TMK Wanaume Halisi wee acha tuu!

Kuntakinte

JF-Expert Member
May 26, 2007
701
30
Baada ya Dar, yaua Dom, Moro matangana Vumilia Kondo, MorogoroKUNDI la muziki wa kizazi kipya la Wanaume Halisi, limefanikiwa kuwafunika tena wapinzani wao, Wanaume Family katika maonyesho mawili yaliyofanyika katika mikoa ya Dodoma na Morogoro.

Katika onyesho la Dodoma lililofanyika Ijumaa iliyopita, Wanaume Familiy ndio walikuwa wa kwanza kupanda jukwaani kurusha kete yao.

Walianza na wimbo wa ‘Pisha Njia’, lakini hawakupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa mashabiki na ndipo ilipofika zamu ya Wanaume Halisi ambao wao walianza na wimbo wa ‘Shemeji Shemeji’ ambao ulionekana kuwazingua vilivyo mashabiki waliofika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani humo.

Katika hali isiyotegemewa, kundi la Wanaume Family liliwavamia wenzao wa Wanaume Halisi katika klabu ambayo walipata mwaliko wa kufanya shoo usiku huo na kuanza kuwafanyia fujo, ikiwemo kuwatukana matusi ya nguoni na kuwatishia maisha.

Aidha, katika onyesho la mjini Morogoro lililofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Vijana, mashabiki pia walionekana kuzinguliwa na kundi la Wanaume Halisi kuliko lile la Wanaume Family ingawa walikuwa na wimbo waliotaja mkoa huo ujulikanao kama ‘Dar mpaka Moro’.

Hali ilikuwa mbaya zaidi hata pale walipopanda jukwaani kwa mara ya pili kuimba nyimbo nyingine ambapo mashabiki walikuwa wakiwaonyeshea 3-0 hali iliyodhirisha kwao jinsi Wanaume Halisi walivyo juu.

Aidha, kiongozi wa Wanaume Halisi, Juma Kassim ‘Sir Nature’ amewataka wenzao hao kuacha ugomvi kwani hakuna maana yoyote ila wajipange upya ikiwezekana kutoa nyimbo zilizosimama ili waweze kuwateka mashabiki kama wao walivyofanikiwa.

“Unajua si kama sisi ugomvi hatuuwezi. Tunauweza sana ila sisi tumekuja kufanya kazi, hatujafuata ugomvi ila kama wao wamekuja na mawili sawa, sisi tunafanya muziki na wao wajitahidi kufanya muziki si ugomvi,” alisema Nature.

Makundi hayo yanatarajiwa kukutana tena Ijumaa hii katika Mkoa wa Arusha.

Hadi sasa tathimini ya ‘Mkali Nani’, inaonyesha Wanaume Halisi kuwa juu zaidi.
juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 18 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Wanaume Family wanapigwa bao 3 BILA hivi hivi wakijiona!

na Safari, Dar/ Tanzania, - 21.04.08 @ 10:29 | #7651

Haya makundi yote mawili ni makali ile mbaya. Kinachokosekana kwa Wanaume Family ni mtu anaebeba kundi. Hapa ndipo Nature anapowazidi. Huyu jamaa anakubalika sana kwa washabiki kwa jinsi anavyowajibika jukwaani. Kwaujumla anacho kipaji cha hali ya juu. Pia hapa yupo Inspector "Babu" Harun. Mimi naamini vichwa hivi vikichanganyika na wengine wengi kama akina Lt Karama Wanaume Family wanahitaji muda wa kutosha kushindana kwenye game. Hili la ugomvi nalo litazidi kufanya kundi lao lichukiwe. Mimi nawashauri wawe wapole tu!Vinginevyo watakula 6-0 na si 3-0 tean!!!!

Wakatabahu,

na Mtanashati, TZ, - 21.04.08 @ 09:05 | #7735

ivi watanzania mnamacho kweli. kati ya wanaume halisi na wanaume family ,bado mnampa kichwa juma nuture,hana kitu kwa ukweli zaidi,jamani mwenye macho haambiwi tazama,juma nature ana nini zaidi ya kuimba mafumbo,kwani hii taarabu. naweza sema kwamba halisi wamebebwa na juma nature kwakuwa ana dam ya kupendwa na watu,ila game kashashindwa han a lolote,zaidi ya mafumbo ya kipumbavu kwemye game,angalia nyimbo za tmk wanaume,zichanyganye na halisi,juma nature kabaki kuwa mwimba taarabu,mafumbo fumbo aende kumsaidia ,khadija kopa.labda naweza sema ni mshirikina ,awezi kufagiliwa sehem isiyokuwa na ukweli,naomba huu ujumbe utoke kwenye gazeti,halisi hawana kitu,labda mizizi,tumeona mara ngapi anaimba pumba na watu wanashangilia,kama babu yake mchawi aseme.kwangu mimi huwa naangalia ukweli na reality,uchawi akaroge wajinga. ania

na ania laura, tanzania, - 21.04.08 @ 09:14 | #7741

WATANZANIA WENGI NI WAJINGA NA NDIO MAANA WANAWAPENDA WANAUME HALISI AMBAO NYIMBO ZAO ZIMEJAA MAJUNGU 2 NA KWA SABABU WAJINGA NI WAPENDA MAJUNGU NDIO MAANA WANANSHANGILIA NATURE HILA HAWANA LOLOTE.

na JOHN - 21.04.08 @ 09:51 | #7758

WANAUME HALISI JUUUUUUUUUUUUUUUUUUU. 3-O kitu na box.

na Sweet, Tanzania, - 21.04.08 @ 10:18 | #7770

nature anaimba real life ya uswahili,amekulia kwenye shida,japo namafanikio yote hujawahi kumsikia akiimba ujinga wa kujisifia au maisha ya kifahari,analilia shida,na wa tz wengi wanashida thats why anapendwa,sio kina temba mara sijuibaba yake baaresa,mara anaenda kuimba nyimbo za dini then anarudi anaimba kuhusu bangi,hajijui anasimama wapi,na wanaume family wanamuweka mbele,wanaume halisi ndo wanajua maisha ya tz,hata sisi tulio nje tukiwasikiliza jamaa inatufanya tusijisahau na kujiona tumefika.baadhi ya mistari ya nature "kijana anaonekana mvivu wa kufahamu,hafai kumuita dogo anaonekana mtu wa makamu" shule tumekuja kusoma au kupewa adhabu za vyoo,hata nibanwe vp sijisaidii ngo"

na john - 21.04.08 @ 10:36 | #7778

john shika adabu watanzania tuna akili na wanaume halisi wanatisha isipokuwa tu hawawezi ugomvi unaoupenda wewe

na mosses, tz, - 21.04.08 @ 11:44 | #7801

hakuna bwana labda kwa majungu sio kuimba 3 - 0 inaelimisha nini

na john - 21.04.08 @ 12:58 | #7824

nature nyota inawaka hakuna uchawi wakinga wanashine kariako mnaidanganya akili yenu hela za uchawi acheni imani potofu tafuteni acheni visingizio kama soka la bongo

na jacklin, dsm, - 21.04.08 @ 13:12 | #7828

Mimi nakubaliana na john kwamba wanaume family nyimbo zao ni nzuri tatizo nature ana nyota ya kupendwa na watu.Nafikiri ili kumpata mshindi wa kweli wateuliwe wataalamu wa muziki na waanze kuchambua nyibo zao kitaalamu, ninaimani watakuja na matokeo mazuri. Hii ya kuzunguka mikoani ni biashara na wala si ushindani
inno

na innocent, dar, - 21.04.08 @ 14:04 | #7847

KUNDI LA WANAUME HALISI NI BORA KULIKO WANAUME TMK,TMK FAMILY WANA WIMBO GANI AMBAO UMEELIMISHA JAMII?HATA KWA MSANII MMOJAMMOJA WA HILO KUNDI HANA WIMBO WENYE KUELIMISHA TUTAKE TUSITAKE HUU NDO UKWELI WENYEWE,ANGALIA KUNDI LA WANAUME HALISI WASANII KAMA NATURE,INPECTOR,RICH ONE NA WENGINE NYIMBO ZAO ZINA ELIMISHA HATA NYIMBO ZA KUNDI AU HAMJUI MAANA YA 3 BILA?HILI SIO JUNGU WAMETUMIA TAFSIDA KAMA UNAVYOJUA BABU YUPO KWENYE HILO KUNDI KWA MISAMIATI ZAIDI,TATIZO TUNASHABIKIA MUZIKI WAKATI HATUJUI NINI MAANA YAKE,WANAUME HALISI WANAKILA SABABU YA KUWASHINDA WANAUME FAMILY,TUSEMA ULE UKWELI TMK FAMILY WANA WIMBO GANI WA KUELIMISHA JAMII?ZAIDI WANAIMBA MAPENZI KUCHOCHEA NGONO NCHI.MIMI HAPA SINA KUNDI ILA NAANGALIA NYIMBO ZINAZO ELIMISHA JAMII,HUWEZI KUWA FANANI BILA HADHILA,SASA MIMI NI HADHILA NIMEKATAA KAZI ZA WANAUME FAMILY SIO NZURI.NI HAYO TU.

na ALLYBABA, MARA, - 21.04.08 @ 15:34 | #7869

Acheni majungu wanaume halisi wapo juu kwa fani.

na Mussa, Tanzania, - 21.04.08 @ 19:11 | #7933

Acheni majungu wanaume halisi wapo juu kwa fani.

na Mussa, Tanzania, - 21.04.08 @ 19:11 | #7934

wanaume halisi ndo namba moja.mtoto wakiume utmfuataje demu.ndomana tatu bila zinawtosha

na almex, ar, - 21.04.08 @ 19:17 | #7935

Wewe John akili yako nahisi ni machicha kabisaaaa, huwezi ukawaita watanzania wajinga. wewe unajua kipimo cha Ujinga. kama huna nyimbo, kaa kimya mtoto. Toa maoni sio kutukana. halisi mpaka sasa wanafanya vizuri, why don't you appreciate. Jipangeni upya mkiweka jitihada na kuacha ugomvi mtafanikiwa na mtapata kura nyingi.
Punguza jazba kijana, au hujatahiri?

na emmanuel, usa, - 22.04.08 @ 08:05 | #7954


Wahenga walisema wengi wape,hakuna sababu ya kucharurana bila sababu,huwezi kushindana na sauti ya wengi,kwanini tuandikie mate? eti waje wataalamu wa muziki wachambue mnataka kutuletea majaji waleeee walio mchagua misoji na idi? ni ajabu nalazima tukubali mtu anaamua kutoka kundi ambalo liko juu anaanzisha jipya na bado anapendwa eti uchawi kwanini na wao wasirogee.kuna wasanii wangapi waliimba vinyimbo(visenti) vichache na hawasikiki tena? Nature ni moja wa waanzilishi wa nyimbo hizi za kizazi kipya nayupo juu mpaka leo.lazima tukubali 3-0 wamebana wameachiaaaaaa.

Na Shemeji

na mossi, dar-es-salaam,Tanzania, - 22.04.08 @ 09:55 | #7966

kila mtu ana hisia zake juu ya kitu fulani km mtu anawafeelwanaume halisi ya nini wewe kumuita ******** wewendie ******** haswaa.
WANAUME HALISI JUUUUUUUUUUU!!!!!!!

na kimson, tz dsm, - 22.04.08 @ 11:09 | #8004

TMK WANAUME WANATISHA ILA TU KITU KIMOJA HAWANA KICHWA AMBACHO KINA BEBA KUNDI ILA JAMAA NAWAKUBALI CNA NI NOMA TMK WANAUMEEEEEE JUUUUU!!!!!!!!!!!!

na manento miraji , KASULU - TANZANIA, - 22.04.08 @ 11:32 | #8008
 
Imebidi nitafute uzi kuhusu TMK wanaume family na TMK halisi baada ya kuangalia #tbt ya mkali nani clouds tv..hakika tmk halisi walitisha sana
and mashabiki wanaonekana hawakuihitaji wasanii wengine waperform zaidi ya tmk halisi.
Walipanda Watupori, Nako2Nako ila Waliishia kutupiwa chupa kama tmk family
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom