Precise Pangolin
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 12,998
- 6,659
Punguza jazba bro, we utakuwa CDM unaandamana hadi kwenye maoni.
Wewe gamba ndio mmetufikisha nyamaza!!!
Punguza jazba bro, we utakuwa CDM unaandamana hadi kwenye maoni.
Katika kufanya tafiti ya jumla nimegundua moja ya tofauti kubwa kati ya Mwafrika na Mzungu ni kwamba, Sisi waafrika tuna ungana na kushirikiana zaidi kimwili wakati wenzetu wanashirikiana na kuungana zaidi kimawazo na kiakili.
Mzungu akipata elimu, ataandika vitabu ili mwenzake asome aendeleze pale yeye alipo ishia, ataunganisha mawazo yake na ya mwenzake wataunda ama watatengeneza kitu au machine fulani. Ndiyo maana utakuta kifaa kimoja kimetengenezwa na watu wa fani mbalimbali ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Wazungu hawashirikiani kimwili zaidi, ni vigumu kukuta wanapelekeana mialiko kama ya kitchen party au misiba, ni vigumu kujua jirani yake ni nani na anafanya nini. Hata akitoka out na girlfriend wake, kila mtu anatalipia bili yake kwa mfuko wake. Harusi zao hazikusanyi watu wengi na kutumia siku nzima wakila na kunywa labda awe ni mtu maarufu sana!
Sisi waafrika hatuko pamoja kiakili, hata mtu akiwa nawazo zuri kivipi, litadharauliwa na kila mtu kubaki na mambo yake. Tumekuwa wajinga wa kuwa achia wanasiasa kutuamulia nini cha kufanya na nini tusifanye hata kwenye mambo ya kisayansi na utafiti kwa mambo ya kawaida. Wasomi wazuri hawatungi vitabu bali wanakimbilia kwenye siasa, sii ajabu ukakuta profesa haandika kitabu chochote kwa miaka 20 na bado anajiita Profesa!
Waafika tunashindwa kuunganisha tafiti za kisayansi za fani mbalimbali ili kupata kitu bora kwa matumizi ya kila siku na tumebaki kununua vilivyotengenezwa na wazungu. Watunga sera wamekuwa wakidharau hata mawazo ya wengine na kuona ya wazungu ndo bora kuliko ya mwafrika mwenzao. Lakini likija swala la kuzikana, harusi na mengi yanayofanana na hayo, utakuta waafrika wamerundikana utafikiri wana umoja wa kweli!
Punguza jazba bro, we utakuwa CDM unaandamana hadi kwenye maoni.
na wewe unaishia kumwambia mwenzako analalamika badala kusema nini kifanyike!
mkuu, kabla hatujaendelea na mchango wa uzi wako, naomba ufafanuzi toka kwako. Mzungu ni mtu wa aina gani?
Wewe unafikiri kila mtu mweupe ni mzungu?
Umetumia njia zipi za kitafiti (research methodology) au ni kwa mujibu wa maoni yako!
Usitake kupandikiza udhaifu waku Binafsi kwa watu wengine!
Mkuu, hilo la Maprofesa wetu hawawezi kuandika vitabu ikiwa lengo letu ni kuwa kama Ulaya ndio maana tunatumia vitabu vya Ulaya zaidi. Wakiandika vitabu vinavyohusiana na mazingira yetu wananchi hawavitaki isipokuwa vile vilivyoandikwa na wazungu kwa sababu sisi tunataka kuwa kama wao na sii sisi kama sisi..tatizo hapa kuna watu wako huku kwa ajili ya kupinga hoja za wengine,,, kimsingi hata kama mtu kaleta hoja menzani ni vyema ukamcritisize kwa kutoa arguments zenye mashiko ili ajifunze kupitia wewe... kimsingi ninaueshimu mchango wa mwanajamii MKANDARA maana amejielekeza kutoa argument yenye mantiki....
ninamuunga mtoa hoja kwa sababu zifuatazo:
1. je tanzania tuna maprofesa wanagapi? nafikiri ni wengi lakini kila siku wadau wa elimu wanalia kuwa hakuna vitabu vya kutosha, sasa utaniambia kuwa maprofesa wamefanya kazi ya kutunga vitabu.... na hii inatokana na maprofesa wetu kuwa affected na mfumo wa kisiasa
2. mtanzania ukimwambia akuchangie ili ukasome sahau kabisa lakini ukimwambia ni sherehe basi hata laki kadhaa anatoa? maana yake hatuthamini maendeleo ya wenzetu kwa uoga wa kuzzidiwa na hoja ya kwanini nimsaidie mtu ambaye si ndugu yangu... kwa maana nyingine sisi ni wabinafsi wa maendeleo
zingine zitafuata hapo baadae
Refer the following case study;
American Presidency vs. Tanzanian Presidency, majibu yote utayapata.
Samaki hawezi kuzaa nyoka, vivyo hivyo jinsi Rais alivyo na Taifa lake vivyo hivyo kwa vile Rais ametoka kwenye jamii hiyo hiyo! Thanks!
Mkuu, hilo la Maprofesa wetu hawawezi kuandika vitabu ikiwa lengo letu ni kuwa kama Ulaya ndio maana tunatumia vitabu vya Ulaya zaidi. Wakiandika vitabu vinavyohusiana ana mazingira yetui wananchi hawavitaki isipokuwa vile vilivyoandikwa na wazungu kwa sababu sisi tunatakja kuwa kama wao na sii sisi kama sisi..
Kwa hiyo ndio maana utasikia shule haina vitabu vya kusomea na tunaletewa misaada kutoka nje na NGOs. Na ndio maana tumeshindwa, tumeshindwa kuelekeza nguvu zetu kufanikisha mahitaji yetu krk mazingira tuliyopo isipokuwa kuichubua Afrika iwe kama Ulaya sawa na mawazo ya mdada anayejichubua ngozi ili awe mweupe!..Hivyo, sabuni isiyochua ngozi haina soko.
Nakubaliana na hiyo tofauti lakini tufanye ni ni?????????
Your Thread is Lacking the Following:
- Relevance,
- Comprehensiveness, and
- Reference.
Hao wanathibitisha jinsi waafrika tulivyo!