Tochi ya kumulika magari almanusura isababishe ajali Korogwe

papaa masikini

Senior Member
Mar 5, 2011
176
69
Tabia ya trafiki,wanaotumia tochi ku record mwendo wa magari,imeendelea kushika kasi,baada ya leo trafic aliyekuwa amejificha chini ya mwembe kuibuka ghafla nakuzua tafrani kwa mabasi ya Ngorika na Kilimanjaro yliyokuwa yanaongozana,ambapo basi la ngorika limeligonga basi la kilimanjaro kwa nyuma,
Wakati huo huo basi la Kirumo limeligonga gari ndogo aina ya toyota Rav4.
Magari yote yamefikishwa kituo cha police nakuachiwa kuendelea na safari.
Katika matukio yote hakuna aliyejeruhiwa.
 
kama sikosei hapo ni kabuku-Tanga......wana mchezo mchafu sana wale maafande
 
Hivi si majuzi tu yule mtoto wa mkulima tumesikia akisema kuwa hao tigo wa tochi wakome kujificha vichakani na kuwataka wakae kwenye vituo vyao? Ina maana tuamini kuwa kwa sasa kila mtu anatawala kwa amri na kanuni yake?
 
Hizo tochi hazina ushaidi wowote mahakani. Walishawahi nikamata nikawatimulia vumbi
 
Kuna li-dada limoja pale limenenepeana! Mi nilimpa live, nikamwambia rushwa zitawamaliza! Aliniambia nisimame na sikusimama, nikasepa zangu! Yaani wanaboa sana, na huu ndio haswaaaaaa msimu wao wa kuvuna!
 
Hivi si majuzi tu yule mtoto wa mkulima tumesikia akisema kuwa hao tigo wa tochi wakome kujificha vichakani na kuwataka wakae kwenye vituo vyao? Ina maana tuamini kuwa kwa sasa kila mtu anatawala kwa amri na kanuni yake?

prblm hii nchi kila kitu kinaenda kisiasa!
 
Yaani hawa trafiki huwa wananishangaza sana. Kujificha inamaanisha ni kumuacha mtu atende kosa halafu upate sababu ya kumkamata/kumtoa pesa.
Hawafanyi preventive measures, wanafanya detective measures.
Ni sawasawa na mtu asubiri abakwe ili apate ushahidi wa mahakamani wakati alikuwa na nafasi ya kupiga kelele/kukimbia!
 
ni kutokusimama tuu kama mimi
hata hapa dar ile vizia vizia yao ooh tumakagua sijui fire sisimami kukaguliwa veta au usafirishaji stoop.
 
Ni jana nikiwa safarini kutokea Mbeya ndo tumevuka Iringa kidogo baada ya Police check, aliibuka traffic kichakani akiwa na tochi lake hilo, nusra asababishe ajari ktk mabasi yalokuwa yametufuata ya NGANGA'S na Summry, .....
kweli hawa traffic wanahitaji kupewa elimu kuhusu hizi tochi na kama sio wanavyozitumia kama vyanzo vya mapato yao
 
Nikikiwaza hicho kitendo chao chakujificha nabaki nacheka sana kha
 
Hivi si majuzi tu yule mtoto wa mkulima tumesikia akisema kuwa hao tigo wa tochi wakome kujificha vichakani na kuwataka wakae kwenye vituo vyao? Ina maana tuamini kuwa kwa sasa kila mtu anatawala kwa amri na kanuni yake?
hawajapokea barua rasmi kiongozi!!!
 
ni kutokusimama tuu kama mimi
hata hapa dar ile vizia vizia yao ooh tumakagua sijui fire sisimami kukaguliwa veta au usafirishaji stoop.
hivi hawa jamaa wa fire wapo!!!nikilipia road licence mwaka huu walikata hadi hela ya fire lakini sikuambiwa nikachukue wapi stika!!!kurudi tena sikukumbuka!
 
Yaani hawa trafiki huwa wananishangaza sana. Kujificha inamaanisha ni kumuacha mtu atende kosa halafu upate sababu ya kumkamata/kumtoa pesa.
Hawafanyi preventive measures, wanafanya detective measures.
Ni sawasawa na mtu asubiri abakwe ili apate ushahidi wa mahakamani wakati alikuwa na nafasi ya kupiga kelele/kukimbia!

Mkuu kama ulivyosema hizi tochi hazifanyi kazi iliokusudiwa zinatumika kama chanzo cha mapato
 
Back
Top Bottom