TISS, Jichunguze ili Muepuke Kuchunguzwa

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Siungi mkono TISS kuundiwa tume ya uchunguzi ya wazi.

Chombo hiki ni muhimu si kwa kizazi hiki, chama hiki wala serikali hii, bali ni kwa mustakabali wa taifa lililopo na lijalo. Sikubaliani na wanaokipa chombo hiki "Umungu" kuwa hakikosei, lakini nachelea kusema kuwa kuna mambo hayaendi vizuri na hasa sasa kwa hivi wakati tuna mkulu ambaye ni mgeni sana katika chombo hiki.

Ili kuepuka mambo mengi kusambazwa na kumwaga hadharani na hatimaye kuhatarisha maisha ya wazlendo wengi sana walio katika chombo hiki, nashauri chombo kijichunguze na kionekane kimejichunguza kweli kweli. Yanatakiwa mabadiliko makubwa ya tabia na mafunzo. Kuwadharau wazee na wana taasisi wa zamani hakusaidii kwa sasa. Ebu tazama haya kama mfano:

- Ilikuwa marufuku kwa mwana taasisi hii, kukamata (arrest) au hata kuhoji (interogate) hadharani. Daima amri ya kukamata ilipelekwa polisi na Afisa wa juu kwa Afisa wa juu wa polisi. Mtuhumiwa alikamatwa na polisi na kuweka ndani kwa "kunyimwa dhamana". Wana taasisi walimchukua baadaye kwa muda wao na kumhoji ili kupata walichokihitaji, kisha walimrudisha polisi. Ilipobidi polisi walifungua mashtaka feki na kesi kufukuzwa baadaye. Hii ilisaidia mtuhumiwa kufikiri waliomhoji ni polisi wakati hata wana taasisi wamehusika. Ni nani aliruhusu kukamatwa (sasa kunaitwa kutekwa) kwa Roma Mkatoliki na kusababisha uzembe mbaya namna hii.

- Ilikuwa marufuku kwa mwana taasisi kuonyesha kitambulisho chake kwa matukio madogo madogo. Siku hizi eti mwana taasisi anasimamishwa barabarani na Trafiki na hapo hapo anatoa kitambulisho kumtisha trafiki huyo! Mwana taasisi wa kweli alikuwa anaweza hata kukamatwa anakunywa gongo, kuwekwa pingu, na kulala ndani kwa siku mbili bila mdhamana. Mwana taasisi alikwa anaweza kukamatwa na maafisa wengine wa serikali katika mkoa mwingine wasiomfahamu na asijitambulishe. Siku hizi, vitambulisho vya taasisi vinatumika hata uwanja wa taifa kuingilia kutazama mechi.

-Ilikuwa marufuku kwa mwana taasisi kuonyesha silaha hadharani. Jamani hata walinzi wa viongozi bado wanaficha silaha sembuse mtu aliyekwenda kuvinjali na kutathmini hali ya kusanyiko la kawaida. Hulka hii inahatarisha maisha ya wengine na kujenga chuki ya jamii dhidi ya taasisi. Lilipotokea kosa na namna hii, uchunguzi ulienda mbali kuanzia alivypatikana, alivyofundishwa na nani alimpa kazi (assignemnt) iliyosababisha afanye kosa la kujilipua. Kwa wachunguzi makini, lazima wangegundua kasoro katika maeneo hayo matatu.

- Pamoja na kwamba ni wana taasisi ni maaskari, lakini ni kosa kwa mwana taasisi kupokea na kutekeleza amri ya "kijinga". Mwana taasisi daima hushikilia mikononi mwake uhai wa aina tatu: uhai wake, wa wana taasisi wenzake na wa nchi. Amri inayohatarisha mojawapo ya hayo, hukubaliwa kwa maandishi si kwa maneno wala simu.

Hapa tulipofikishwa, kimya cha taasisi hakisaidii. Kina Lizaboni na kazi za kujituma kwenye mitandao hakusaidii. Utii kwa mamlaka za juu bila kujali uendelevu wa taasisi baadaye, hausaidii. Kuivunja bila kufikiri hakusaidii. Mwalimu aliivunja mwaka 1964 na kuiunda upya lakini kulikuwa na sababu kubwa. Uhuru wa taasisi hii ni muhimu pengine kuliko chombo kingine chochote isipokuwa mahakama. Mwalimu aliwahi kufanya uamuzi mgumu binafsi ili kulinda uhuru wa chombo hiki kikiwa bado kichanga. Mandela alikubali kufanya uamuzi mgumu binafsi wa kutengana na mkewe Winnie pale alipobaini kuwa alikuwa anakiingilia chombo hiki. Ili kuficha ukweli huu, alitumia sababu nyingine zinazotamkika ili kupunguza maswali katika jamii. Mkuu asiyeheshimu uhuru wa chombo hiki ni hatari kwa mshikamano wa nchi (sitaki kusema usalama wa nchi).

Mwana taasisi aliyeingia kwa kupindisha baadhi ya vipengere aondolewe hata kama nashikilia funguo za "chungu" au "ashugulikiwe" kipekee.

No person is greater than a nation

---/Baija
 
Mtoa mada nikupongeze kwakuwa umejitofautisha na watu wengi sana katika kufikiri.

Umetoa a constructive criticism against a status quo. Kwa yale mawazo yenye ukweli tuombe yachukuliwe ila mengine kama hayana tija yatupiliwe mbali. Kwasababu wengi tunaongea tu ila hatujui hawa jamaa wamejipanga vipi katika utendaji wao wa kazi wa kilasiku....
 
Post ina mashiko. vijana wa siku hizi nafikiri vetting haifanyiki sawasawa, make wengi ktk taasisi hii wanatamani wajulikane wao ni nani. Nafikiri kuna mahala tumekosea ni vyema tujisahihishe sasa kuinusuru taasisi..
 
TISS haichunguzwi na hilo Bunge wala TISS haita chunguzwa na Kamati yoyote ya Bunge la Jamhuru ya Muungano wa Tanzania.

Na Wabunge wote wa najua kuwa hawawezi kuichunguza TISS kwa mujibu wa kanuni za Bunge.
 
Sawa TISS haichunguzwi na hivyo hivyo haikamati!, hapo kuwa sasa hivi imeanza kukamata/kuteka na kupoteza kama inavyo tuhumiwa sasa hivi. Shinikizo la kuchunguzwa limekuja baada ya wao kukiuka taratibu. Lakini pia Sheria inayi ongoza usalama wa taifa kama haiweki namna ya kuwa wajibisha, basi nayo ina mapungufu kwani wale siyo melaika!!!!! .........na sasa ndo watuhumiwa!!. Utasema waachwe?????.
 
Hakuna ushahidi wowote kuwa TISS ndiyo wako nyuma ya yote yanayotokea hapa nchini kama tunavyosikia huko Bungeni wakina Zitto,Bashe na wengine wakisema wana ushahidi.

Kama kila kitu wanacho na ushahidi wanao basi mahali salama kwao ni kwenda kufungua jarada Polisi ili kesi ifunguliwe dhidi ya Idara hii then nyeupe na nyeusi itajulikana mbele ya Mahakama.

Ila suala kuifanyia uchunguzi eti kupitia Kamati za Bunge kanuni hazuruhusu na haitafanyika.
 
Siungi mkono TISS kuundiwa tume ya uchunguzi ya wazi.

Chombo hiki ni muhimu si kwa kizazi hiki, chama hiki wala serikali hii, bali ni kwa mustakabali wa taifa lililopo na lijalo. Sikubaliani na wanaokipa chombo hiki "Umungu" kuwa hakikosei, lakini nachelea kusema kuwa kuna mambo hayaendi vizuri na hasa sasa kwa hivi wakati tuna mkulu ambaye ni mgeni sana katika chombo hiki.

Ili kuepuka mambo mengi kusambazwa na kumwaga hadharani na hatimaye kuhatarisha maisha ya wazlendo wengi sana walio katika chombo hiki, nashauri chombo kijichunguze na kionekane kimejichunguza kweli kweli. Yanatakiwa mabadiliko makubwa ya tabia na mafunzo. Kuwadharau wazee na wana taasisi wa zamani hakusaidii kwa sasa. Ebu tazama haya kama mfano:

- Ilikuwa marufuku kwa mwana taasisi hii, kukamata (arrest) au hata kuhoji (interogate) hadharani. Daima amri ya kukamata ilipelekwa polisi na Afisa wa juu kwa Afisa wa juu wa polisi. Mtuhumiwa alikamatwa na polisi na kuweka ndani kwa "kunyimwa dhamana". Wana taasisi walimchukua baadaye kwa muda wao na kumhoji ili kupata walichokihitaji, kisha walimrudisha polisi. Ilipobidi polisi walifungua mashtaka feki na kesi kufukuzwa baadaye. Hii ilisaidia mtuhumiwa kufikiri waliomhoji ni polisi wakati hata wana taasisi wamehusika. Ni nani aliruhusu kukamatwa (sasa kunaitwa kutekwa) kwa Roma Mkatoliki na kusababisha uzembe mbaya namna hii.

- Ilikuwa marufuku kwa mwana taasisi kuonyesha kitambulisho chake kwa matukio madogo madogo. Siku hizi eti mwana taasisi anasimamishwa barabarani na Trafiki na hapo hapo anatoa kitambulisho kumtisha trafiki huyo! Mwana taasisi wa kweli alikuwa anaweza hata kukamatwa anakunywa gongo, kuwekwa pingu, na kulala ndani kwa siku mbili bila mdhamana. Mwana taasisi alikwa anaweza kukamatwa na maafisa wengine wa serikali katika mkoa mwingine wasiomfahamu na asijitambulishe. Siku hizi, vitambulisho vya taasisi vinatumika hata uwanja wa taifa kuingilia kutazama mechi.

-Ilikuwa marufuku kwa mwana taasisi kuonyesha silaha hadharani. Jamani hata walinzi wa viongozi bado wanaficha silaha sembuse mtu aliyekwenda kuvinjali na kutathmini hali ya kusanyiko la kawaida. Hulka hii inahatarisha maisha ya wengine na kujenga chuki ya jamii dhidi ya taasisi. Lilipotokea kosa na namna hii, uchunguzi ulienda mbali kuanzia alivypatikana, alivyofundishwa na nani alimpa kazi (assignemnt) iliyosababisha afanye kosa la kujilipua. Kwa wachunguzi makini, lazima wangegundua kasoro katika maeneo hayo matatu.

- Pamoja na kwamba ni wana taasisi ni maaskari, lakini ni kosa kwa mwana taasisi kupokea na kutekeleza amri ya "kijinga". Mwana taasisi daima hushikilia mikononi mwake uhai wa aina tatu: uhai wake, wa wana taasisi wenzake na wa nchi. Amri inayohatarisha mojawapo ya hayo, hukubaliwa kwa maandishi si kwa maneno wala simu.

Hapa tulipofikishwa, kimya cha taasisi hakisaidii. Kina Lizaboni na kazi za kujituma kwenye mitandao hakusaidii. Utii kwa mamlaka za juu bila kujali uendelevu wa taasisi baadaye, hausaidii. Kuivunja bila kufikiri hakusaidii. Mwalimu aliivunja mwaka 1964 na kuiunda upya lakini kulikuwa na sababu kubwa. Uhuru wa taasisi hii ni muhimu pengine kuliko chombo kingine chochote isipokuwa mahakama. Mwalimu aliwahi kufanya uamuzi mgumu binafsi ili kulinda uhuru wa chombo hiki kikiwa bado kichanga. Mandela alikubali kufanya uamuzi mgumu binafsi wa kutengana na mkewe Winnie pale alipobaini kuwa alikuwa anakiingilia chombo hiki. Ili kuficha ukweli huu, alitumia sababu nyingine zinazotamkika ili kupunguza maswali katika jamii. Mkuu asiyeheshimu uhuru wa chombo hiki ni hatari kwa mshikamano wa nchi (sitaki kusema usalama wa nchi).

Mwana taasisi aliyeingia kwa kupindisha baadhi ya vipengere aondolewe hata kama nashikilia funguo za "chungu" au "ashugulikiwe" kipekee.

No person is greater than a nation

---/Baija

Umeandika vyema,lakini kwenye taasisi hii kuna Malimbukeni wamefichwa humo ambao ndiyo watekelezaji wa uchafu unaoendelea.

Kuna kesi ya Mwenyekiti wa UVCCM Arusha kutumia kitambulisho cha TISS kupora Mali za watu na kujipatia fedha mpaka Leo hakuna kinachoendelea,hivyo kwa akili za kawaida kabisa zinanifanya niamini kitengo hicho kuna UVCCM kwa jina la Green Guard wapo na inawezekana ndiyo watumishi vibaya wa taasisi hii.

Wazee walisema usipoziba UFA utajenga UKUTA.

Kaka UFA umeshakuwa mkubwa sana hapo hakuna namna ni kujenga UKUTA. Usipoujenga leo au sasa kesho utatubomokea.
 
Post ina mashiko. vijana wa siku hizi nafikiri vetting haifanyiki sawasawa, make wengi ktk taasisi hii wanatamani wajulikane wao ni nani. Nafikiri kuna mahala tumekosea ni vyema tujisahihishe sasa kuinusuru taasisi..

Vetting ya maana haifanyiki.Na hawa wanafanya upuuzi ni wale walioletwa kwa sababu maalu,wenye Serikali yao wanajua.

Siku Taasisi kama taasisi ikiamka nitafanya kazi inayotakiwa kufanya japo itakuwa imechelewa.

Ila Ufa umeshakuwa mkubwa Waache wake kujenga UKUTA.
 
Hakuna ushahidi wowote kuwa TISS ndiyo wako nyuma ya yote yanayotokea hapa nchini kama tunavyosikia huko Bungeni wakina Zitto,Bashe na wengine wakisema wana ushahidi.

Kama kila kitu wanacho na ushahidi wanao basi mahali salama kwao ni kwenda kufungua jarada Polisi ili kesi ifunguliwe dhidi ya Idara hii then nyeupe na nyeusi itajulikana mbele ya Mahakama.

Ila suala kuifanyia uchunguzi eti kupitia Kamati za Bunge kanuni hazuruhusu na haitafanyika.

Kama Bunge hawezi kuwagusa polisi itaweza?

Uzuri Taasisi yenyewe unajua kinachoendelea ila inakifumbia macho,siku wakiamua kufungua macho wanafanya kazi yao ika waswahili wanasema mchelea maana kulia atalia yeye.

Pili kumekuwa na tendency ya Uongozi mkubwa kuwatumia vibaya hawa jamaa zetu na sababu ya tumbo wameacha kufuata taaluma yao wanafuata tumbo.

Enzi za JKN hakuna Taifa lingethubutu kutuingilia na wala kusikia kelele zake tu,Leo Watanzania wanauawa na askari wa nchi jirani kesi inapelekwa kwa wahusika mwenye Mali yake anakatazwa kutumia kisa jirani anataka kutumia Raslimali zetu.

Kama mtakumbuka RAIA wasio na hatia 50 wameuawa mto Kagera Serikali badala ya kuwasaidia inatia onyo Kali kwa wenye MTO Kagera ati kuacha Mara moja kutumia MTO, ika Wale Wanyarwanda kule waendelee kunufaika ni ajabu na kweli lakini ndilo lililopo Leo.Nikamuuliza hawa Tiss maana yake ni kukaa ofisini tu??Au wamebadilishiwa kazi wamekuwa watekaji na watekaji wa RAIA wachokonozi??

Kwa sasa Taasisi hii haina moral authority ya kujichunguza sana kuvunjwa tu.
 
Chadema walivuma sana kwa matukio ya kifirauni utekaji na utesaji. Hawajaacha hao. Ndio watekelezaji wa haya yanayoendelea
 
Wilfred lwakatare aliwahi kunaswa akipanga mikakati ya utekaji watu. Leo ni mbunge. Kwanini tunawasahau hawa tuelekeza mashambulizi kwingine?
 
Kama Bunge hawezi kuwagusa polisi itaweza?

Uzuri Taasisi yenyewe unajua kinachoendelea ila inakifumbia macho,siku wakiamua kufungua macho wanafanya kazi yao ika waswahili wanasema mchelea maana kulia atalia yeye.

Pili kumekuwa na tendency ya Uongozi mkubwa kuwatumia vibaya hawa jamaa zetu na sababu ya tumbo wameacha kufuata taaluma yao wanafuata tumbo.

Enzi za JKN hakuna Taifa lingethubutu kutuingilia na wala kusikia kelele zake tu,Leo Watanzania wanauawa na askari wa nchi jirani kesi inapelekwa kwa wahusika mwenye Mali yake anakatazwa kutumia kisa jirani anataka kutumia Raslimali zetu.

Kama mtakumbuka RAIA wasio na hatia 50 wameuawa mto Kagera Serikali badala ya kuwasaidia inatia onyo Kali kwa wenye MTO Kagera ati kuacha Mara moja kutumia MTO, ika Wale Wanyarwanda kule waendelee kunufaika ni ajabu na kweli lakini ndilo lililopo Leo.Nikamuuliza hawa Tiss maana yake ni kukaa ofisini tu??Au wamebadilishiwa kazi wamekuwa watekaji na watekaji wa RAIA wachokonozi??

Kwa sasa Taasisi hii haina moral authority ya kujichunguza sana kuvunjwa tu.
OK lakini kumbuka wakati wa Mwl Nyerere Idara hii ilikuwa inatumia sheria ya Dentetion order Law chini ya Ofisi ya Rais na walikuwa na uwezo wa kukamata muda wowote eneo lolote na kukupeleka wanakokujua wao.

Lakini baada ya kuunda TISS kwa sheria ya mwaka 1996 na Bunge na kuanisha majukumu yao na mpaka yao then kipengele cha kukamata au Ku arrest kinabaki kwa Polisi tu.

Na majukumu ya TISS yameanishwa vizuri tu katika sheria ya TISS ya mwaka 1996.Na kama kuna kuna Viongozi wanawatumia vibaya TISS Basi Viongozi hao ni wa kulaumiwa na kulaniwa kabisa.

TISS ni rafiki wa jamii na hupenda kukaa na jamii ili kupata taarifa sahihi za jamii kuhusu usalama wa Taifa ila hawapendi sana MTU anayevuruga Usalama wa Taifa na ukiingia ktk anga zao utajuta kuzaliwa.....tahadhari tu hiyo.
 
Binafsi napenda kuwapongeza TISS kwa amani tuliyonayo Tanzania ila napendekeza kwamba hii idara adhimu iwe mbali na siasa tutafika tu.
 
Mimi
Umeandika vyema,lakini kwenye taasisi hii kuna Malimbukeni wamefichwa humo ambao ndiyo watekelezaji wa uchafu unaoendelea.

Kuna kesi ya Mwenyekiti wa UVCCM Arusha kutumia kitambulisho cha TISS kupora Mali za watu na kujipatia fedha mpaka Leo hakuna kinachoendelea,hivyo kwa akili za kawaida kabisa zinanifanya niamini kitengo hicho kuna UVCCM kwa jina la Green Guard wapo na inawezekana ndiyo watumishi vibaya wa taasisi hii.

Wazee walisema usipoziba UFA utajenga UKUTA.

Kaka UFA umeshakuwa mkubwa sana hapo hakuna namna ni kujenga UKUTA. Usipoujenga leo au sasa kesho utatubomokea.
=====
Tetty nakubaliana nawe.
Ziko kesi nyingi za namna hiyo kama hiyo ya Arusha. Kama kweli kitambulisho kile kilikuwa feki kama ilivyotangazwa, kwa nini hatusikii kesi tena? Inavyoonekana ni kuwa kuna uzembe ulifanyika wa kufikiri kila mwana UVCCM ni mtu safi na wakaingizwa wengi au wakapewa priviledges za kutumia jina la taasisi ili kuokoa mambo ya kisiasa. Matokeo yake, wanapoharibu, ni taasisi inayolaumiwa na wala si vyama vinavyokuwa vinatafuta kusaidiwa.

Lakini pia liko eneo jingine ambalo limeachwa kushughulikiwa siku hizi na kusababisha uchafu katika taasisi.
Zamani wana taasisi hakuoa/kuolewa ovyo ovyo bila wachumba wao kufanyiwa vetting ya kutosha na kupewa maonyo/ semina. Siku hizi vijana wa taasisi wanaoa wanavyotaka na kuacha wanavyotaka. Kibaya zaidi wanaoa/kuollewa na watu wasio raia wa Tanzania. Wengine wana michepuko "isiyo ya kikazi", wamezaa/ kuzalishwa nayo na unageuka uchochoro wa wana taasisi kujilipua kila mara. Mwana taasisi akikuta mchepuko wake nao umechepuka, hachelewi kijilipua kila mtu amjue alivyo wa taasisi!

Linatakiwa fagio kupita katika eneo hili la ndoa. Wana taasisi wanaofanya kazi mikoa ya mipakani wengi wao wameibuka na mabinti wa Kinyarwanda na hii ni business kubwa ya Rwanda kupenya ngome ya taasisi yetu.
 
Nina siku nyingi sijalogin JF lakini baada ya kusoma bandiko la Baija nimeguswa na nikaona kuna umuhimu wa kuchangia.

Wakuu, niukweli usio pingika tangu 2010 pamekuwepo juhudi za makusudi ku-recruit vijana wa UVCCM kwenye KITENGO. Mkuu wa mkoa wa dar ni miongoni mwa vijana hao.

Kwa Bahati mbaya vijana hawa wameiva vizuri kiitikadi (chama) lakini sio kwenye misingi ya Kitengo. Kwa vijana hawa Usalama wa taifa maana yake ni usalama wa chama. Kwao Usalama wa taifa nicheo cha kutambia.

Vijana hawa hata siri hawana.
 
Back
Top Bottom