TLS na viongozi "Radical"

Kubwa jinga limezoea uchawa na kujipendekeza. Ulitaka waendelee kuwa ma-chawa wa CCM kama walivyokuwa! Utapiga kelele sana lakini wananchi tuko nyuma yao.
 
Nchi yoyote ile ambayo Ina wananchi wenye uelewa mkubwa na wenye misimamo mikali isiyoyumba (radicals or extremists), daima huwa kunakuwa na Utawala ambao umestaarabika na unaotenda haki. And vice versa is true.
 
misimamo mikali ndani ya Tanganyika Law Society (TLS)

Msimamo mkali wa kutetea umma mpana na siyo kuwa chawa wa viongozi walafi, wezi wa mali za raia na taifa ndiyo wanatakiwa kwa wingi.

Nasi wananchi tuwaunge mkono viongozi watetezi wa haki za raia na mali zao, badala ya kuwabeza au kuwaita majina ya kujaribu kuwatisha .
 
nadhani kuna tatizo katika tasnia nzima ya sheria, society inayoundwa na wasomi watupu inakuwa na viongozi kama fatma lissu mwambukusi naona kuna tatizo mahala, nilitegemea taasisi kama hiyo iongozwe na wasomi kisomi, nilitegemea kiwe chombo cha kuishauri serikali kuisaidia serikali badala yake kinakuwa cha kupambana na serikali
 
Kwa iyo raisi yeye hataki mtu nyeenda against hata km anakosea this is nonsense hatuwez kujenga nchi kwa style yaani mtu aone loophole akishauri afu aendelee ndio mzee and ameeona kuna mashimo ndo mana tunapoteana kwenye kesi za kimataifa our president anabid ajue binaadamu wote sawa chini ya sheria na katiba ya Tanzania hiz za kusema anaangalia sura hyu anaenda against mie simshirikishi its too personal bado tuna safari ndefu mnooo kufika tunapopataka.
 
Kuwa na viongozi wenye misimamo mikali ndani ya Tanganyika Law Society (TLS) kunaweza kuleta athari kadhaa mbaya kwa chama hicho, ingawa pia kuna faida. Hapa chini ni baadhi ya athari mbaya zinazoweza kutokea...
Kwahiyo wakiwa wapolewapole na wanyenyekevu kwa serikali ndiyo wanachama hawatagawanyika?
 
Tumaini la watanzania limebaki Kwa TLS pekee chini ya mwambukusi taasisi zingine zimekuwa chawa wa serikali kama huyu mleta mada.
 
Kuwa na viongozi wenye misimamo mikali ndani ya Tanganyika Law Society (TLS) kunaweza kuleta athari kadhaa mbaya kwa chama hicho, ingawa pia kuna faida. Hapa chini ni baadhi ya athari mbaya zinazoweza kutokea...
Nchi yoyote ile ambayo Ina wananchi wenye uelewa mkubwa na wenye misimamo mikali isiyoyumba (radicals or extremists), daima huwa kunakuwa na Utawala ambao umestaarabika na unaotenda haki. And vice versa is true
Msimamo mkali wa kutetea umma mpana na siyo kuwa chawa wa viongozi walafi, wezi wa mali za raia na taifa ndiyo wanatakiwa kwa wing...
Wewe kumbe bado hujagundua lengo la mleta mada, huyo anachojaribu ni kufanya "Characters Assassination and Smear Campaign" dhidi ya Viongozi wa TLS waliopo hivi sasa ili kujaribu kuwapunguzia ushawishi wao kwa umma baada ya kuona kwamba "Sponsor" wao anakabwa Koo Sana na TLS.
 
Hasara kubwa kwa sababu TLS itatekwa nyara na kuwa chombo cha mapambano badalq ya mashauriano na mashauri
Yes ni vzur wakawa watiifu na wakawa wanaimba nyimbo na pambio za kuisifu serikali ili wapate teuzi
Yes pia hujaweka hasara ya kukosa teuzi za kua majaji ni vzur wakawa watiifu na wakawa wanaimba nyimbo na pambio za kuisifu serikali ili wapate teuzi ,,,
 
miaka ya 435bc ulikuwepo utawala wa wagiriki, walikuwepo wanafalsafa akina socretes plato na wasomi waliojulikana kama sophiest, zilitungwa sheria za kila aina ngumu na zenye misimamo mikali, nchi ilianguka kiuchumi, na hatimae walivamiwa na utawala wa warumi, socretes alijinyonga kukwepa kuwa mwana falsafa kama yeye angeweza dhalilishwa na utawala wa kirumi iwapo wangemkamata. hivyo kuwa extrimist haimaanushi kuwa tutajenga familia iliyoendelea na ya kistaarabu
 
TLS ilipokuwa chombo cha mashauriano na mashauri chini ya Edward Hosea na Harlod Sungusia raia walifaidikaje?
Kwa mantiki ya hoja yangu mimi ndo nikuulize walipokuwepo radical walifanikisha kipi cha pekee kwa maendelea ya sheria, na jamii. Swali ni lako mkuu. Asante
 
Kwa mantiki ya hoja yangu mimi ndo nikuulize walipokuwepo radical walifanikisha kipi cha pekee kwa maendelea ya sheria, na jamii. Swali ni lako mkuu. Asante
Wote mnazunguka palepale tu, hiyo taasisi siasa za kutoka upinzani zinai-overrate sana ikiwa kiuhalisia haina impact yoyote
Akiwa anaefanya mashauriano na maelewano na serikali bado hakuna impact kwa mwananchi yoyote
Pia akiwepo radical hakuna impact yoyote kwa mwananchi

TLS is overrated
 
Toka hapa. Socrates alikufa mwaka 399BC na Plato alikufa mwaka 348, himaya ya wagiriki ilianguka mikononi mwa Warumi mwaka 146BC
 
Hakuna mgongano wowote, wanachotaka hao ni TLS isifanye majukumu yake ili waje kusema TLS na Mwabukusi wamenunuliwa.
Hao ni wapiga kelele wasio na uwezo wa kufanya reasoning matokeo yake kila atakachoongea Mwabukusi wakiina kipo dhidi ya serikali basi wanakuja na propaganda za kwamba ni msimamo wake binafsi. Wakati mwenzao anaongea akitumia machinery za TLS wao wanatumia bundle zao tu na huenda hata si wanachama wa TLS.
 
Kwa mantiki ya hoja yangu mimi ndo nikuulize walipokuwepo radical walifanikisha kipi cha pekee kwa maendelea ya sheria, na jamii. Swali ni lako mkuu. Asante
Radicals ni wakina nani na wasio radicals ni wakina nani na waliisaidia nini TLS?
Au unadhani TLS ni kama CCM ambapo kila tamko la mwenyekiti mnaungana kuunga mkono kwa vifijo?
 
nadhani TLS inaweza kubadilika na kua chama cha siasa pia kwa uelekeo huu
 
Raia wa kawaida wananufaika/walinufaika na nini pindi TLS inapokuwa/ilipokuwa imeshikamana na Serikali?
Hapo we jamaa hayo yote uliyoyasema ni kwa maono yako na unaonekana wazi unaunga mkono matendo maovu ila umeona noma tu kueleza kinaga ubaga unachokifikiria jaribu tu kupitia upya bandiko lako na uone kama kuna lolote ambalo viongozi TLS wameenda kinyume na sheria hamna cha mgogoro wala nini zaidi ni ubakwaji wa demokrasia unaofanywa na gavooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…