"Dondoo muhimu za msimu wa mvua za Vuli; Oktoba - Disemba 2023"

Mashima Elias

Member
Dec 22, 2010
18
52
"Dondoo muhimu za msimu wa mvua za Vuli; Oktoba - Disemba 2023"
Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
"Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli katika kipindi cha Oktoba – Disemba, 2023, ushauri kwa wadau wa sekta na mamlaka mbalimbali kama vile Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Utalii na Wanyamapori, Uchukuzi, Mamlaka za miji, Nishati, Maji na Madini, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa.

Baadhi ya mambo muhimu katika taarifa hii ni: -
i. Uwepo wa El-Niño unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mvua za msimu wa Vuli, 2023.
ii. Mvua za Vuli, 2023 zinatarajiwa kuwa za Juu ya Wastani hadi Wastani katika maeneo mengi ya pwani ya kaskazini na ukanda wa Ziwa Victoria.

Aidha, kwa maeneo ya nyanda za Juu kaskazini mashariki na maeneo machache ya mashariki mwa Ziwa Victoria mvua zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Juu ya Wastani.

iii. Mvua za Vuli, zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2023 katika maeneo ya magharibi mwa Ziwa Victoria na kusambaa katika maeneo mengine mwezi Oktoba, 2023. Kwa kawaida mvua za Vuli huisha mwezi Disemba, hata hivyo msimu huu mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kuendelea Januari, 2024.
iv. Ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Disemba, 2023.

Athari zinazotarajiwa:
i. Shughuli za kilimo zinatarajiwa kuendelea kama ilivyo kawaida kwa msimu wa Vuli, 2023. Hata hivyo, ongezeko la unyevu wa udongo linaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na shughuli za kilimo.

ii. Kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka.

iii. Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji."

sw1692872_20230825_144223_1.jpg
 
View attachment 2728246
🙏🙏👏
 
Back
Top Bottom