Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,727
Siungi mkono TISS kuundiwa tume ya uchunguzi ya wazi.
Chombo hiki ni muhimu si kwa kizazi hiki, chama hiki wala serikali hii, bali ni kwa mustakabali wa taifa lililopo na lijalo. Sikubaliani na wanaokipa chombo hiki "Umungu" kuwa hakikosei, lakini nachelea kusema kuwa kuna mambo hayaendi vizuri na hasa sasa kwa hivi wakati tuna mkulu ambaye ni mgeni sana katika chombo hiki.
Ili kuepuka mambo mengi kusambazwa na kumwaga hadharani na hatimaye kuhatarisha maisha ya wazlendo wengi sana walio katika chombo hiki, nashauri chombo kijichunguze na kionekane kimejichunguza kweli kweli. Yanatakiwa mabadiliko makubwa ya tabia na mafunzo. Kuwadharau wazee na wana taasisi wa zamani hakusaidii kwa sasa. Ebu tazama haya kama mfano:
- Ilikuwa marufuku kwa mwana taasisi hii, kukamata (arrest) au hata kuhoji (interogate) hadharani. Daima amri ya kukamata ilipelekwa polisi na Afisa wa juu kwa Afisa wa juu wa polisi. Mtuhumiwa alikamatwa na polisi na kuweka ndani kwa "kunyimwa dhamana". Wana taasisi walimchukua baadaye kwa muda wao na kumhoji ili kupata walichokihitaji, kisha walimrudisha polisi. Ilipobidi polisi walifungua mashtaka feki na kesi kufukuzwa baadaye. Hii ilisaidia mtuhumiwa kufikiri waliomhoji ni polisi wakati hata wana taasisi wamehusika. Ni nani aliruhusu kukamatwa (sasa kunaitwa kutekwa) kwa Roma Mkatoliki na kusababisha uzembe mbaya namna hii.
- Ilikuwa marufuku kwa mwana taasisi kuonyesha kitambulisho chake kwa matukio madogo madogo. Siku hizi eti mwana taasisi anasimamishwa barabarani na Trafiki na hapo hapo anatoa kitambulisho kumtisha trafiki huyo! Mwana taasisi wa kweli alikuwa anaweza hata kukamatwa anakunywa gongo, kuwekwa pingu, na kulala ndani kwa siku mbili bila mdhamana. Mwana taasisi alikwa anaweza kukamatwa na maafisa wengine wa serikali katika mkoa mwingine wasiomfahamu na asijitambulishe. Siku hizi, vitambulisho vya taasisi vinatumika hata uwanja wa taifa kuingilia kutazama mechi.
-Ilikuwa marufuku kwa mwana taasisi kuonyesha silaha hadharani. Jamani hata walinzi wa viongozi bado wanaficha silaha sembuse mtu aliyekwenda kuvinjali na kutathmini hali ya kusanyiko la kawaida. Hulka hii inahatarisha maisha ya wengine na kujenga chuki ya jamii dhidi ya taasisi. Lilipotokea kosa na namna hii, uchunguzi ulienda mbali kuanzia alivypatikana, alivyofundishwa na nani alimpa kazi (assignemnt) iliyosababisha afanye kosa la kujilipua. Kwa wachunguzi makini, lazima wangegundua kasoro katika maeneo hayo matatu.
- Pamoja na kwamba ni wana taasisi ni maaskari, lakini ni kosa kwa mwana taasisi kupokea na kutekeleza amri ya "kijinga". Mwana taasisi daima hushikilia mikononi mwake uhai wa aina tatu: uhai wake, wa wana taasisi wenzake na wa nchi. Amri inayohatarisha mojawapo ya hayo, hukubaliwa kwa maandishi si kwa maneno wala simu.
Hapa tulipofikishwa, kimya cha taasisi hakisaidii. Kina Lizaboni na kazi za kujituma kwenye mitandao hakusaidii. Utii kwa mamlaka za juu bila kujali uendelevu wa taasisi baadaye, hausaidii. Kuivunja bila kufikiri hakusaidii. Mwalimu aliivunja mwaka 1964 na kuiunda upya lakini kulikuwa na sababu kubwa. Uhuru wa taasisi hii ni muhimu pengine kuliko chombo kingine chochote isipokuwa mahakama. Mwalimu aliwahi kufanya uamuzi mgumu binafsi ili kulinda uhuru wa chombo hiki kikiwa bado kichanga. Mandela alikubali kufanya uamuzi mgumu binafsi wa kutengana na mkewe Winnie pale alipobaini kuwa alikuwa anakiingilia chombo hiki. Ili kuficha ukweli huu, alitumia sababu nyingine zinazotamkika ili kupunguza maswali katika jamii. Mkuu asiyeheshimu uhuru wa chombo hiki ni hatari kwa mshikamano wa nchi (sitaki kusema usalama wa nchi).
Mwana taasisi aliyeingia kwa kupindisha baadhi ya vipengere aondolewe hata kama nashikilia funguo za "chungu" au "ashugulikiwe" kipekee.
No person is greater than a nation
---/Baija