Tofauti kati ya kuitika Beee na Eeee ........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tofauti kati ya kuitika Beee na Eeee ........

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by KipimaPembe, Nov 5, 2011.

 1. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wakati wa uchumba na miaka michache ndani ya ndoa wife wangu nikimuita alikuwa akiitika Beeee .... ikifuatiwa na smile. Miaka kama saba na kuendelea ndani ya ndoa kila nikimuita anaitika Eeeee ..... ikifuatiwa na kunyanzi usoni.

  Sasa nikimsikia kwenye simu anaitika Beeeeee .... nieleweje?? JF tusaidiane!
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Elewa kuna watu pembeni kaona asiwape faida :]

  or maybe

  Anakupenda zaidi ukiwa mbali naye :]]
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  mie hata sikumbuki mama ngina huwa anaitikaje nikimuita, ngoja nifanye utafiti...........................
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mzee usishangae sena, mwanamke ukisha muoa ni kama mkubwa mwenzio sasa hiyo mishikamoo unayoitakaa au hiyo beeee itakusaidia nini. Wapo ambao walikuwa wanapigiwa magoti lakini sasa hivi hakuna cha shikamoo wala magoti. Sana sana akijitahidi akuite dear, maana kutamka mpenzi kwa kiswahili ni ngumu kinoma. Au pengine kisha kuzoea sana na kwa kuwa anajua huna lolote la maana zaidi ya kujambajamba usiku unapokuwa usingizini tu.

  Na hii ndiyo maana hata umasaini mzee wa miaka hata 70 akishaoa katoto hata kakiwa ka mika 18, basi huyo binti anahesabiwa kama ni mzee pia hivyo hata namna ya kusalimia wazee wa rika la mumewe, yeye anawasalimia kama wazee wenzake, si kaolewa na mzee mwenza naye pia ni wa riak lao hata kama miaka yake ni 18.

  La muhimu mnaheshimiana ktk mapenzi yenu na ndani nyumba
   
 5. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Gaijin,

  Hiyo beee ya kwenye simu siyo mie ninayeitikiwa; ila ni mpigaji simu mwingine! Mie nikipiga simu naitikiwa Eeeee
   
 6. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  I like this!!!
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ni hivyo?

  Elewa kuwa wewe keshakuzowea sana, kachoka kutumia "formalities" wakati huyo anaemuitikia Beeee bado kuna ukuta mzito wa formality umewatenga :]]
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Heheheh...jamani yani mpaka Eeeeh na Beeeh unavitilia wasiwasi???
  Ulishasema zamani alikua anaitika Beeh na kutabasamu ..that means alikua anafurahia ukimwita...ulikua bado hujamchosha.
  Sasa hivi ukimwita tabasamu halipo kwasababu inawezekana unamsumbua sana...kumwiita ita kila saa na kutaka akusikilize bila kujali kama ana shughuli nyingine au la. Kama anafanya shughuli nyingine jaribu kua wewe ndio unamfuata badala ya kumtaka yeye akufuate....au kama unahitaji kitu nenda kachukue mwenyewe au tuma watoto umpe break...unaweza kushangaa beeeh inarudi!!

  Kuhusu kutumia beeeh kwenye simu inawezekana ni kwasababu kwenye simu halazimiki kwenda/sogea popote kwahiyo kuitwa kwenye simu hakumkeri.
   
 9. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  OK, kumbe beee ina aina fulani ya u-formality?
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...okey, kwani nawe ulikuwa unamuitaje
  • kipindi cha 'fungate'...
  • miaka saba na ushee iliyofuatia..
  ...isijekuwa nawe umebadilisha 'tone' jinsi unavyomuita
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mhhh..inawezekana kweli nae kabadili namna ya kuita ila hajaona ...kaona tu mabadiliko ya mwenzake.
   
Loading...