Tetesi: Tishio la kumuondoa Mufti BAKWATA

Hali si shwari ndani ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) na sasa kundi la viongozi ndani ya baraza hilo wanakula njama za kumuondoa kiongozi wao makini Mufti Zubeir.

Hali hiyo inakuja huku Zaidi ya miezi miwili Bakwata haina ofisi na Zaidi ya wafanyakazi 50 wa Bakwata Makao Makuu hawajalipwa mishahara yao kwa Zaidi miezi kumi na moja(11).

Kadhaloka zaidi ya walimu kumi na tano wa shule ya Bondeni Arusha hajalipwa mishahara yao ,na huku Baraza lote la Masheikh la mkoa wa Katavi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bakwata Mkoa wa Katavi kujiuzulu kutokana na kutokuwa na IMANI na mufti zuberi.

Tayari zipo taarifa sasa za kuandaliwa mpango wa kuondolewa madarakani mufti kutokana kile kinachodaiwa kwamba ni kushindwa kuongoza Bakwata na ubadhilifu mkubwa wa mali za Bakwata uliofanywa na mufti na ndugu zake wa karibu.

Wajumbe kadhaa wa Baraza la masheikh Taifa wanajiandaa kutumia katiba ya Bakwata kumuengua mufti katika nafasi yake ya umufti kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Wakati wajumbe wengine kumi wa halmashauri kuu ya Bakwata Taifa wakijiandaa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na Imani na mufti katika kikao kijacho ili kutoa nafasi ya mufti kujiuzulu kabla hawajatoa taarifa za siri za ubadhilifu mkuu wanaoujua wajumbe hao dhidi ya mufti.

Wakati huo huo viongozi wa Bakwata toka mikoa mitano,wanajiandalia kujiuzulu kutokana na kuchoshwa kwao na vitendo vya mufti Zuberi. Vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na mufti zuberi kuingoza bakwata kwa miaka miwili sasa bila muelekeo wowote,huku vitendo vya ubadhilifu,ubinafsishaji wa mali za bakwata na ubabaishaji kushika kasi na ndugu wa mufti kupewa kipaumbele bila kuzingatia katiba ya Bakwata.
Shida iko wapi? Wauwache Uislamu waendelee na mambo yao!
 
kundi la viongozi ndani ya baraza hilo wanakula njama za kumuondoa kiongozi wao makini Mufti Zubeir.

Kwa nini unasema "wanakula njama"?

Kwani dhambi kutaka kumng'oa mtu??????????? Lazima iwe negative conspiracy? Yale yale ya Zitto, Kitila, Mbowe na Chadema

Waafrika tatizo hatuwezi kukubali kuwa it's okay kumchoka kiongozi na kufanya mipango ya wazi ya kumwondoa, lazima iwe ni njama! Amezaliwa awe Mufti mpaka afe?

Katiba ya BAKWATA haina "expansion joints" za kuruhusu sauti za wadau kudai mabadiliko ya madaraka bila kuleta mpasuko na bila "kula njama"?
 
Mufti wa mwisho alikuwa ni marehemu Hemed bin Jumaa bin Hemed. Hawa wengine wote waliofuata hakuna hata mmoja aliyewahi kuenea kwenye kile kiti.

Akaja Marehemu Simba ndiyo kabisaa, akaboronga boronga kabla ya kwenda zake. Zaidi akaishia kufumaniwa na wake zake huko hijjah akizini na hawara walipokwenda kuhiji mecca
Nilikuwa napenda sana kusikiliza hotuba na mawaidha yake. Alikuwa na busara na hekma sana yule Mzee.
 
Muogope mungu sana,
Unamsingizia maiti huogopi wewe,

Kosa kumsingizia alokuwa hai, jee huyu alokuwa maiti jee?
Vipi utamuomba msamahan wakati hayupo tena, usiwe unafanya mambo kwa kufurahisha nafsi au kwa ajili ya chuki ni hatari zaidi.

Na hatari zaidi ya kuwa ulipomsingizia ni pahali patakatifu ambapo waislam wote wanakutana kutimiza nguzo ya tano pamoja na kumuomba allaah awasamehe madhambi yao.

Leo unakuja kusema ya kuwa mufti kazini! Hata angekuwa si mufti, mtu yoyote yule hauwezi kumsemea kosa hilo.

Jee wajua ya kuwa katika uislam kumsingizia mtu zinaa, adhabu yake ni kupigwa fimbo thamanini?

Laiti hukumu ya allaah ingekuwa inatumika basi wewe sasa hivi ni kuhukumiwa fimbo hizo, na bora zaidi kupata hiyo hukumu kuliko adhabu ambayo allaah atakutia katika maisha yako yote ya hapa duniani na kaburini na mpaka kukufuliwa.

Kwa hili huna msamaha mpaka umuombe mwenyewe samahani, sasa sijui umejitayarisha vipi kusimama mbele ya allaah na kumpa hoja ya kuwa kwa nini ulisema hivi, na pia sijui ulomsingizia hata hiyo siku ya siku atakuwa mwenye kukusamehe.

Note:
Mufti simba simjui namsikia tuu, ila nimesema haya kwa yoyote yule anaemsingizia mtu uongo, uwe wowote ule, ajitayarishe makaazi yake motoni

Acha ujinga wako wewe. Usifikiri unaongea na watoto wenzako hapa, ebwoo!!
 
uongozi sio elimu tu bali busara, maarifa, hekma na uadalifu, mbona tunaongozwa na madokta lakini utadhani mangumbalu? jitathimini
Uongozi Ni taaluma kwanza alafu ndo ifuate busara.kama taaluma ya uongozi huna au huijui tegemea kufanya vituko na uharibifu
 
uongozi sio elimu tu bali busara, maarifa, hekma na uadalifu, mbona tunaongozwa na madokta lakini utadhani mangumbalu? jitathimini
Ni kweli ila sasa hayo maelezo mbona hayajanijibu kuhusu Ilmu zao?
 
Mimi napita tu! Ila wewe una uhakika gani kama kilichosemwa ni uongo ama ukweli? Na wewe unaelekea katika mkumbo wa kusingizia kama si kusema uongo.
Mkuu umeghafilika,uislamu unatukataza kusema mabaya ya marehemu hata Kama ni ya kweli.fanya toba mkuu na Allah Ni mwingi wa msamaha
MUOGOPE MUNGU SANA,
UNAMSINGIZIA MAITI HUOGOPI WEWE,
KOSA KUMSINGIZIA ALOKUWA HAI, JEE HUYU ALOKUWA MAITI JEE?
VIPI UTAMUOMBA MSAMAHAN WAKATI HAYUPO TENA, USIWE UNAFANYA MAMBO KWA KUFURAHISHA NAFSI AU KWA AJILI YA CHUKI NI HATARI ZAIDI.
NA HATARI ZAIDI YA KUWA ULIPOMSINGIZIA NI PAHALI PATAKATIFU AMBAPO WAISLAM WOTE WANAKUTANA KUTIMIZA NGUZO YA TANO PAMOJA NA KUMUOMBA ALLAAH AWASAMEHE MADHAMBI YAO.
LEO UNAKUJA KUSEMA YA KUWA MUFTI KAZINI! HATA ANGEKUWA SI MUFTI, MTU YOYOTE YULE HAUWEZI KUMSEMEA KOSA HILO.
JEE WAJUA YA KUWA KATIKA UISLAM KUMSINGIZIA MTU ZINAA, ADHABU YAKE NI KUPIGWA FIMBO THAMANINI?
LAITI HUKUMU YA ALLAAH INGEKUWA INATUMIKA BASI WEWE SASA HIVI NI KUHUKUMIWA FIMBO HIZO, NA BORA ZAIDI KUPATA HIYO HUKUMU KULIKO ADHABU AMBAYO ALLAAH ATAKUTIA KATIKA MAISHA YAKO YOTE YA HAPA DUNIANI NA KABURINI NA MPAKA KUKUFULIWA.
KWA HILI HUNA MSAMAHA MPAKA UMUOMBE MWENYEWE SAMAHANI, SASA SIJUI UMEJITAYARISHA VIPI KUSIMAMA MBELE YA ALLAAH NA KUMPA HOJA YA KUWA KWA NINI ULISEMA HIVI, NA PIA SIJUI ULOMSINGIZIA HATA HIYO SIKU YA SIKU ATAKUWA MWENYE KUKUSAMEHE.
NOTE:
MUFTI SIMBA SIMJUI NAMSIKIA TUU, ILA NIMESEMA HAYA KWA YOYOTE YULE ANAEMSINGIZIA MTU UONGO, UWE WOWOTE ULE, AJITAYARISHE MAKAAZI YAKE MOTONI
 
Mkuu umeghafilika,uislamu unatukataza kusema mabaya ya marehemu hata Kama ni ya kweli.fanya toba mkuu na Allah Ni mwingi wa msamaha
Yes Uislam unakataza kusema mabaya ya Marehemu, je huyo aliyesema hayo ni Muislam? Lakini hata usipoyasema mabaya yake haiwezi kufuta ukweli kama marehemu alikuwa na mabaya yake au mazuri yake.
 
Uzuri na ubaya wa Uislam ndio huo? Hakuna ukiritimba na hakuna aliyembora zaidi ya mwenzie. Wangemchapa bakora kabla ya kuendelea na mengine.
 
Back
Top Bottom