Tofauti kubwa kati ya Ke/Me ni kwamba "mwanamke ana roho mbaya na mwanaume ana roho ngumu"

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
6,661
20,995
Kichwa cha habari kinajieleza,

Ukifuatilia matukio mengi maovu ya kiubinadamu utagundua kuna tofauti kubwa ya utekelezwaji kati ya yale yaliyotendwa na mwanamke na yaliyotekelezwa na mwanaume.

Sifa ya kwanza ya mtu mwenye roho mbaya ni unafiki na sifa ya kwanza ya mtu mwenye roho ngumu ni ujasiri, pili sifa nyingne iliyopo kwenye kivuli cha unafiki ni uoga.

Ukichunguza utagundua ya kua mtu mwenye roho mbaya ni mwoga na ndo maana analazimika kua mnafiki kuficha maovu yake na sifa ya pili ya mwenye roho ngumu ni kutojali/ogopa.

Tuangalie mfano mwanamke akitaka kufanya mauaji labda kwenye familia yake, atafanya hivyo lakini atafanya kwa njia ambayo hatataka kujulikana, mfano anataka kuua familia basi atatia sumu kwenye chakula halafu atajitia anakula na nyie(unafiki) mkizidiwa anajua kabisa haponi mtu anapiga mayowe kuita majirani na kwenye kesi akihojiwa tu anaanza kulia(unafiki grade A)

Je ushawahi sikia mwanaume anatia sumu kwenye chakula? Mwanaume anacharanga panga wote mkiwa mnamwangalia halafu anatia kwenye kiroba anazika(roho ngumu).

Ukamletea mwanamke mtoto wa kambo hatakataa kuishi nae ila anachomfanya pindi haupo, ndo yale unaskia kalazmishwa kula kinyesi chake au mkojo, kachomewa madaftari, kanyimwa chakula, kachomwa na pasi, kafungiwa ndani n.k.

Halafu anatishiwa ole wako mtu ajue, baba akija anacheka na wewe(unafiki), ushasikia mwanaume anamnyima mtoto wa kambo chakula au kumlisha kinyesi? Labda ndio je mara ngapi? Mwanaume atakuambia wazi waz sitaki mtoto wa kambo(roho ngumu) nayo ni mara chache.

Wanaume kuongoza kua wengi gerezani si kwamb a wao ni waovu sana kuzidi wanawake, kuna wanawake wengi sana wanapaswa kua kule ila unafiki ndo unawabakiza majumbani.

Jumapili njema, ni mawazo tu na kumbuka hii si kwa wote ke/me, za kuambiwa changanya na zako.

Call me: Mr symbian.
 
Sii kweli mkuu kila binadamu ameubwa na sifa ya wema ila kinachotokea MTU akafanya jambo baya tambua sii yeye bali shetani yupo nyuma yake ndo maana akishatekeleza lile jambo adui anaondoka anabaki yeye ndani ya majuto makubwa.
 
Wa kwanza siti ya mbele

Mkuu huu uzi wako umemgusa jirani yangu mmoja wa kiume yeye alimwambia mke wake sitaki mtoto wa kambo yule mama alipo goma alitimua wote hivyo nakubaliana na wewe

Wengine wako church wasubili watakuja
 
nakubaliana kabisa wanawake wana roho mbaya.matukio meng yakunyanyasa watoto yapo kwa kina mama.wanaume ni majasiri na roho ngumu.
 
na ndo wanaongoza kwa mahudhurio huko
Wa kwanza siti ya mbele

Mkuu huu uzi wako umemgusa jirani yangu mmoja wa kiume yeye alimwambia mke wake sitaki mtoto wa kambo yule mama alipo goma alitimua wote hivyo nakubaliana na wewe

Wengine wako church wasubili watakuja
 
Kichwa cha habari kinajieleza,

Ukifuatilia matukio mengi maovu ya kiubinadamu utagundua kuna tofauti kubwa ya utekelezwaji kati ya yale yaliyotendwa na mwanamke na yaliyotekelezwa na mwanaume.

Sifa ya kwanza ya mtu mwenye roho mbaya ni unafiki na sifa ya kwanza ya mtu mwenye roho ngumu ni ujasiri, pili sifa nyingne iliyopo kwenye kivuli cha unafiki ni uoga.

Ukichunguza utagundua ya kua mtu mwenye roho mbaya ni mwoga na ndo maana analazimika kua mnafiki kuficha maovu yake na sifa ya pili ya mwenye roho ngumu ni kutojali/ogopa.

Tuangalie mfano mwanamke akitaka kufanya mauaji labda kwenye familia yake, atafanya hivyo lakini atafanya kwa njia ambayo hatataka kujulikana, mfano anataka kuua familia basi atatia sumu kwenye chakula halafu atajitia anakula na nyie(unafiki) mkizidiwa anajua kabisa haponi mtu anapiga mayowe kuita majirani na kwenye kesi akihojiwa tu anaanza kulia(unafiki grade A)

Je ushawahi sikia mwanaume anatia sumu kwenye chakula? Mwanaume anacharanga panga wote mkiwa mnamwangalia halafu anatia kwenye kiroba anazika(roho ngumu).

Ukamletea mwanamke mtoto wa kambo hatakataa kuishi nae ila anachomfanya pindi haupo, ndo yale unaskia kalazmishwa kula kinyesi chake au mkojo, kachomewa madaftari, kanyimwa chakula, kachomwa na pasi, kafungiwa ndani n.k.

Halafu anatishiwa ole wako mtu ajue, baba akija anacheka na wewe(unafiki), ushasikia mwanaume anamnyima mtoto wa kambo chakula au kumlisha kinyesi? Labda ndio je mara ngapi? Mwanaume atakuambia wazi waz sitaki mtoto wa kambo(roho ngumu) nayo na mara chache.

Wanaume kuongoza kua wengi gerezani si kwamb a wao ni waovu sana kuzidi wanawake, kuna wanawake wengi sana wanapaswa kua kule ila unafiki ndo unawabakiza majumbani.

Jumapili njema, ni mawazo tu na kumbuka hii si kwa wote ke/me, za kuambiwa changanya na zako.

Call me: Mr symbian.

Duh! Ni ajabu sana Mama yako aliyekulea, kwenda kliniki kila siku ili tuwe uweze kuwa na afya njema leo hii unamuita ana roho mbaya, halafu unategemea kufanikiwa Dunia hii?
 
Sii kweli mkuu kila binadamu ameubwa na sifa ya wema ila kinachotokea MTU akafanya jambo baya tambua sii yeye bali shetani yupo nyuma yake ndo maana akishatekeleza lile jambo adui anaondoka anabaki yeye ndani ya majuto makubwa.
Nilitegemea rejection hapa,alichozungumzia mtoa mada ni uhalisia kabisa tena 100% Yani msipende kumuhukumu shetan vingine ni hulkaa na natural,jumapil njema
 
Hakuna binadamu aliyezaliwa na roho mbaya , roho inakuja kutokana na mazingira na hii kwa wote waume na wanawake.
 
Duh! Ni ajabu sana Mama yako aliyekulea, kwenda kliniki kila siku ili tuwe uweze kuwa na afya njema leo hii unamuita ana roho mbaya, halafu unategemea kufanikiwa Dunia hii?
Barbarosa mbona jamaa kaielezea vizuri sana bila kuweka bias na mwishoni katoa angalizo!.
Juwa kujenga hoja sio Viroja!, binafsi nakubaliana na mtazamo wake wanawake wana roho mbaya na wanaume tuna roho ngumu.
Mimi nikitaka fanya jambo baya nahakikisha nalifanya mhusika ujue nimelifanya tuone utafanyaje, lakini wanawake wana roho mbaya atalifanya kwa siri/au kwa kuzunguka zunguka mpaka ukija tambua kalifanya unaanza juta kwanini hukujua mapema!.
Nice sunday!.
 
Lkn Mama yako si ni Mwanamke? Pia ana roho mbaya?
 
asante Palantir, mkuu barbarosa huwez kufanikiwa kwa kumsifu mama hata kama anatenda maovu, hembu chuku mfano(ni mfano ulio hai maana tunayaona kbsa yakitokea katka maisha) mama yako anamnyanyasa ndugu yako wa damu mlieshare baba(mtoto wa kambo) wazi wazi, hv utamsifu ana roho nzuri kisa anakupendelea wewe, na ukimkosoa hutafanikiwa? Haya basi umemsifu mama kwa maovu akakubariki huku Mungu na kiumbe chake wakakulaani unategemea nini? Ninachojua na kuamin mimi n kwamb muheshm mama upate heri na maisha meng duniani, suala la kufanikiwa ni pana sana kana kwamb kila mtu ana mtizamo wake cha msing utafte mafanikio kwa njia iliyo safi, haya mambo yapo tunayaona au kuskia kila siku. Mwisho kbsa nimesema si kwa wote ndugu
 
Lkn Mama yako si ni Mwanamke? Pia ana roho mbaya?
Acha kukwepa ukweli.kwani akiwa mama au shangaz ndio itapunguza roho mbaya? Anaweza kua ni mama yako mzazi na bado akawatendea ubaya wengine.au utasema hujawahi ona kitu kama hiko? Kuzaa hakuondoi roho mbaya.wanawake acheni tabia ya kinafik..mkiambiwa ukweli mnajitetea eti tumezaa!
 
Ni wapi nimekwepa huo unaouita ukweli? Nimeuliza kama Mama yako mzazi ana roho mbaya, jibu ni ndiyo au hapana!
 
Back
Top Bottom