Yaani tusiingize magari kutoka nje ya Nchi?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Polisi wakamata magari 96 ya wizi

Na Romana Mallya

28th May 2009

headline_bullet.jpg
Mengi ni aina ya Toyota Land Cruiser na Rav4
headline_bullet.jpg
44 yameibwa Japan, chassis namba zimefutwa



MAgari.jpg

Magari.

JeshiI la Polisi Nchini kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) wamekamata magari 96 ya ya wizi ya aina mbalimbali katika operesheni iliyofanyika katika mikoa kadhaa nchini.

Kati ya magari hayo, 34 yamebainika kuwa chassis na namba za injini zake zimevurugwa wakati magari 57 na pikipiki 57 yaligunduliwa kuibwa katika nchi saba.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Peter Kivuyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mkurugenzi wake, Robert Manumba.

Kivuyo alisema kati ya magari hayo, 44 yameibiwa Japan, sita Afrika Kusini, matatu yameibiwa Uingereza wakati magari mawili yaliibiwa Slovenia.

Alisema gari moja limegundulika kuibiwa Namibia na lingine liliibwa Marekani.

Sambamba na hilo alisema wamefanikiwa kuzikamata pikipiki nne ambazo ziliibiwa Kenya.

Alisema msako huo ambao pia ulifanywa kwa kushirikiana na nchi za Burundi na Rwanda na wadau wengine kama Idara ya Uhamiaji na ya Wanyamapori ulifanyika kuanzia Mei 21, hadi 22 mwaka huu.

Aliitaja mikoa iliyokuwa imepewa kipaumbele zaidi katika operesheni hiyo kuwa ni Arusha, Mbeya, Mwanza, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Mara, Dar es Salaam na Zanzibar.

Kivuyo alisema baada ya kukamilika operesheni hiyo juzi, kamati ya uchunguzi ilianza kazi mara moja makao makuu ya polisi kwa kuyapitia majalada yote na vielelezo vilivyopatikana katika msako huo.

Aidha, Kamanda Kivuyo alisema katika uchunguzi wao wataangalia magari yaliyokamatwa yaliingizwaje nchini.

Alisema uchunguzi huo utazihusisha balozi zote ambazo magari hayo yanadaiwa kuibwa.

Aliongeza kuwa Japan kwa hivi sasa, wanafanya utafiti ili kubaini magari yao yaliibiwaje na kwa njia zipi.

Alitaja baadhi ya magari yaliyokamatwa katika operesheni hiyo kuwa ni pamoja na Toyota Saloon, Toyota Rav 4 na Land Cruiser na amewataka wananchi ambao hununua magari, kabla ya kufanya hivyo, waende ofisi ya Interpol makao makuu ya polisi ili yakaguliwe.

"Operesheni hii ni ya kudumu, hivyo, ninawaomba wananchi kabla ya kununua magari wafike ofisini kwetu kwanza ili gari liweze kufanyiwa uchunguzi kama ni la wizi au la, kwani watu huyaagiza kwa njia za mtandao au kutumia mawakala na njia nyingine," alisema...

CHANZO: NIPASHE




Wiki ilopopita nilsimamishwa na askari wa trafiki, ni magari mengi yalikuwa yanasimamishwa na kukaguliwa. Nilijua kuwa tumeingiliwa na Polisi wa Kimataifa (Interpol) maana si mara ya kwanza kufanyika ukaguzi mkali wa magari ambapo magari yanosyosimamishwa hukaguliwa namba za injini na chesisi.

Habari kuwa magari kadhaa yamekamatwa kwa kuhisiwa kuwa yaliibiwa na kuingizwa kutoka nje ya nchi si ngeni ingawa mwaka huu idadi imekuwa kubwa. Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) amesema kuwa magari hayo yaliyoingizwa Tz kutokea Japan na nchi nyingine yaliibiwa!

Amekaririwa akitoa woto kwa wanaoagiza magari kwa njia ya mtandao kutoka Japan au nchi nyinginezo ati waende Interpol Kinanchonishangaza ni kuwa kabla ya gari kusajiliwa ni lazima lipitue polisi kwa ukaguzi na tunajua kuwa Polisi wana mtandao mkubwa ukiwamo huo wa Interpol. Sasa linapokuja suala la mtu akitaka kununua gari aulizie Interpol na alikague chasis na engine namba (raia wa kawaida ni vigumu sana hata kujua hizo namba ziko sehemu gani kwenye gari) ni unyanyasaji wa hali ya juu na ni ukwepaji wa majuku kwa upande wa Polisi wetu.

Nijuavyo mimi kabla Japan hawajasafirisha gari kuja huku kwetu lazima gari hilo lipate deregistration certificate na kukaguliwa na JAAI kwa niaba ya TBS, sasa iweje mlaji ndiyo aingizwe kwenye tuhuma na kupoteza gari lake? Huu ni uonevu.

Nimeshasikia tetesi huko nyuma kuwa kule Afrika Kusini mgeni anayetaka kuhamisha gari nje ya Afrika Kuaisni anauziwa gari kwa beii chee sana (muuzaji anakuwa amesalikatia comprehensive insurance) na baada ya muuzaji kuhakikisha kuwa gari limeshatoka nje ya nchi huenda kuripoti Polisi kuwa ameibiwa gari ili alipwe na Insurance!

Nasema tena kuwa kwa Polisi wetu kuwatwisha wanaonunua magari kutoka Japan na nje ya nchi (ukiondoa nchi za Jirani) ni uonevu mkubwa. Wangapi wanaweza kununu magari mpaya ili kuepuka usumbufu huo?
 
mie nadhani sisi wanunuzi ndio tuwe makini sana tukinunua gari kuepukana na kupata hasara baadae au kuwajibika kama hivi.tupitie sheria zote na kama unanunua gari kwa mtu binafsi basi nenda nae polisi huyo mtu kuhakikisha hilo gari sio la wizi na polisi watoe karatasi ya kwamba hilo gari si la wizi .vinginevyo tutaendelea kulizana tu kila siku kutokana na system yetu mbovu.
 
Kila mtu anajitamkia utaratibu mpya akijisikia, au akishauriwa na hawara wake.

  • "Wanafunzi wasome shule zilizoko kwenye maeneo wanakoishi - Dar"
    .
  • "Ni marufuku kuishi Dar es Salaam kama unafanya kazi mkoa wa Pwani, kwani pasipo hivyo Pwani haitaendelea"
    .
  • ....
 
"Operesheni hii ni ya kudumu, hivyo, ninawaomba wananchi kabla ya kununua magari wafike ofisini kwetu kwanza ili gari liweze kufanyiwa uchunguzi kama ni la wizi au la, kwani watu huyaagiza kwa njia za mtandao au kutumia mawakala na njia nyingine," alisema...

Mawazo mengine ni kumuongezea mlaji kazi isiyo mhusu. Hapa kuna mahali wahusika walishindwa kufanya kazi yao (uzembe wa hali ya juu). Leo hatuwezi kwenda polisi kutoa maelezo, eti nahitaji kununua gari nao walithibitishe kuwa ni la wizi au la! ni upuuzi mtu. Magari mengine hununuliwa mnadani kwa kutumia mtandao. Ni wajibu wa vyombo husika vinavyosimamia biashara hizi kuhakikisha kuwa wanasimamia taratibu zote stahili. Ndio maana kuna taratibu za kuandikisha makampuni yanayojihusisha na biashara hizi. Ingekuwa hakuna utaratibu, basi isingewezekana hata wateja kulipia magari na bidhaa nyingine maili zaidi ya 5000 kwa mtu usiyemuona wala kumfahamu.
 
Back
Top Bottom