To Lock down or not to Lock down is the Wrong Question…

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,456
19,482
Debate ya Lockdown au kuendelea as is, binafsi naona ni mjadala hasi…., Swali muhimu la kujiuliza ni endapo lockdown itakuja (nchi na wananchi tumejitayarisha ?), issue sio kama tunaweza ku-survive lockdown bali tunafanya nini ili ku-survive

Chakula kitatoka wapi ?, tumejitayarisha vipi kama nchi kuwahifadhi na wapi tutawaweka Watoto wa mitaani ?

Serikali inabidi kuangalia wananchi as a whole na individuals inabidi kujiangalia wao na familia zao.., ukifungiwa utakula nini na kwa muda gani ? una stock kiasi gani n.k.

Wewe kama machinga au mission town na una Kijiji kwenu, je ni vema kurudi kijijini kwenye kuni na shamba ambalo unaweza kulima na kujilisha wewe na jamii yako ? (ukizingatia vijijini sidhani kama kutakuwa na lockdown). Pia kama unauza nguo, chupi n.k. Je ni wakati labda wa kuuza products zinazoendana na wakati ?, mfano Chakula n.k., pia Je ni wakati wa kuwapa wakulima nguvu ili walime zaidi kuongeza stock ya chakula?, Vilevile Je ni vema kuanza kuhifadhi mboga kwa njia za mababu zetu hata kwa wale ambao hawa fridge ?

Survival instinct lockdown ikija vibaka na wizi unaweza kuongezeka Serikali imejitayarisha vipi kuhakikisha kuna Amani na hakuna panic, looting au hooliganism?

Hayo ni maswali machache tu ambayo individual kama una familia inabidi uwaze kwa niaba ya Jamhuri ya Serikali yako ya Nyumba yako…, sababu kumbuka binadamu tuta-survive hili, ila hakuna guarantee kama na wewe utakuwa katika hao watakao-survive pindi patakapokucha…..

Pia tunamuachia Mungu inabidi iwe kauli ya mwisho baada ya kupigana na kuhakikisha mbinu zote tumezijaribu (ama sivyo tungefunga mahospitali yote na kujenga misikitini na makanisa mahali pake)…. Unaomba Mungu ukiwa na Sanitizer Mfukoni

Peace……
 
Hapo ulipoandika wale mission town warudi vijijini kulima, hivi kuna kilimo unachoweza kwenda mwezi wa nne huu halafu ulime uanze kupata chakula?

Kwanza ukiwa unalima utakuwa unakula wapi wakati mishe zako ni za kila siku kupata pesa ndio unakula?
 
Hapo ulipoandika wale mission town warudi vijijini kulima, hivi kuna kilimo unachoweza kwenda mwezi wa nne huu halafu ulime uanze kupata chakula??

Kwanza ukiwa unalima utakuwa unakula wapi wakati mishe zako ni za kila siku kupata pesa ndio unakula??
Mahitaji Muhimu ya Binadamu...
1) Chakula (most important)
2) Mavazi (ingawa hata bila mavazi hautakufa)
3) Malazi (Kupumzika)

Pesa ni just medium ya kupata hayo hapo juu.., ndio maana nikasema wale mission town ambao wana vijijini wanaweza kurudi kwao ukipanda shamba la mchicha wiki mbili unavuna, kuni unaweza kuzipata (mjini ukiwa magorofani hizo mission town utazifanyia wapi)?, ukifungiwa mjini hakuna kuni gesi mtungi utakaa siku ngapi.., na hizo mission town utazifanya na kina nani ikiwa watu wapo lockdown ?

Wenye vijiji wana choice ambayo wakiifuata watakuwa kwenye better position ya ku-survive (ingawa kuna risk ya kuwapelekea ndugu zao maambukizi), pia time is running out mambo yakiwa mabaya usishangae watu wakakatazwa kwenda vijijini...
 
AKIli zako kama mwigulu tu
Hoja sio umahili wa akili zangu.., swali la muhimu ni wapi hapako sawa, Kutokuangalia tumejitayarisha vipi ni sawa na kuficha uso mchangani na kudhani sababu hatuwaoni wengine na wao hawatuoni....

Mwisho wa siku ni wewe na jamii yako mmejipanga vipi, sio Mwigulu au Serikali inafanya au haijafanya nini (kuwajibika au kutokuwajibika kwao isiwe fursa ya kutokuwajibika kwako)
 
KeyserSoze,
Mkuu unaongea theory sana..

Mtu ametoka town hana pesa.. akafika Mungu saidia akakuta shamba kijijini.. siku hio hio akaanza kulima huo mchicha unaosema wewe.. baada ya week mbili akavuna..

Swali linakuja.. hizo week 2 anaishije?? Huo mchicha akivuna anaula au anauza ?? Akila - unahisi mtu anaweza kuishi kwa kula mchicha?? Akiuza unadhani anaweza kupata hela ya kumfanya aishi ??
 
Mkuu unaongea theory sana..
Kwanza kabisa nashukuru sababu sasa hivi mjadala sio tufunge au tusifunge bali tukifunga tunafanyaje na practicability ipoje

Mtu ametoka town hana pesa.. akafika Mungu saidia akakuta shamba kijijini.. siku hio hio akaanza kulima huo mchicha unaosema wewe.. baada ya week mbili akavuna..

Ukisoma maelezo niliyotoa ni wale wenye vijiji (sio kila mtu aende vijijini) which means tayari kuna infrastructure kule yeye na familia yake wanaenda kuongeza nguvu kazi

Swali linakuja.. hizo week 2 anaishije?? Huo mchicha akivuna anaula au anauza ?? Akila - unahisi mtu anaweza kuishi kwa kula mchicha?? Akiuza unadhani anaweza kupata hela ya kumfanya aishi ??
Hivi ikija lockdown huyu mission town ataishi vipi ?, Mission town aliyerudi kijijini na mission town aliyepo town bila mission nani yupo katika nafasi nzuri ya survival ?

Pia kumbuka kwenye janga kama hili commodity yenye maana kuliko zote ni chakula..., sidhani kama atakuwa na uwezo wa kusupply demand ila kama uwezo anao demand itakuwa sio ya kawaida na hata rafiki zake mission town wa town anaweza kuwasaidia kwa kuwatumia fungu chache za nyanya na mchicha......
 
Back
Top Bottom