Tofauti kubwa ya Mwafrika na Mzungu

Nashukuru kwa michango yenu. Hebu fikirieni sayansi zetu zilivyodumaa zikibaki ni wazo la mtu yule yule mwanzilishi bila wataalamu wengine kuunganisha utaalamu wao ili bidhaa iwe bora zaidi.

1. Mtungi-Mtungi wa kuwekea maji ya kunywa aliye utengeneza mpaka leo haujaongezewa utaalamu na makundi mengine, umebeki vile vile!
2. Kinu-Kinu cha kutwangia mpaka leo ni cha vile vile hakuna tecknolojia iliyo ongezeka.
3. Chungu-Chungu cha kupikia hakija ongezewa utaalamu wowote!

Wanao pinga ukweli huu siwashangai kwani wanakamilisha utafiti wangu. Walete mifano inayotuonnyesha kuwa sisi waafrika tunashirikishana kiakili.
 
Nafikili tofauti kubwa ambayo huhitaji kufanya utafiti ni kwamba waafrica ni WEUSI na wazungu ni WEUPE.
Kafanye tafiti zenye manufaa kwenye jamii sio hizi zisizo na mantiki

Wapo waafrika wasio weusi, mfano nchi nyingi za kaskazini mwa afrika ni waarabu weupe lakini siyo wazungu. Au unaposema mwafrika una maana ni wale weusi tu? Nijuavyo mimi kuna waafrika weupe wengi tu, hata hapa kwetu Tanzania kuna baadhi ya makabila watu wake ni weupe lakini si wazungu. Au unaposema waafrika una maana wenye nywele nyembembe zinzokunjamamna (curl)?
 
mkuu, kabla hatujaendelea na mchango wa uzi wako, naomba ufafanuzi toka kwako. Mzungu ni mtu wa aina gani?
Wewe unafikiri kila mtu mweupe ni mzungu?

Kama mpaka leo hujui mzungu ni mtu wa aina gani, basi kwenye mfumo wetu wa elimu nchini kuna mushkeli. Sikulaumu wewe kwa kushindwa kuelewa mzungu ana sifa gani mpaka akaitwa mzungu, bali nailaumu serikali ya CCM kwa kuweka mitaala mibovu ya elimu mpaka mtanzania anashindwa kutofautisha races za binadamu.

Kama umeshindwa kujua mzungu ni mtu wa namna gani, je mwafrika mwenzako akikwambia "mtanzania ni mtu wa aina gani"? utasemaje?
 
Punguza jazba bro, we utakuwa CDM unaandamana hadi kwenye maoni.

Tunapokataa ukweli na kutafuta ku-cover mapungufu yetu, hakuta saidia kitu zaidi ya kuachwa mbali kimaendeleo. Hasa wanao kataa kuambiwa ukweli ni CCM ambapo baadaye wanakubali bila kuchukua hatua ya maana. Mfano; Wana CCM walikataa hakuna pesa zilizoibwa kwa mgongo wa EPA, baadaye walikubali, walikataa CCM hakuna mafisadi, baadaye walikubali na wameshidwa kujivua gamba, Walikataa hatuli mapanki, nenda kanda ya Ziwa ushudie, Walisema Mramba ni mtu safi, siku si nyingi wakampeleka mahakamani. Walisema Richmond ikianza uzalishaji umeme, mgao utakuwa historia lakini sasa kuna mgao huku mikoani balaa! Nk.
 
sasa yeye amecheza upande wake, sasa ni kazi yako wewe kuongeza hao wengine uliowaona wewe!

Adoe hajui maana ya tafiti, anafikiri tafiti inachukua kila kitu. Tunarudi palepale, Adoe anadhilihisha uafrika wake, badala aendeleze nilipoishia mimi yeye anaponda utafiti wangu. Mwache ndo uafrika huo "hatushirikiani kiakili lakini nikimwambia achangie harusi ya Mkuu wa Chuo atatoa laki!
 
Huo útafiti umeufanyia wapi?

Sijaufanyia sayari nyingine ni hii hii Dunia ndo wanapatikana waafrika na wazungu. Katika nchi za kiafrika na za wazungu nilizotembelea kila race inatabia zinazofanana sana. Kama huwezi safiri basi tazama hata filamu zao utajua mila na desturi zao linganbisha naza kwako.
 
yaani hapa mshaonyesha uafrika wenu,jamaa kaongea point nzuri hapa lakini nie badala ya kuongelea hoja mmeingiza maswali ya ajabuajabu na ubishi wenu baada ya kuvimbiwa wali maharage

Hao wanathibitisha jinsi waafrika tulivyo!
 
Anko Sam nakubaliana na wewe kabisa lakini kama we umegundua hilo ni hatua gani ulishachukua kwa either kuandika kitabu and so forth.....

Namalizia utafiti wangu, utafiti siyo kitu cha siku moja bali ni mchakato wa muda kidogo. Pia hii thread ni moja kudadisi kama waafrika tunakubali mapungufu yetu ama tunakataa, na kwa asilimia ngapi? Kisha nta-compile ili nitoe mbadala wa nini kifanyike.
 
Mtoa hoja yuko sawa kwa maana ya generalization (mzungu) na Mwafrika (ngozi nyeusi) hasa mtanzania.Nadhani ameeleweka kwani angeanza kumtaja Mchina,Mkorea, Mkambodia ama Mtridad pengine angetuchanganya na kutupa maswali mengi zaidi ya haya.

Isipokuwa changamoto ya Mzungu ni kuwa asili yake Uingereza, huko Marekani na asia wnawaita English man/men/woman. Ndio maana mtu akikwambia ongea kizungu- tafsiri yake ni kingereza na wala si Kijerumani wala Kipakistani.Nadhani tupo sawa hapa.
 
Daah, nakpongeza xana mtoa mada bt watz 2kiendlea kukalia kupngapnga tu kla ki2 2tabweteka na umaskin we2!Utafit utafit gan mnautaka?Twachen mawazo pevu au ndo wiv usomana?Hoja ipo imara,2seme 2fanye nin na hli tatzo la MFUMO make ndo mpango mzma!
 
Katika kufanya tafiti ya jumla nimegundua moja ya tofauti kubwa kati ya Mwafrika na Mzungu ni kwamba, Sisi waafrika tuna ungana na kushirikiana zaidi kimwili wakati wenzetu wanashirikiana na kuungana zaidi kimawazo na kiakili.

Mzungu akipata elimu, ataandika vitabu ili mwenzake asome aendeleze pale yeye alipo ishia, ataunganisha mawazo yake na ya mwenzake wataunda ama watatengeneza kitu au machine fulani. Ndiyo maana utakuta kifaa kimoja kimetengenezwa na watu wa fani mbalimbali ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Wazungu hawashirikiani kimwili zaidi, ni vigumu kukuta wanapelekeana mialiko kama ya kitchen party au misiba, ni vigumu kujua jirani yake ni nani na anafanya nini. Hata akitoka out na girlfriend wake, kila mtu anatalipia bili yake kwa mfuko wake. Harusi zao hazikusanyi watu wengi na kutumia siku nzima wakila na kunywa labda awe ni mtu maarufu sana!

Sisi waafrika hatuko pamoja kiakili, hata mtu akiwa nawazo zuri kivipi, litadharauliwa na kila mtu kubaki na mambo yake. Tumekuwa wajinga wa kuwa achia wanasiasa kutuamulia nini cha kufanya na nini tusifanye hata kwenye mambo ya kisayansi na utafiti kwa mambo ya kawaida. Wasomi wazuri hawatungi vitabu bali wanakimbilia kwenye siasa, sii ajabu ukakuta profesa haandika kitabu chochote kwa miaka 20 na bado anajiita Profesa!

Waafika tunashindwa kuunganisha tafiti za kisayansi za fani mbalimbali ili kupata kitu bora kwa matumizi ya kila siku na tumebaki kununua vilivyotengenezwa na wazungu. Watunga sera wamekuwa wakidharau hata mawazo ya wengine na kuona ya wazungu ndo bora kuliko ya mwafrika mwenzao. Lakini likija swala la kuzikana, harusi na mengi yanayofanana na hayo, utakuta waafrika wamerundikana utafikiri wana umoja wa kweli!
Ni mada nzuri tu hiii ikiwa tunataka kujifunza kufahamu mapungufu yetu ambayo hayatokani na maumbile bali FIKRA...

Kweli zipo tofauti nyingi tu baina na mzungu na mwafrika (mtu mweusi) na nakubaliana na maneno yako uliposema - "Katika kufanya tafiti ya jumla nimegundua moja ya tofauti kubwa kati ya Mwafrika na Mzungu ni kwamba, Sisi waafrika tuna ungana na kushirikiana zaidi kimwili wakati wenzetu wanashirikiana na kuungana zaidi kimawazo na kiakili."

Lakini haya ni matokeo tu ya kihulka ambazo zimetokana na neno moja kubwa sana - UTAMADUNI.. Waafrika kwa ujumla wetu tumepoteza Utamaduni wetu na kujaribu kuiga wa mzungu ambaye mambo yote anayoyafanya ni kutokana na MAHITAJI yake yeye. Hivyo mzungu anakwenda shule kusoma ili kupata elimu yakumwezesha kukabiliana na matatizo ktk mazingira yake nasi weusi kwa kuiga tunakwenda shule ili kujifunza mbinu za kukabiliana na matatizo ya mzungu badala ya matatizo yetu.

Sasa kwa nini tunashirikiana zaidi kimwili, Ni kwa sababu hatuna ufumbuzi wa matatizo yetu hivyo nguvu ya pamoja ambayo haihitaji elimu ndio hutumiwa kama mbadala ya mahitaji ambayo tumeyaiga kwa mzungu. Haya ya Kitchen Party tumeyaiga na kuyachukua kama yalivyo wakati hayakuwa ktk mahitaji yetu isipokuwa maadam wazungu wanafanya basi nasi tukaiga mila zao ili tuonekane tumeendelea.

Tatizo la waafirka halipo kabisa ktk unyonge ama uhafifu ktk maumbile bali tatizo la mwafrika ni kupoteza UTAMADUNI wake, mila na desturi ambazo zinamfanya yeye awe tofauti na mzungu ktk mazingira anayoishi. Tunataka kuibadilisha Afrika iwe kama Ulaya ambayo kila kitu kilichoijengwa kimetokana na mahitaji ya sehemu zao. Tena kama ingewezekana kukata rufaa kwa Mwenyezi Mungu basi tungeoma atupe hata barafu (Snow) na baridi kama la Ulaya, atupe season nne kama ulaya na kadhalika.

Tumeisha poteza Lugha, mavazi, nyimbo na ngoma zetu na sasa tumeiga hadi jinsi ya kujitawala badala yake tumeiga kila kitu kutoka kwa masters wetu kiasi kwamba leo hii tunabishana juu ya vazi la Taifa ati kuna watu wanataka KUVUMBUA vazi la Taifa..na linavumbuliwa kwa sababu tunaklihitaji au kwa sababu na sisi tuonekane tuna utamaduni?.. nani anayevumbua vazi hilo? msanii ambaye hana asili ya Uafrika wala sii mwana historia isipokuwa wamechaguliwa watu kulingana na utamaduni wa mzungu.

Kwa hiyo sii kwamba kushindwa huko kunatokana na rangi ya ngozi isipokuwa kushindwa huko kunatokana na KUTAWALIWA na ndio maana wasomi wenye kuelewa maana husema Umaskini wetu unatokana na KUTAWALIWA..na vijana wa siku hizi wasomi walioshiba mila na desturi za wazungu hushindwa kuelewa kwa nini mtu mweusi husingizia UKOLONI kama sababu ya umaskini wake ili hali akiendelea kutazama mafanikio na mahitaji ya mzungu kama kielelezo cha mwafrika kuweza kufanikiwa pia.

Mzungu ana deal na matatizo yake kwa imani ya kwamba - Necessity is the mother of invention, sisi hatulisomi neno hilo kwa maana ile ile maana elimu tulosoma haihusiani kutazama mahitaji yetu kama neccesity bali tuna DEMAND ya vitu vya Ulaya hivyo tunacho kihitaji ni Supplier ili tuwe sawa na mzungu.

Afrika tuna matatizo ya maji safi toka enzi za nabii Nuhu ingawa maziwa na mito ipo lakini hadi leo tatizo hilo lipo na halijawahi kupatiwa ufumbuzi mahala popote, mazao ya chakula ni shida toka enzi za Azania tukipigana vita kutafuta ardhi kubwa ya kilimo lakini hatujawahi kupata ufumbuzi ktk kilimo na kuondoa njaa hadi imekuwa moja ya identity na mazingia yetu. AFRIKA = UKAME!
 
Tunapokataa ukweli na kutafuta ku-cover mapungufu yetu, hakuta saidia kitu zaidi ya kuachwa mbali kimaendeleo. Hasa wanao kataa kuambiwa uk
weli ni CCM ambapo baadaye wanakubali bila kuchukua hatua ya maana. Mfano; Wana CCM walikataa hakuna pesa zilizoibwa kwa mgongo wa EPA, baadaye walikubali, walikataa CCM hakuna mafisadi, baadaye walikubali na wameshidwa kujivua gamba, Walikataa hatuli mapanki, nenda kanda ya Ziwa ushudie, Walisema Mramba ni mtu safi, siku si nyingi wakampeleka mahakamani. Walisema Richmond ikianza uzalishaji umeme, mgao utakuwa historia lakini sasa kuna mgao huku mikoani balaa! Nk.


Mzee swala la kukataa ukweli haliko CCM pekee, njoo na hoja ya ukweli kukosoa chama chetu chenye mlengo wa kulia katikati utakumbana na masaburi ya kufa mtu mpaka utakimbia jamvi.

Rejea katika mada yako ya Uzungu na Uafrika lakini kama utachanganya hapa ni dhahiri utatuaminisha ya kuwa uliposema Mwafrika ulikuwa unamaanisha CCM na wala sio Mtu mweusi.Kama mtoa hoja epuka biasness ili kuruhusu mjadala unoge na sio itikadi (U-ccm na U-cuf au U-cdm).
 
Katika kufanya tafiti ya jumla nimegundua moja ya tofauti kubwa kati ya Mwafrika na Mzungu ni kwamba, Sisi waafrika tuna ungana na kushirikiana zaidi kimwili wakati wenzetu wanashirikiana na kuungana zaidi kimawazo na kiakili.

Mzungu akipata elimu, ataandika vitabu ili mwenzake asome aendeleze pale yeye alipo ishia, ataunganisha mawazo yake na ya mwenzake wataunda ama watatengeneza kitu au machine fulani. Ndiyo maana utakuta kifaa kimoja kimetengenezwa na watu wa fani mbalimbali ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Wazungu hawashirikiani kimwili zaidi, ni vigumu kukuta wanapelekeana mialiko kama ya kitchen party au misiba, ni vigumu kujua jirani yake ni nani na anafanya nini. Hata akitoka out na girlfriend wake, kila mtu anatalipia bili yake kwa mfuko wake. Harusi zao hazikusanyi watu wengi na kutumia siku nzima wakila na kunywa labda awe ni mtu maarufu sana!

Sisi waafrika hatuko pamoja kiakili, hata mtu akiwa nawazo zuri kivipi, litadharauliwa na kila mtu kubaki na mambo yake. Tumekuwa wajinga wa kuwa achia wanasiasa kutuamulia nini cha kufanya na nini tusifanye hata kwenye mambo ya kisayansi na utafiti kwa mambo ya kawaida. Wasomi wazuri hawatungi vitabu bali wanakimbilia kwenye siasa, sii ajabu ukakuta profesa haandika kitabu chochote kwa miaka 20 na bado anajiita Profesa!

Waafika tunashindwa kuunganisha tafiti za kisayansi za fani mbalimbali ili kupata kitu bora kwa matumizi ya kila siku na tumebaki kununua vilivyotengenezwa na wazungu. Watunga sera wamekuwa wakidharau hata mawazo ya wengine na kuona ya wazungu ndo bora kuliko ya mwafrika mwenzao. Lakini likija swala la kuzikana, harusi na mengi yanayofanana na hayo, utakuta waafrika wamerundikana utafikiri wana umoja wa kweli!
Nakushauri uliangalie hili kimfumo zaidi kuliko rangi(race) ya watu.
 
Namalizia utafiti wangu, utafiti siyo kitu cha siku moja bali ni mchakato wa muda kidogo. Pia hii thread ni moja k
udadisi kama waafrika tunakubali mapungufu
yetu ama tunakataa, na kwa
silimia ngapi? Kisha nta-compile ili nitoe mbadala wa nini kifanyike.

Kama utafiti wako utaishia humu JF (data collection) basi jiandae kuwa na poor analysis kwani kwa sehemu kubwa wako ki-ideology hasa ki-vyama na wewe ni miongoni mwao.Maake huwezi kuja na conclusion ya chama kimoja eti hakikubali ukweli kisha eti unafanya utafiti (hii itakua imposition) hali ya kuwa majibu unayo.
 
Mzungu ni mtu yeyote ambaye si mwafrika. Mfano Obama, Whitney Houston, Oprah Winfrey na wengine.

Moja ni identity ya mtu kutokana na rangi yake (mzungu) na nyingine ni identity ya mtu kutokana na mahali anapaoishi(mwafrika). Labda mtoa mada angesema mweusi na mzungu, au mwafika na mtu wa Ulaya, au mwafrika na mmarekani. Na hata waafrika wanatofauti sana, si kila mwafrika ni ovyo kama "mtanzania", na sila m'ulaya ni bora kuliko mtanzania.

It is more comlicated than that. Tembea uone utakuja kuona kuwa, ile Tanzania ifanane na Ulaya inahitaji watu 500 tu makini na wakweli. Ulaya wana watu kama hao (bila kujali rangi zao), Marekani wanao watu kama hao(bila kujali rangi zao au wanatoka wapi.
 
Daah, nak
pongeza xana mtoa mada bt watz 2kiendlea kukalia kupngapnga tu kla ki2 2tabweteka na umaski
n we2!Utafit utafit gan mnautaka?Twachen mawazo pevu au ndo wiv usomana?
Hoja ipo imara,2seme 2fanye nin na hli tatzo la MFUMO make ndo mpango mzma!

Mzee umeandika ki-facebook sikuelewi maake namba na maneno.Huu sio uharibifu wa lugha huu?
 
Nafikili tofauti kubwa ambayo huhitaji kufanya utafiti ni kwamba waafrica ni WEUSI na wazungu ni WEUPE.
Kafanye tafiti zenye manufaa kwenye jamii sio hizi zisizo na mantiki

MSISITIZO: yes Waafrica ni WEUSI WA NGOZI mbaya
zaidi akiwa mweusi from BRAIN to SKIN to assholes, kama ni skin color only doesn't make a difference, na kuna wazungu WEUPE from SKIN to assholes but WEUSI ktk BRAIN, hawa pia wapo,...So hawa waafrika na wazungu niliyowataja hawana tofauti mentally of which color is nothing
 
Nafikili tofauti kubwa ambayo huhitaji kufanya utafiti ni kwamba waafrica ni WEUSI na wazungu ni WEUPE.
Kafanye tafiti zenye manufaa kwenye jamii sio hizi zisizo na mantiki

Tofauti yako imekaa kizuzu zuzu, yani inaonyesha ni jins gani hupendi na huwezi kufikiria
 
Back
Top Bottom