to the fallen Fathers

Asili100

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
240
250
Leo namkumbuka baba yangu mzazi aliyenitoka mwaka 1996 tarehe kama ya leo nikiwa kinda kabisa, pamoja na ukinda wangu bado nakumbuka ucheshi, uwajibikaji, ukali wa mafunzo na ubaba wa ukweli kwangu maana alinikuza katika maadili bila hata ya mama kuwepo hakupata shida nami hakuwahi kuona mzigo wala kuchoka akiwa single parent, Asante baba... alifariki siku kama ya leo kweli miaka inasogea ila kama mtu aliacha alama kubwa kama ya baba yule moyoni mwangu basi huzuni yake unaiona kama ni jana tu ameondoka... Nakupenda mzee Gerson, R.I.P

Kwa mlioondokewa na Baba zenu jamani tujumuike pamoja kuwakumbuka mashujaa hawa! Nawasilisha
 

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,536
1,225
^^
Poleni nyinyi mlioondokewa!
Na mkasimama imara mkaaminiwa!
.
Sote tutaondoka katika hii dunia!
Tusichoke wazazi wetu kuwaombea!
.
Kwani kazi ya mola haina makosa!
Walotenda mema yatawatakasa!
.
Daima tusonge mbele tukiwa imara,
Tusipoteze alama njema walizochora.
.
Tuwaenzi kwa maneno na vitendo,
Nasi tuwe nguzo zenye vishindo.
.
Mauti yatakapotufika dunia ituone mioyoni,
Mwa wale tulowasaidia na sio makaburini
^^
 

byb sac

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
910
500
R.I.P mzee Gerson.mwanao amekukumbuka.yeye katangulia wengine tutafata.sisi ni udongo na udongoni tutarud Bwana alitoa na Bwana ametwaa.jina lake lihimidiwe.ameeeeen.hongera kwa kusimama imara katika kipindi chote cha uzun.majozi na masikitiko.mungu akusimamie ili nawe uje kuwa mzazi bola kama huyo baba yako.one love...
 

tinna cute

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
4,633
0
Pole sana,,
Ni jambo jema kukumbuka marehemu. Kaombe misa mkuu kwa ajili ya maombi!
 

gigifiona

Member
Dec 18, 2013
14
0
Usiishie humu jf tu nenda kanisan pia mmnampenda sn baba kuliko mama maana baba alinilea tng utoto nikiwa na miaka mitatu si kwamba nama alitangulia mbele za haki Nope bali aliamua kwenda zake kujichagulia maisha ayatakayo kisa tu baba alipata matatizo kazin til nw cna mapnz namama kbsaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom