ISMAIL na DENIS, hampo nasi kwa macho lakini mtaendelea kuishi daima katika mioyo yetu na katika historia ya Tanzania. Mmekufa kwaajili ya wengi kwaajili ya kuutafuta uhuru wa kweli, demokrasia inayoonekana na haki inayotendeka. Leo mmeandika madai ya kutafuta haki na demokrasia kwa damu yenye thamani kuu kupita mamlaka yeyote ya Ulimwengu huu. Kwetu wananchi wa Tanzania tunathamini na kuheshimu uhai wenu na kutambua uhai wenu una thamani kuliko madaraka ya mtu yeyote hapa Duniani. Mamlaka pekee yenye kuondoa uhai wa binadamu yeyote hutoka kwa Mwuumba wetu pekee yake. Walioingilia mamlaka ya Mungu na kuondoa uhai wenu, kwa kuwa Mungu Muumba wetu ni mwenye mamlaka na haki kuliko utawala wowote wenye nguvu, awalipe kadiri ya hekima yake lakini sisi tunaomba awasamehe kwa kuwa hawajui watendalo.
Tunamwomba Muumba wetu awape uvumilivu na ustahimilivu ndugu wote wa Marehemu, Amina.