TLS: Tumejiridhisha pasipo shaka kwamba Ndugu Baraka Mkama, aliyefanya vurugu Mahakamani sio Wakili na sio Mwanachama wa Tanganyika Law Society

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,457
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimejitenga na ‘Wakili’ Baraka Mkama anayedaiwa kusababisha vurugu katika lango kuu la kuingilia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam, kikisema sio Wakili na wala sio mwanachama wa chama hicho cha kitaaluma.

Mkama anadaiwa kusababisha taharuki hiyo Jumanne Mei 23, 2023 katika mahakama hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwazuia Polisi wasiwakamate upya washtakiwa aliokuwa anawatetea mahakamani hapo ambao walifutiwa kesi yao, hali iliyosababisha kukamatwa kwake.

Hata hivyo baada ya taarifa hiyo kuruka katika vyombo vya habari na mitandao yake ya kijamii, taarifa ziliibuka kuwa Mkama sio Wakili na hata namba ya uwakili aliyoitaja wakati anahojiwa na TLS haikuwa yake bali ya Wakili mwingine na ndipo Baraza la TLS lilipounda timu kuchunguza sakata hilo.

Taarifa iliyotolewa Mei 27, 2023 na kusainiwa na Rais wa TLS, Harold Sungusia imeeleza baada ya TLS kupokea taarifa ya uchunguzi uliofanywa na timu uliyounda imejiridhisha pasina shaka kuwa Mkama sio wakili wala mwanachama wa TLS na hata katika mfumo wa usajili wa mawakili (e-wakili) hayupo.

Mei 24, 2023, TLS iliunda timu ya mawakili watano kuchunguza sakata la ‘Wakili’ Mkama anayedaiwa kusababisha vurugu katika eneo hilo la Mahakama.

Walioteuliwa kufanya uchunguzi katika sakata hilo ni Mawakili Magreth Mwihava (Mwenyekiti), Hekima Mwasipu (mjumbe) Emanuel Augustine (mjumbe) na Anastazia Muro ambaye ni Katibu wa timu.

Timu hiyo pamoja na mambo mengine ilifanya uchungu wa kina kwa kumfanyia mahojiano Mkama mwenyewe, Uongozi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jeshi la Polisi, Ofisa wa Polisi aliyehusika katika sakata hilo, na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, ili kujua sababu za vurugu hizo na kuangalia katika mfumo wa e-wakili.

Hata hivyo, Ijumaa Mei 26, 2023 timu hiyo iliyongozwa na Mwenyekiti wa TLS Tawi la Ilala, Margreth ilikabidhi ripoti ya uchunguzi kwa Baraza la TLS kwa ajili ya uamuzi.

“Katika kufuatilia tukio hili, TLS imepata taarifa muhimu za ziada kuhusu mtandao wa watu wasiokuwa Mawakili wanaofanya kazi za uwakili (vishoka) hivyo imeiongezea muda Kamati teule ya uchunguzi kuendelea kufuatilia mtandao huo na kuwasilisha taarifa zake za ziada ifikapo Mei 31, 2023.”

Kwa upande mwingine, TLS imeunda kikosi kazi (Anti-Vishoka Taskforce) kitakachofanya kazi ya kudhibiti watu ambao hawastahili kufanya kazi za mawakili.

Baraza la Uongozi la TLS linaomba ushirikiano toka kwa wanachama wake na wadau wengine pamoja na wananchi ili kwa pamoja waweze kukomesha uharifu huo.


TAARIFA KAMILI YA TANGANYIKA LAW SOCIETY:

TAARIFA KWA UMMA

SUALA LA MWANANCHI ALIYEDHANIWA KUWA WAKILI AMBAYE TAREHE 23 MEI 2023
ALIRIPOTIWA KUFANYA FUJO KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI – KISUTU – DAR ES

SALAAM

Chama cha Sheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS) kinapenda kutoa taarifa kwa Wanachama wake na umma wa Watanzania kuhusiana na tukio lililotokea tarehe 23 Mei 2023 katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi – Kisutu, Dar es Salaam. Katiko tukio hilo, vyombo vya habari vilitoa taarifa kuwa mtu aliyefahamika kwa jina la Baraka Mkama na ambaye alitambulishwa kama wakili alionekana akiwazuia askari Polisi wasiwatie nguvuni wateja wake baada ya kuachiwa huru na Mahakama.

Baada ya kupokea taarifa hizo, tarehe 24 Mei 2023, Baraza la uongozi la TLS lilifanya kikao cha dharura na kuamua kuteua Kamati Teule ya Uchunguzi ambayo ilipewa hadidu za rejea za kufanya uchunguzi wa haraka na wakitaalam wa tukio hilo, kisha kuujulisha uongozi wa TLS kwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria. Kamati hiyo ya watu wa nne ikiongozwa na Mwenyekiti wa TLS Tawi la Ilala, ilianza kazi yake tarehe hiyo hiyo 24 Mei na kukamilisha taarifa yake jana tarehe 26 Mei 2023. Kamati ilifanikiwa kumhoji mhusika – Baraka Mkama; na kisha mazungumzo na Jeshi la Polisi, Uongozi wa Mahakama pamoja na baadhi ya Mawakili waliokuwa na taarifa za tukio hilo. Kamati pia ilipitia mfumo wa usajili wa Mawakili (e-Wakili) ili kujiridhisha kuhusu taarifa za Baraka Mkama. Katika mahojiano na kamati, Mkama alikiri kuwa yeye sio wakili ingawa amekuwa akifanya kazi kama wakili tangu mwaka 2019. Vilevile katika mashauri aliyokuwa anayasimamia akiigiza kama wakili, alikuwa akiwatoza wateja wake shs milioni 3 na kuendelea kwa kesi.

Baada ya kupokea taarifa ya kamati, Baraza la Uongozi la TLS liliipitia na kuijadili, kwa hivyo, tunapenda kuwafahamisha Wanachama wote wa TLS, Wadau wa TLS na Umma wa Watanzania kwamba, TLS TUMEJIRIDHISHA PASIPO SHAKA KWAMBA MHUSIKA WA TUKIO HILO NDUGU BARAKA MKAMA SIO WAKILI NA SIO MWANACHAMA WA TANGANYIKA LAW SOCIETY.

Kwa sababu hiyo, TLS itashirikiana na vyombo vya dola na vyombo vya utoaji haki ili kuhakikisha kuwa hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa dhidi ya mhusika, pamoja na watu wengine kama yeye ili kukomesha tabia hii ambayo inaelekea kuenea maeneo mengi nchini.

Katika kufuatilia tukio hili, TLS imepata taarifa muhimu za ziada kuhusu mtandao wa watu wasiokuwa mawakili wanaofanya kazi za uwakili (Vishoka) hivyo imeongezea muda Kamati Teule ya Uchunguzi kuendelea kufuatilia mtandao huo na kuwasilisha taarifa zake za ziada ifikapo tarehe 31 Mei 2023. Vilevile, TLS imekamilisha kuunda kikosi kazi (Anti-Vishoka Taskforce) kitakachofanya kazi ya kudhibiti watu ambao hawastahili kufanya kazi za mawakili. Baraza la Uongozi la TLS linaomba ushirikiano toka kwa Wanachama wa TLS, Wadau wa TLS na Wananchi katika hizi juhudi za kutokomeza uhalifu huu.

TLS inawakumbusha wananchi na wadau wake wote kila wakati kuhakiki taarifa za watu wanaoruhusiwa kufanya kazi za mawakili kwa kutumia mfumo wa utambuzi wa wakili wa Mahakama yaani e-wakili. TLS itahakikisha kuwa inalinda na kusimamia maslahi ya mawakili; itawalinda na kuwatetea wananchi dhidi ya vishoka; na kushirikiana na vyombo vya dola katika kudumisha hadhi, nidhamu na heshma ya Mawakili kama maafisa wa Mahakama wakati wote.

Imetolewa leo tarehe 27 Mei 2023 na Baraza la Uongozi la TLS

Harold Giliard Sungusia

Rais Wa TLS – 2023/24
 

Attachments

  • TAARIFA KWA UMMA.pdf
    436.1 KB · Views: 5
TLS njooni Jf, mtuambie sheria inasemaje kama mukama ni wakili kishika na alisimamia kesi nyingi akashinda?

Je hizo kesi zitafutwa?

2. Ni nini Matokeo ya mteja kuwa na wakili kishoka mahakamani?

3. TLS mukama Ana elimu gani? kumbe-mkama-siyo-wakili-tls-yamkana

4. Mbona wakati wa uchaguzi wa Rais wa TLS mukama Ali kuwepo ukumbini na alikuwa mkpiga Kura halali?
 
Kuna mkuu wa kitengo cha sheria katika halmashauri fulani hakua wakili bado hivyo katika kesi zinazohitaji mwenye mhuri watu wa chini yake ndiyo walikua wanaziingia.

Sikumbuki vizuri ila kisheria alikua anaweza kumuwakilisha mwajiri wake to some extent na siyo zaidi ya hatua fulani au ni anaweza wakilisha taasisi ila siyo mtu binafsi.

Huyu Mkama kuanzia 2019 alishindwa kwenda law school?
 
Mimi nashauri apewe cheti , maana amedhiirisha kuwa anaweza kazi na Anaimudu .
Hivyo apewe Muhuri maisha yaendelee.
 
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimejitenga na ‘Wakili’ Baraka Mkama anayedaiwa kusababisha vurugu katika lango kuu la kuingilia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kikisem sio wakili na wala sio mwanachama wa chama hicho cha kitaaluma.

Mkama anadaiwa kusababisha taharuki hiyo Jumanne Mei 23, 2023 katika mahakama hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwazuia Polisi wasiwakamate upya washtakiwa aliokuwa anawatetea mahakamani hapo ambao walifutiwa kesi yao, hali iliyosababisha kukamatwa kwake.

Hata hivyo baada ya taarifa hiyo kuruka katika vyombo vya habari ikiwemo gazeti la Mwananchi na mitandao yake ya kijamii, taarifa ziliibuka kuwa Mkama sio Wakili na hata namba ya uwakili aliyoitaja wakati anahojiwa na TLS haikuwa yake bali ya Wakili mwingine na ndipo Baraza la TLS lilipounda timu kuchunguza sakata hilo.

Taarifa iliyotolewa leo Julai 27, 2023 na kusainiwa na Raisi wa TLS, Harold Sungusia imeeleza baada ya TLS kupokea taarifa ya uchunguzi uliofanywa na timu uliyounda imejiridhisha pasina shaka kuwa Mukama sio wakili wala mwanachama wa TLS na hata katika mfumo wa usajili wa mawakili (e-wakili) hayupo.

Mei 24, 2023 TLS iliunda timu ya mawakili watano kuchunguza sakata la ‘Wakili’ Mkama anayedaiwa kusababisha vurugu katika eneo hilo la Mahakama.

Walioteuliwa kufanya uchunguzi katika sakata hilo ni Mawakili Magreth Mwihava (Mwenyekiti), Hekima Mwasipu (mjumbe) Emanuel Augustine (mjumbe) na Anastazia Muro ambaye ni Katibu wa timu.

Timu hiyo pamoja na mambo mengine ilifanya uchungu wa kina kwa kumfanyia mahojiano Mkama mwenyewe, Uongozi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jeshi la Polisi, Ofisa wa Polisi aliyehusika katika sakata hilo, na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, ili kujua sababu za vurugu hizo na kuangalia katika mfumo wa e-wakili.

Hata hivyo, Ijumaa Mei 26, 2023 timu hiyo iliyongozwa na Mwenyekiti wa TLS Tawi la Ilala, Margreth ilikabidhi ripoti ya uchuguzi kwa Baraza la TLS kwa ajili ya uamuzi.

Taarifa hiyo inasema katika mahojiano yaliyofaywa baina ya Mkama na timu hiyo, alikiri kuwa yeye sio wakili ingawa amekuwa akifanya kazi kama wakili tangu mwaka 2019.

Pia katika mashauri aliyokuwa anayasimamia akiigiza kama wakili, alikuwa akiwatoza wateja wake kiasi cha Sh3 milioni na kuendelea kwa kesi na kwamba katika mfumo wa usajili wa Mawakili (e-Wakili) ilibainika kuwa Mukama sio mwanchama wa TLS.

“Kwa sababu hiyo, TLS itashirikiana na vyombo vya dola na vyombo vya utoaji haki ili kuhakikisha kuwa hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa dhidi ya muhusika, pamoja na watu wengine kama yeye ili kukomesha tabia hii ambayo inaelekea kuenea maeneo mengi nchini,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;

“Katika kufuatilia tukio hili, TLS imepata taarifa muhimu za ziada kuhusu mtandao wa watu wasiokuwa Mawakili wanaofanya kazi za uwakili (vishoka) hivyo imeiongezea muda Kamati teule ya uchunguzi kuendelea kufuatilia mtandao huo na kuwasilisha taarifa zake za ziada ifikapo Mei 31, 2023.”

Kwa upande mwingine, TLS imeunda kikosi kazi (Anti-Vishoka Taskforce) kitakachofanya kazi ya kudhibiti watu ambao hawastahili kufanya kazi za mawakili.

Kwa mantiki hiyo, Baraza la Uongozi la TLS linaomba ushirikiano toka kwa wanachama wake na wadau wengine pamoja na wananchi ili kwa pamoja waweze kukomesha uharifu huo.

Sakata la Mkama:
Itakumbukwa kuwa sakata la Mkama lilitolea Mei 23, 2023 katika Mahakama hiyo, baada ya washtakiwa Khalid Somoe (54), Raphael Lyimo (40), Betty Mwakikusye (41), Abdiel Mshana (57), kufutiwa kesi ya jinai namba 99/2019.

Kesi hiyo ilifutwa na Hakimu Mkazi Mkuu Romuli Mbuya, baada ya Wakili wa utetezi, Agatha Fabian na Baraka Mkama kuwasilisha maombi ya kuifuta kesi hiyo kutokana na kutoendelea kwa muda mrefu.

Hata hivyo muda mfupi baada ya Mahakama kuwafutia kesi, askari polisi waliokuwa wakilinda usalama katika mahakamani hapo, waliwakamata washtakiwa hao na katika harakati hizo, alijitokeza Mkama na kuanza kuzuia wateja wake wasikamatwe.

Hali hiyo ilizua taharuki ambayo ilisababisha akamatwe na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi na kisha kupelekwa kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya uchunguzi.

Mwananchi
alijitakia angekaa kimya pengine angeendelea kula pesa za vipofu. Ila mwizi arobaini. Alijidhihirisha wazi tu, we huwezi kumzuia askari wa jeshi la polisi kufanya km una akili timamu. Ametorosha mhalifu moja ktk wale waliokuwepo pale. Alikuwa anafanya mambo ya kipupmbavu.
 
TLS njooni Jf, mtuambie sheria inasemaje kama mukama ni wakili kishika na alisimamia kesi nyingi akashinda?

Je hizo kesi zitafutwa?

2. Ni nini Matokeo ya mteja kuwa na wakili kishoka mahakamani?

3. TLS mukama Ana elimu gani? kumbe-mkama-siyo-wakili-tls-yamkana

4. Mbona wakati wa uchaguzi wa Rais wa TLS mukama Ali kuwepo ukumbini na alikuwa mkpiga Kura halali?
ulikuwepo wakati wa upigaji kura? Ilipigwa wapi na lini.
 
Hii nchi hata kama umesoma na ukahitimu vyema kama haupo kwenye hivi vyama vinayosimamia ulichosomea jina litakalokufaa ni kishoka..

Hivi vyama inapaswa kuwa ni hiari ya mtu kujiunga navyo na si kwa kulazimishana ili tu kupata ada za wanachama.
 
Back
Top Bottom