TLS haitausahau uongozi uliotukuka wa Tundu Lissu

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,549
3,722
Ndugu wanabodi, salamu mbele!

Ikiwa leo ni siku ambayo chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) wanafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wake kuanzia kwa wajumbe wa baraza la viongozi mpaka Rais. Ikiwa ni jana tu Mheshimiwa Rais wa TLS Tundu Lissu amehutubia mkutano wa TLS akiwa Ubeligiji na kuaga rasmi. Tundu Lissu hatasahaulika katika uongozi wake makini na shupavu ndani ya TLS.
Amekuwa Rais wa mfano ambaye sasa hivi kila mgombea Urais TLS anaahidi kufuata nyayo zake ili tu akubalike miongoni mwa wapiga kura.

Tundu Lissu ndiye Rais pekee aliyefanikiwa kusimamisha jengo la Ofisi za TLS lililowashinda marais wote waliopita TLS.

Tundu Lissu amefanikiwa kupunguza mzigo wa ada kwa wanachama wa TLS.

Tundu Lissu amekuwa mtetezi wa wanyonge na hata mawakili wanapopatwa na matatizo, wengi mtakumbuka alivyolichukulia kwa uzito swala la kupigwa mabomu kwa ofisi ya mawakili ya IMMA Advocate.
Ndiye Rais aliyeifanya TLS ikajulikana na kusifika mbele ya jamii.
Yapo mengi ya kuelezea naomba niishie hapa kwa leo
IMG-20180414-WA0020.jpg
IMG-20180414-WA0023.jpg
 
Tanzania inahitaji huyu mtu sana. Na Mungu anampango mkubwa sn na huyu bwn
 
Tukiachana ni itikadi Tundu Lissu Binafsi Napenda ,Hasa hasa Mungu ambariki ampe Afya njema amponye majeraha kutokana na kisa Kushambuliwa kwa risasi Naamini Mungu ana makusudi yake juu ya Lissu
 
Back
Top Bottom