TLS yaingilia kati sakata la Mbowe

TLS yaingilia kati sakata la Mbowe

"Kufanya kongamano haijawahi kuwa kosa la jinai kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi.

Katiba yetu ibara ya 21(1) inatoa haki ya kujumuika na ibara ya 13(1) inatoa masharti ya watu wote kuwa sawa mbele ya Sheria.

Kitendo cha kumkamata usiku wa manane Mheshimiwa Freeman Mbowe na wenzake, kwa sababu ya kuandaa kongamano ni ukiukwaji wa Katiba na Sheria za nchi yetu.

Ikiwa kuna tuhuma nyingine dhidi yake bado kwa sheria zetu alipaswa kuwa amefikishwa kwenye mamlaka za kisheria na si kuendelea kuzuiliwa.

Natoa mwito kwa mamlaka kumwachia huru kwa sababu kuendelea kumshikilia ni kukiuka utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

Chama cha Mawakili wa Tanganyika tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu suala hili na tutatoa msimamo wetu na mwelekeo baada ya mashauriano kufanyika kupitia Baraza la Uongozi".

Rais wa TLS.
Edward HoseahView attachment 1867618
Wasikuyumbishe mzee, TLS ilishaanza kuwa chama kigaidi hadi ulipokuja ukaokia jahazi watu walikuwa wamechoka. Umesema:

......Katiba yetu ibara ya 21(1) inatoa haki ya kujumuika na ibara ya 13(1) inatoa masharti ya watu wote kuwa sawa mbele ya Sheria.......?

Yaani kama Mbowe akitenda ugaidi ashitakiwe ugaidi sawa tu namagaidi wengine.
 
Ety katiba ya sasa imepitwa na wakati halafu bado mnaendelea kufuata kilichoandikwa humo, kama kawaida ukiitwa mpinzani bc kazi yako ni kupinga-pinga
Kama raia wenyewe TZ ndio Kama wewe Basi maendeleo tutasubiri Sanaa?.
Yaani hioni haja ya katiba mpya?, Seriulously?
 
Wasikuyumbishe mzee, TLS ilishaanza kuwa chama kigaidi hadi ulipokuja ukaokia jahazi watu walikuwa wamechoka. Umesema:

......Katiba yetu ibara ya 21(1) inatoa haki ya kujumuika na ibara ya 13(1) inatoa masharti ya watu wote kuwa sawa mbele ya Sheria.......?

Yaani kama Mbowe akitenda ugaidi ashitakiwe ugaidi sawa tu namagaidi wengine.
Yes "kama ametenda"
 
Ety katiba ya sasa imepitwa na wakati halafu bado mnaendelea kufuata kilichoandikwa humo, kama kawaida ukiitwa mpinzani bc kazi yako ni kupinga-pinga
Watu kama wewe ni wa kusamehe kwa sababu siyo kosa lako. Hujui kinachoongelewa kuhusu katiba! Na hata katiba hujui ni nini!
 
Nawaomba sana Ccm (ambao vyombo vya dola viko chini yao), wajue kwamba idadi kubwa ya Watanzania wa sasa ni vijana. Kwa kawaida, vijana ni watu ambao katika kutenda jambo lolote wana jazba nyingi kuliko utulivu. Ukichanganya hali hii na athari za corona zilizofanya biashara nyingi zidorore, na pia ukweli kwamba zaidi ya 90% ya vijana waliomaliza masomo hawana ajira, vijana wengi sana wana msongo wa mawazo (stress).

Kwa sababu hiyo, wale ambao ni mashabiki wa upinzani, hawawezi kukubali kabisa kwamba Mbowe anaweza kuwa na tuhuma za kweli za ugaidi kama ambavyo vyombo vya usalama vinavyosema. Bado wanakumbuka jinsi Mdude Nyagali alivyofungwa kwa kesi ya kubambikwa hadi alipoachiwa juzi juzi tu. Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa sana kwamba wataona kwamba hata hizo tuhuma dhidi ya Mbowe bila shaka ni za kubambikiza tu. Kwa stress walizonazo, hao vijana mashabiki wa upinzani watakuwa wameundiwa chuki kubwa sana mioyoni mwao.

Jambo moja ambalo pia linawafanya watu wengi waamini kwamba kukamatwa kwa Mbowe ni moja ya matukio ya Ccm kuonea wapinzani (hasa Chadema) ni ukweli kwamba viongozi wa Chadema walikamatwa wakati huo huo Mbowe alipokamatwa kwa kosa la kutaka kwenda kufanya kongamano la kudai katiba mpya. Wangekuwa wamekamatiwa kwenye ukumbi tungesema wamekiuka amri ya kuzuia mikutano kwa sababu ya corona. Lakini walikamatiwa hotelini. Nashindwa kuelewa hao waliowakamatia hoteli watathibitisha vipi mahakamani kwamba waliokamatwa kweli walikuwa na mpango wa kukutana ilhali hawakuwa wamefika ukumbini.

Kwa mawazo yangu, naamini matendo ya kuwakamata wapinzani kwa mtindo huo yanachochea chuki kubwa ndani ya mioyo ya wapinzani. Naomba wana Ccm mtambue kwamba chuki ikishapandwa ndani ya mioyo ya watu, inakuwa vigumu sana kuiondoa. Mauaji ya kimbari ya Rwanda yalitokana na chuki zilizokuwa "zimejikusanya" ndani ya mioyo ya watu kwa muda mrefu. Kwa sababu tu Tanzania imekuwa nchi yenye amani kwa muda mrefu,.haina maana amani hiyo haiwezi ikapotea ghafla kwa sababu ya chuki zilizo ndani ya mioyo ya watu. Halafu, tukumbuke kwamba kule Soweto Afrika Kusini, watoto wadogo wa shule za msingi waliamua "liwalo na liwe" wakaanza kupambana na askari wa makaburu wenye mabunduki, mabomu na mbwa bila kujali kwamba wenzao walikuwa wanauawa wao wakiona. Kwa hivyo tusidhani ya kuwa hata hapa Tanzania hali kama hiyo haiwezi ikatokea kama vijana wengi wanaona wanaonewa kwa sababu tu ni wapinzani.

Nawaombeni sana, sana, vyombo vya ulinzi. Mnapofanya kazi zenu, msizifanye kwa namna ambayo itawafanya mwonekane mnaonea watu. Kama mlikuwa mmeshapata habari za tuhuma dhidi ya Mbowe kabla hajaenda Mwanza, basi mngemkamata kabla hajaenda huko. Kama mlipata hizo habari baada ya kujua anajipanga kuingia kwenye kongamano la katiba, mngemwacha amalize kongamano ndipo mumkamate. Hapo ingeonekana wazi kwamba kosa alilokamatwa nalo sio la kudai katiba mpya. Nawaomba mtambue kwamba mnasababisha nchi yetu ionekane katika "picha mbaya" kwa Watanzania wengi na mataifa ya nje (wakiwemo wafadhili na wahisani wetu).
 
Wewe inaonekana ni used
Huyo jamaa ni mhanga wa elimu ya Bongo. Pia inaonekana huu utamaduni wa kushinda vijiweni kubishana kwa vitu vilivyowazidi uwezo umemwa-affect sana. Huyu hajui hata kifungu kwenye katiba ya Tanzania na kuna uwezekano mkubwa hata maana ya katiba hajui. Usimpe attention kubwa ya kulumbana naye.
 
Nawaomba sana Ccm (ambao vyombo vya dola viko chini yao), wajue kwamba idadi kubwa ya Watanzania wa sasa ni vijana. Kwa kawaida, vijana ni watu ambao katika kutenda jambo lolote wana jazba nyingi kuliko utulivu. Ukichanganya hali hii na athari za corona zilizofanya biashara nyingi zidorore, na pia ukweli kwamba zaidi ya 90% ya vijana waliomaliza masomo hawana ajira, vijana wengi sana wana msongo wa mawazo (stress).

Kwa sababu hiyo, wale ambao ni mashabiki wa upinzani, hawawezi kukubali kabisa kwamba Mbowe anaweza kuwa na tuhuma za kweli za ugaidi kama ambavyo vyombo vya usalama vinavyosema. Bado wanakumbuka jinsi Mdude Nyagali alivyofungwa kwa kesi ya kubambikwa hadi alipoachiwa juzi juzi tu. Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa sana kwamba wataona kwamba hata hizo tuhuma dhidi ya Mbowe bila shaka ni za kubambikiza tu. Kwa stress walizonazo, hao vijana mashabiki wa upinzani watakuwa wameundiwa chuki kubwa sana mioyoni mwao.

Jambo moja ambalo pia linawafanya watu wengi waamini kwamba kukamatwa kwa Mbowe ni moja ya matukio ya Ccm kuonea wapinzani (hasa Chadema) ni ukweli kwamba viongozi wa Chadema walikamatwa wakati huo huo Mbowe alipokamatwa kwa kosa la kutaka kwenda kufanya kongamano la kudai katiba mpya. Wangekuwa wamekamatiwa kwenye ukumbi tungesema wamekiuka amri ya kuzuia mikutano kwa sababu ya corona. Lakini walikamatiwa hotelini. Nashindwa kuelewa hao waliowakamatia hoteli watathibitisha vipi mahakamani kwamba waliokamatwa kweli walikuwa na mpango wa kukutana ilhali hawakuwa wamefika ukumbini.

Kwa mawazo yangu, naamini matendo ya kuwakamata wapinzani kwa mtindo huo yanachochea chuki kubwa ndani ya mioyo ya wapinzani. Naomba wana Ccm mtambue kwamba chuki ikishapandwa ndani ya mioyo ya watu, inakuwa vigumu sana kuiondoa. Mauaji ya kimbari ya Rwanda yalitokana na chuki zilizokuwa "zimejikusanya" ndani ya mioyo ya watu kwa muda mrefu. Kwa sababu tu Tanzania imekuwa nchi yenye amani kwa muda mrefu,.haina maana amani hiyo haiwezi ikapotea ghafla kwa sababu ya chuki zilizo ndani ya mioyo ya watu. Halafu, tukumbuke kwamba kule Soweto Afrika Kusini, watoto wadogo wa shule za msingi waliamua "liwalo na liwe" wakaanza kupambana na askari wa makaburu wenye mabunduki, mabomu na mbwa bila kujali kwamba wenzao walikuwa wanauawa wao wakiona. Kwa hivyo tusidhani ya kuwa hata hapa Tanzania hali kama hiyo haiwezi ikatokea kama vijana wengi wanaona wanaonewa kwa sababu tu ni wapinzani.

Nawaombeni sana, sana, vyombo vya ulinzi. Mnapofanya kazi zenu, msizifanye kwa namna ambayo itawafanya mwonekane mnaonea watu. Kama mlikuwa mmeshapata habari za tuhuma dhidi ya Mbowe kabla hajaenda Mwanza, basi mngemkamata kabla hajaenda huko. Kama mlipata hizo habari baada ya kujua anajipanga kuingia kwenye kongamano la katiba, mngemwacha amalize kongamano ndipo mumkamate. Hapo ingeonekana wazi kwamba kosa alilokamatwa nalo sio la kudai katiba mpya. Nawaomba mtambue kwamba mnasababisha nchi yetu ionekane katika "picha mbaya" kwa Watanzania wengi na mataifa ya nje (wakiwemo wafadhili na wahisani wetu).
Mzee wa hekima umenena hekima yako

Tuliambiwa rais ni mmoja tu,huyu katoka wapi?

Kuna yule mnyaturu wa ubeligiji alipewa urais wa hao mawakili sijui akajiona kashakua rais wa JMT.
Alichopata anakijua
 
Ety katiba ya sasa imepitwa na wakati halafu bado mnaendelea kufuata kilichoandikwa humo, kama kawaida ukiitwa mpinzani bc kazi yako ni kupinga-pinga
Katiba Mpya (bora) ni hitaji la Watanzania na wewe ukiwa mmojawapo. Katiba iliyopo siyo kwamba ni mbaya yote, ila ina maeneo mengi ambayo inabidi kuyarekebisha. Kama ulishawahi kusoma Rasimu ya Katiba II Iliyopendekezwa (2013) ina mambo mazuri mengi - mfano mbunge angalau awe na elimu kuanzia Kidato cha Nne. Ya sasa inasema mbuge awe anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza, halafu linapokuja suala la kujadili mikataba ya kimataifa au mambo muhimu yanayohitaji elimu nzuri na busara, unaona huyo wa kujua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza utamweka wapi. Matokeo yake badala ya kujadili hoja, kunakuwa na mipasho na lugha ya kudhalilishana kama ambavyo mara nyingi huwa tunaona. Rasimu hiyo pia imeweka mgawanyo mzuri wa madaraka na teuzi mbalimbali serikalini namna gani zifanyike. Hivyo, badala ya kuwaangalia wanaodai Katiba Mpya kwa jicho la ubaya (wao wabaya kwa vile wanadai na sisi ni wema kwa vile hatudai), tujaribu kuona hoja zao na kuzipima kuliko kuwa na 'hoja zoazoa' (wholesale/sweeping/blanket statements) tu.
 
Baada ya watu kumponda huyo Hosea kwenye mitandao ya kijamii ndio kujitokeza. Aende mahakamani kupata tafsiri ya kisheria kuhusu huu uhuni unaondelea wa kuwazuia cdm kufanya mikutano, lakini mechi za mpira zinaendelea, na wanaccm wanafanya mikutano wakavyo.
Well said!

Agizo lake limechelewa limelegea halina mkazo msisitizo lipolipo tu
Amesema tu kuondoa lawama

The guy is full sisiem sijui kwa nini wengi wanaamini he will make changes.
Wapinzani kuna wakati wanavuruga watu
Huyu ni chawa point blank period!
 
Back
Top Bottom