Tofauti kati ya wanawake wa Mkoa na jiji hasa Dar

Tofauti kati ya wanawake wa Mkoa na jiji hasa Dar

Nuran Jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2017
Posts
273
Reaction score
234
Habari za muda huu wana jamvi,

Leo nimekuja na mambo kadhaa kuhusiana na tofauti kati ya wanawake wa jiji la Dar na mikoa mingine japo hao waliopo Dar nao wanatoka mikoa tofauti ikiwemo mikoa ambayo nimekuwa nikifanya shughuli zangu.

Kwa experience yangu ndogo ya kuishi jiji la Dar kwa takribani miaka7 sasa nimepata ufumbuzi kuwa kunatofauti kubwa sana kati ya wanawake wanaoishi jiji la Dar na mikoa michache ambayo nimezunguka kwa ajili ya kutafuta chochote kitu, hii nimeanzia kufanya uchunguzi tangu nikiwa nasoma chuo pale mlimani nitaziainisha tofauti hizo kama ifuatavyo;

1.Wengi wao wanaishi maisha ya kuigiza wakati wa mkoa wako real maana yangu ni kuwa wanawake wa Dar wanaishi maisha ya maigizo hasa kwenye social medias ukimkuta instagram na maisha yake halisi ni tofauti kabisa anapolala, chakula anachokula ni tofauti na kile tunachokiona akipost.

2. Wengi wao wamekosa mwelekeo wa maisha hivyo wanaishi maisha ya mizinga, wengi wanakwenda Dar bila kuwa na enough information kuhusiana na jiji la Dar labda awe mzawa au wazazi wake wapo Dar hivyo mambo yakiwashinda wanaogopa kurudi mkoa kutokana na maisha magumu yaliyopo mikoa yao husika au familia za hali ya chini.

3. Wengi wao wamekata tamaa kutokana na kutokuwa na shughuli za kufanya either kwa kutokuwa na elimu ya kutosha au kutokuwa na mahitaji ya kutosha, wengi wao wameshajikatia tamaa ndio maana maeneo ya kujiuza hawakosekani na hili linasababisha wao kujiweka cheep kwenye maeneo ya kujiuza wakati mwanamke wa mkoa hata akiuza mboga mboga hana shida na anaweza kuendesha maisha yake safi.

4. Ugumu na gharama kubwa ya maisha ya jiji la Dar, zinawafanya wajiweke expensive kwa wanaume ili waweze kuyamudu maisha, ndio maana msemo wa mwanaume pesa sura tutavumilia nahisi ulitokana na hili wengi tunajua ili uishi Dar lazima uwe na pesa ya kutosha, vinginevyo utaishia kuabika na mkoa ulishaaga kwamba unaenda kutafuta kwa wanaume huwa sio shida sababu mwanaume kulala kwenye mabox pale Ubungo haoni shida ila katika pitapita sijawahi kumuona mwanamke amelala sehemu za nje labda akeshe kwa Kimboka, Manzese na maeneo mengine maarufu ya kujiuza wao wanayajua zaidi.

6. Hawadumu kwenye mahusiano kutokana na kuwa tegemezi kwa 250% kutoka kwa mwanaume, wanawake wengi wa jiji la Dar ni tegemezi sana ukimtongoza na kuanza naye mahusiano anabadirika kuwa yatima, yani case zote zinaenda kwa mwanaume, sikatai kuwa mwanaume anatakiwa amuhudumie mwanamke lakini atleast ujiongeze ili upunguze majukumu mengine ya mwanaume sasa wao wakishaingia kwenye mahusiano tu wanakuwa wafanyakazi wawe wanalipwa mishahara afu mbaya zaidi unakuta hata elimu au kujiongeza hawezi kwa maisha haya bila hivyo unakaribisha umaskini.

NB; Haya ni machache niliyayaona kwa miaka michache ya kuishi kwa jiji la Dar wakati natafuta mwenzi wa maisha nikaamua nijitose tu mkoa kwenye chimbuko lake hasa, sio wanakoishi maisha ya maigozo sijasema kuwa hawafai kuolewa, la hasha!Sababu mapenzi ni hisia.
 
We huwajui wa mkoani naona,,, km umesoma chuo na binti wa mkoani ndo utanieleewa. Wa dar hawana mashauzi km wa mkoa,,,utuache wanawake wa dar,,
 
Mbona mkitoka mkoani mnawaacha wanawake wa mkoani mnakuja kuoa Dar?? Sizitaki mbichi hizi
 
Watakuja wenyewe kujitetea...

Mimi naona ni mikoa yote tu, siyo Dar peke yake...

Hao hao wa mikoa mengine nao wana act kama wapo Dar..

Cc: mahondaw
 
CD ya Dar vs Mkoani ishapitwa na wakati....
 
Back
Top Bottom