Asili100
JF-Expert Member
- Dec 4, 2012
- 240
- 181
Leo namkumbuka baba yangu mzazi aliyenitoka mwaka 1996 tarehe kama ya leo nikiwa kinda kabisa, pamoja na ukinda wangu bado nakumbuka ucheshi, uwajibikaji, ukali wa mafunzo na ubaba wa ukweli kwangu maana alinikuza katika maadili bila hata ya mama kuwepo hakupata shida nami hakuwahi kuona mzigo wala kuchoka akiwa single parent, Asante baba... alifariki siku kama ya leo kweli miaka inasogea ila kama mtu aliacha alama kubwa kama ya baba yule moyoni mwangu basi huzuni yake unaiona kama ni jana tu ameondoka... Nakupenda mzee Gerson, R.I.P
Kwa mlioondokewa na Baba zenu jamani tujumuike pamoja kuwakumbuka mashujaa hawa! Nawasilisha
Kwa mlioondokewa na Baba zenu jamani tujumuike pamoja kuwakumbuka mashujaa hawa! Nawasilisha