Tofauti kati ya Rais Magufuli na Rais Mstaafu Kikwete

TWisheshagi

Member
May 2, 2020
14
209
Tofauti kubwa Kati ya Rais Mstaafu Kikwete na Rais Magufuli ni kwamba JK alikuwa akisema hatendi, na akitenda hasemi! JPM yeye anasema kila kitu, na anatenda kila kitu!

Ukifuatilia hotuba za Mkuu, mambo mawili unabaini: Mosi, unatamani uingilie Kati hotuba yake ili umuokoe au usahihishe anachokisema kabla hakijafika kwa umma lakini unashindwa. Unabaki unaumia ndani kwa ndani kwa kushindwa kuokoa jahazi! Pili, unabaini kuwa, siku hizi ubabe unaitwa ujasiri, na uoga na ukimya umegeuzwa kuwa busara na hekima na kusifia na kujipendekeza umegeuzwa kuwa uzalendo!

Leo nikomee hapo, mimi bado mgeni kwenye Familia hii!
 
Sema wapinzani wa tanzania ni ngumu kuwaelewa

It is never too late to begin. Start now
 
Yaani mimi leo nilikuwa natamani niingie kwenye ubongo wake. By the way mambo ya Mbuzi wangeyamaliza wao huko. Sasa kaleta taharuki tu. Watu hata wakiwa positive watahisi vipimo vimedanganya. Na kuendelea kujichanganya mitaani. Na hivi hakuna cha karantini tena.
 
Hii kauli ya kwamba vipimo vina mashaka, tafsiri yake ni kwamba hakuna haja yakwenda hospital kupima. Bora tuendelee na nyungu na mitishamba. Watu hawaamini tena huduma za hospitali
Yaani mimi leo nilikuwa natamani niingie kwenye ubongo wake. By the way mambo ya Mbuzi wangeyamaliza wao huko. Sasa kaleta taharuki tu. Watu hata wakiwa positive watahisi vipimo vimedanganya. Na kuendelea kujichanganya mitaani. Na hivi hakuna cha karantini tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikwete ni bingwa wa demokrasia na mliberali haswa. wakati wapinzani wakiongea hisia zao dhidi yake tena majukwaani yeye alikuwa akiijenga nchi kwa barabara safi ma madaraja ya uhakika kama lile la Kigamboni. jiji la dar es salaam lilisimikwa maghorofa na maghorofa enzi za Mzee Kikwete na ajira kwa wahitimu zilikuwepo.

Huyu wa sasa yupo busy kununua na kuwatisha wanaompinga na miradi mingi kaibuni kwa hisia huku akisahau kuwa unaweza kuwa kuwa na wazo la kujenga miradi mikubwa lakini kama huna mikakati ni kazi bure. miaka mitano imeenda bure.
 
Anajenga mikubwa ya kimkakati

1.SGR
2.Stiglers HEP
3.Vituo vya Afya 370
4.Hospitali za Wilaya 67
5.Flyover-Dsm, madaraja mf.surrender, busisi n.k
6.Viwanja vya ndege
7.Ununuzi wa ndege
8.Uboreshaji mikataba ya madini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikwete alianza ari mpya nguvu mpya akaja malizia akili ya kuambiwa changanya na za kwako.
Magufuli yeye alianza kwa push up,sijui atamalizia kwa kungu fu?
 
Tofauti kubwa Kati ya Rais Mstaafu Kikwete na Rais Magufuli ni kwamba JK alikuwa akisema hatendi, na akitenda hasemi! JPM yeye anasema kila kitu, na anatenda kila kitu!

Ukifuatilia hotuba za Mkuu, mambo mawili unabaini: Mosi, unatamani uingilie Kati hotuba yake ili umuokoe au usahihishe anachokisema kabla hakijafika kwa umma lakini unashindwa. Unabaki unaumia ndani kwa ndani kwa kushindwa kuokoa jahazi! Pili, unabaini kuwa, siku hizi ubabe unaitwa ujasiri, na uoga na ukimya umegeuzwa kuwa busara na hekima na kusifia na kujipendekeza umegeuzwa kuwa uzalendo!

Leo nikomee hapo, mimi bado mgeni kwenye Familia hii!
Siyo kwamba unelishwa block ukajivua gamba
 
Kikwete ni bingwa wa demokrasia na mliberali haswa. wakati wapinzani wakiongea hisia zao dhidi yake tena majukwaani yeye alikuwa akiijenga nchi kwa barabara safi ma madaraja ya uhakika kama lile la Kigamboni. jiji la dar es salaam lilisimikwa maghorofa na maghorofa enzi za Mzee Kikwete na ajira kwa wahitimu zilikuwepo.

Huyu wa sasa yupo busy kununua na kuwatisha wanaompinga na miradi mingi kaibuni kwa hisia huku akisahau kuwa unaweza kuwa kuwa na wazo la kujenga miradi mikubwa lakini kama huna mikakati ni kazi bure. miaka mitano imeenda bure.
Kikwete ni bingwa haswa
 
Back
Top Bottom