TMA: Mvua za Vuli zitakuwa chini ya wastani wakulima walime mazao yanayostahimili ukame!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,012
142,044
Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dr Kijazi amesema mvua za Vuli zitakuwa chini ya wastani na zitaanza kunyesha wiki ya nne ya mwezi huh

Wakulima wanashauriwa kulima mazao yanayostahimili ukame

Source ITV habari
 
Hawa TMA wanao utaratibu mzuri sana wa kutuma kwenye Simu na e-mails.
 
Lakini si ilinyesha? Siku zote Utabiri (Probability of an event to occur) ni ngumu. Ni kama wale Wazee wa kuweka mzigo-ie. kubet. Wengi wanachemka lakini wanaendelea kucheza.
Basi wakae kimya tu. Wazee wa kubet wasituzuie mashabiki kwenda uwanjani kwa kigezo cha ubashiri wao
 
Basi wakae kimya tu. Wazee wa kubet wasituzuie mashabiki kwenda uwanjani kwa kigezo cha ubashiri wao
Hapana mkuu. Wao hutumia vyombo/vifaa ambavyo navyo vina mapungufu yake. Lakini mara nyingi huwa karibu na Ukweli i.e. Uwezekano wa kutokea kama walivyoTabiri ni mkubwa.
Rejea majuzi kati hapo walitabiri habari za vimbunga n.k. Cha msingi hapo ni kuchukua Tahadhari kama Jamaa alivyosema hapo juu.
 
Basi wakae kimya tu. Wazee wa kubet wasituzuie mashabiki kwenda uwanjani kwa kigezo cha ubashiri wao
Sio vizuri wakakaa kimya kwani wapo kikazi zaidi na hawashughuliki na habari za Mvua tu bali na Masuala mengine mtambuka e.g. magonjwa ya mlipuko(Rejea homa ya bonde la ufa- mifugo na Binadamu), Nzige waharibifu(rejea Kenya 2020/2021), Mafuriko, Baridi kali(rejea 2022 May-Aug) n.k.
Kwa hiyo tusiwalaumu kwa kutofanya vizuri katika kigezo kimoja tu cha mvua.
Inafaa na Inashauriwa kwamba pale wanapotoa Utabiri wao sasa wewe angalia inakuhusu vipi(Faida au Hasara) na uchukue Tahadhari/Hatua fulani i.e. Uanze kujipanga. Wakati mwingine Tangazo lao ni ishara ya Fursa kwa wengine. Kwa mfano wafanya biashara za vyakula (ikiwemo na mbege), wavuvi, Wafugaji na wasafirishaji n.k.
 
Back
Top Bottom