Rais anao wasaidizi waliosomea fani za Idara au Kitengo husika. Katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu japo Kampeni hazijaanza rasmi kwa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, lakini ukweli ni kwamba tupo busy na Kampeni. Ukizunguka huku na kule utaona mapikipiki, khanga, baiskeli nk.
Hivi karibuni tunaona Kampeni zimehamia kwenye vyombo vya habari kama vile mitandao ya Kijamii. Kila uchao utaona maandishi, "Mkoa fulani Rais Samia kaongeza bilioni kadhaa kwenye sekta fulani kutoka bilioni kadhaa zilizokuwepo miaka minne iliyopita.
Ni jambo jema kwa wasaidizi hao wa Rais kufanya yote hayo. Pamoja na hayo wasaidizi hao walitakiwa kufanya counter check au follow up ili kujua Kampeni hizo zinapokelewaje na wananchi hasa wa kawaida.
Si jambo la siri kuwa pamoja na maboresho katika sekta zinazosemwa kuwa zimeboreshwa, bado wananchi wanapoenda kupata huduma katika maeneo husika wanakumbana na changamoto lukuki zaidi ya ilivyokuwa kabla ya maboresho yaliyofanywa na Rais Samia.
Kwa mfano unamwambia mtu hospitali ya Mkoa ilikuwa Ina CT Scan mbili miaka minne iliyopita leo Rais Samia kaongeza vifaa hivyo 400, kama mwananchi anaenda kupata huduma inayohusisha kifaa hicho Kuna kuwa na changamoto za njoo kesho, njoo kesho kutwa, njoo wiki ijayo, Hapo anaambiwa kijanja ajiongeze ( atoe rushwa a.k.a hela ya maji).
Mwananchi huyo ambaye hakuona changamoto hizo wakati ST Scan zilipokuwa mbili, unapomwambia leo Samia kaongeza ST Scan 400 anakuelewa??? Huu ni mfano mmoja tu.
Mtu akizungumza mema na mazuri yaliyofanywa na Serikali wakati wa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli,baadhi ya watu wa kawaida na hata wakubwa wanatoa mapovu. Lakini ukweli ni kwamba Samia na Magufuli wakati ule walifanya kazi kubwa ndani ya muda mfupi. Uwajibikaji Serikalini uliimarika kwa kiwango kikubwa mno. Mambo ya njoo kesho mara wiki ijayo kauli za kuchochea mazingira ya rushwa yalipungua mno. Leo nenda maofisini uone, nenda Polisi uone, nenda Mahospitalini uone. Wananchi wa kawaida tunajua yanayoendelea huko.
Serikali ya Rais Samia imetekeleza hayo, sawa vema, swali ni kwamba kama mwananchi wa kawaida hapati huduma Bora, kwa wakati na bila mizengwe, maboresho hayo yana msaidia Nini? Kampeni hiyo inamsaidia Nini Rais Samia??
TISS, TAKUKURU na Idara nyingine za Serikali mpo, huo ni wajibu wenu tunawalipa kwa Kodi zetu. Msaidieni Mheshimiwa Rais.