Msaada kuhusu tatizo la tumbo kwa Mtoto

Jaylee

Member
Apr 15, 2009
64
93
Ni mtoto wa kiume miaka minne na nusu mwenye afya ya kawaida na uzito kg 21 anasoma chekekea. Hajawahi kupata msukosuko wowote mkubwa wa kiafya na anahudhuria klinik ya watoto kila nwezi.

Kuanzia mwaka jana amekuwa analalamika maumivu ya tumbo ya mara kwa mara ila vipimo vya hospitali havionyeshi tatizo lolote la tumbo au hata minyoo. Hivi karibuni amekuwa anapata tatizo la tumbo la kujirudia rudia likiambatana na homa kali ambavyo hutoweka na kurudi walao mara mbili kwa mwezi.

Nyakati zote hizo huwahishwa hospitali na kupewa matibabu baada ya kupimwa vipimo basic vya damu, mkojo na stool ili kubaini tatizo la Malaria, UTI, typhoid na hivyo vyote huonyesha hana uambukizo wa aina yoyote na yupo HIV negative.

Ninaomba msaada wa ushauri wa kitaalamu kwa JF Doctors, je mtoto huyu atakuwa na tatizo gani kwa kuzingatia kuwa linajirudia kwa frequency ya wastani wa kila wiki mbili sasa?

Kama huna ushauri naomba upite kimya kimya nahitaji wabobezi wanisaidie.

Natanguliza shukrani kwenu
 
Sasa Kama vipimo vya hospital vinadai hamna tatizo unataka watalaam gani wengine waseme me labda nakushauri uende hospital kubwa kubwa zinazofanya diagnosis km regency au muhimbili..tuambie Kwanza hospital ulizokwenda Ni za hadhi gani
 
Pole ..na Salaama yake Prince.
Uchungu wa mwana...
Tiba mbadala:-
Always drink tea with ginger (powder au prickles).
Maji ya kunywa yawe warm always.
Kutomshindilia chakula kingi.
inshaAllah apate uponyi haraka na afya tele.
 
Sasa Kama vipimo vya hospital vinadai hamna tatizo unataka watalaam gani wengine waseme me labda nakushauri uende hospital kubwa kubwa zinazofanya diagnosis km regency au muhimbili..tuambie Kwanza hospital ulizokwenda Ni za hadhi gani
Usimjibu hivo mkuu, kumbuka kuna magonjwa mengine yanatibiwa kienyeji.
Pia hata ushauri tu wakati mwingine ni dawa
 
Pole sana mkuu. Mtoto wako anahitaji further evaluation ya kuonwa na daktari bingwa wa watoto (pediatrician) katika hospitali ambayo inafanya vipimo zaidi beyond UTI, Typhoid, stooll analysis.

Uko mkoa gani? I may recommend you which hospital to go to, or which pediatrician to see kulingana na mkoa uliopo (If you wish so), otherwise uende hospitali yoyote kubwa na uombe kwamba unahitaji kuattend clinic ya PAEDIATRICIAN.

Pole sana mkuu. Jaylee
 
Huyo ana henia (ngiri) afanyiwe tu uchunguzi ana ngiri ya aina gani ili akifika makamo kidogo kama miaka 10 hivi afanyiwe operation
 
Mrejesho: Mtoto alipata fursa ya kuonwa na mmoja wa madaktari bingwa maarufu wa magonjwa ya watoto hapa jijini Dar. Baada ya kumfanyia uchunguzi wa kitaalam hakugundulika kuwa na tatizo lolote kubwa isipokuwa Daktari alihoji iwapo mtoto anatumia dawa ya meno (tooth paste) na iwapo anatumia juisi za dukani, na jibu likawa ndiyo.

Daktari alimwandikia antibiotic na dawa ya maumivu na kushauri kuwa asitumie dawa ya mswaki kwa sasa na pia asipewe tena juisi za viwandani na badala yake apewe matunda fresh.

Nadhani wazazi wanalo jambo la kujifunza kutokana na tukio hili. Nawashukuru nyote mliojitokeza kutoa ushauri.
 
Mrejesho: Mtoto alipata fursa ya kuonwa na mmoja wa madaktari bingwa maarufu wa magonjwa ya watoto hapa jijini Dar. Baada ya kumfanyia uchunguzi wa kitaalam hakugundulika kuwa na tatizo lolote kubwa isipokuwa Daktari alihoji iwapo mtoto anatumia dawa ya meno (tooth paste) na iwapo anatumia juisi za dukani, na jibu likawa ndiyo...
Muwache kutumia Ma-Juisi feki na dawa za miswaki zenye sumu kwa watoto. Nchi yetu imebarikiwa matunda yapo mengi munatumia majusi ya maboksi? Loohhh Majangaa kweli haya auguwe pole mwanao.
 
Back
Top Bottom