Tofauti kubwa ya Mwafrika na Mzungu

Anko Sam

JF-Expert Member
Jun 30, 2010
3,200
820
Katika kufanya tafiti ya jumla nimegundua moja ya tofauti kubwa kati ya Mwafrika na Mzungu ni kwamba, Sisi waafrika tuna ungana na kushirikiana zaidi kimwili wakati wenzetu wanashirikiana na kuungana zaidi kimawazo na kiakili.

Mzungu akipata elimu, ataandika vitabu ili mwenzake asome aendeleze pale yeye alipo ishia, ataunganisha mawazo yake na ya mwenzake wataunda ama watatengeneza kitu au machine fulani. Ndiyo maana utakuta kifaa kimoja kimetengenezwa na watu wa fani mbalimbali ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Wazungu hawashirikiani kimwili zaidi, ni vigumu kukuta wanapelekeana mialiko kama ya kitchen party au misiba, ni vigumu kujua jirani yake ni nani na anafanya nini. Hata akitoka out na girlfriend wake, kila mtu anatalipia bili yake kwa mfuko wake. Harusi zao hazikusanyi watu wengi na kutumia siku nzima wakila na kunywa labda awe ni mtu maarufu sana!

Sisi waafrika hatuko pamoja kiakili, hata mtu akiwa nawazo zuri kivipi, litadharauliwa na kila mtu kubaki na mambo yake. Tumekuwa wajinga wa kuwa achia wanasiasa kutuamulia nini cha kufanya na nini tusifanye hata kwenye mambo ya kisayansi na utafiti kwa mambo ya kawaida. Wasomi wazuri hawatungi vitabu bali wanakimbilia kwenye siasa, sii ajabu ukakuta profesa haandika kitabu chochote kwa miaka 20 na bado anajiita Profesa!

Waafika tunashindwa kuunganisha tafiti za kisayansi za fani mbalimbali ili kupata kitu bora kwa matumizi ya kila siku na tumebaki kununua vilivyotengenezwa na wazungu. Watunga sera wamekuwa wakidharau hata mawazo ya wengine na kuona ya wazungu ndo bora kuliko ya mwafrika mwenzao. Lakini likija swala la kuzikana, harusi na mengi yanayofanana na hayo, utakuta waafrika wamerundikana utafikiri wana umoja wa kweli!
 
Nafikili tofauti kubwa ambayo huhitaji kufanya utafiti ni kwamba waafrica ni WEUSI na wazungu ni WEUPE.
Kafanye tafiti zenye manufaa kwenye jamii sio hizi zisizo na mantiki
 
mkuu, kabla hatujaendelea na mchango wa uzi wako, naomba ufafanuzi toka kwako. Mzungu ni mtu wa aina gani?
Wewe unafikiri kila mtu mweupe ni mzungu?
 
we mchizi unavyoandika hivyo utafikiri ulikwisha fanya utafiti wenye manufaa! Hebu leta na wewe utafiti wako tuone! Mwenzako ameumiza kichwa kufikiri.
 
Mzungu ni mtu yeyote ambaye si mwafrika. Mfano Obama, Whitney Houston, Oprah Winfrey na wengine.
 
we mchizi unavyoandika hivyo utafikiri ulikwisha fanya utafiti wenye manufaa! Hebu leta na wewe utafiti wako tuone! Mwenzako ameumiza kichwa kufikiri.

Ameumiza kichwa wapi wewe! Yaani ktk sayari hii ameona Wazungu na Waafrika tu?
 
yaani hapa mshaonyesha uafrika wenu,jamaa kaongea point nzuri hapa lakini nie badala ya kuongelea hoja mmeingiza maswali ya ajabuajabu na ubishi wenu baada ya kuvimbiwa wali maharage
 
Acheni kudis kila kitu bali inabidi kutafakari yale yaliyo ya muhimu ktk ujumbe na kuyafanyia kazi pia na kwa yale yaliyo so ya muhimu dawa ni kuyaignore.
 
Mkuu, ni vizuri kabla ya kuendelea na topic ni vizuri kuwekana sawa. Utakuwa wa ajabu mtu kama Osama kumuita mzungu kwavile tu ni mweupe, au Hillary Clinton kuwa ni mzungu wakati ni Mmarekani, au David Cameroon kuwa ni Mmarekani wakati ni Mzungu!
 
Katika kufanya tafiti ya jumla nimegundua moja ya tofauti kubwa kati ya Mwafrika na Mzungu ni kwamba, Sisi waafrika tuna ungana na kushirikiana zaidi kimwili wakati wenzetu wanashirikiana na kuungana zaidi kimawazo na kiakili.

Mzungu akipata elimu, ataandika vitabu ili mwenzake asome aendeleze pale yeye alipo ishia, ataunganisha mawazo yake na ya mwenzake wataunda ama watatengeneza kitu au machine fulani. Ndiyo maana utakuta kifaa kimoja kimetengenezwa na watu wa fani mbalimbali ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Wazungu hawashirikiani kimwili zaidi, ni vigumu kukuta wanapelekeana mialiko kama ya kitchen party au misiba, ni vigumu kujua jirani yake ni nani na anafanya nini. Hata akitoka out na girlfriend wake, kila mtu anatalipia bili yake kwa mfuko wake. Harusi zao hazikusanyi watu wengi na kutumia siku nzima wakila na kunywa labda awe ni mtu maarufu sana!

Sisi waafrika hatuko pamoja kiakili, hata mtu akiwa nawazo zuri kivipi, litadharauliwa na kila mtu kubaki na mambo yake. Tumekuwa wajinga wa kuwa achia wanasiasa kutuamulia nini cha kufanya na nini tusifanye hata kwenye mambo ya kisayansi na utafiti kwa mambo ya kawaida. Wasomi wazuri hawatungi vitabu bali wanakimbilia kwenye siasa, sii ajabu ukakuta profesa haandika kitabu chochote kwa miaka 20 na bado anajiita Profesa!

Waafika tunashindwa kuunganisha tafiti za kisayansi za fani mbalimbali ili kupata kitu bora kwa matumizi ya kila siku na tumebaki kununua vilivyotengenezwa na wazungu. Watunga sera wamekuwa wakidharau hata mawazo ya wengine na kuona ya wazungu ndo bora kuliko ya mwafrika mwenzao. Lakini likija swala la kuzikana, harusi na mengi yanayofanana na hayo, utakuta waafrika wamerundikana utafikiri wana umoja wa kweli!

Anko Sam nakubaliana na wewe kabisa lakini kama we umegundua hilo ni hatua gani ulishachukua kwa either kuandika kitabu and so forth.....
 
Back
Top Bottom