service mpaka kifo cha rais.

Rais wa mwisho kuwa na ulinzi wa Secret Service maisha ni Bill Clinton; George W. Bush na baadae marais wote watakuwa wanalindwa na Secret Service kwa upeo wa miaka kumi baada ya kuachia ofisi.
 
FBI inaanza na herufi ya F na CIA inaanza na herufi ya C. Kwenye CIA herufi inayofuata ni I wakati FBI inafuata B. Halafu FBI inamaliza na I wakati CIA inamaliza na A.

Hiyo ndiyo tofauti MKuu.
Duuuu nimecheki kwa sauti
 
Back
Top Bottom