Tetesi: Tishio la kumuondoa Mufti BAKWATA

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
571
225
Hali si shwari ndani ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) na sasa kundi la viongozi ndani ya baraza hilo wanakula njama za kumuondoa kiongozi wao makini Mufti Zubeir.

Hali hiyo inakuja huku zaidi ya miezi miwili Bakwata haina ofisi na zaidi ya wafanyakazi 50 wa Bakwata Makao Makuu hawajalipwa mishahara yao kwa zaidi miezi kumi na moja(11).

Kadhalika zaidi ya walimu kumi na tano wa shule ya Bondeni Arusha hajalipwa mishahara yao, na huku Baraza lote la Masheikh la mkoa wa Katavi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bakwata Mkoa wa Katavi kujiuzulu kutokana na kutokuwa na IMANI na mufti zuberi.

Tayari zipo taarifa sasa za kuandaliwa mpango wa kuondolewa madarakani mufti kutokana kile kinachodaiwa kwamba ni kushindwa kuongoza Bakwata na ubadhirifu mkubwa wa mali za Bakwata uliofanywa na mufti na ndugu zake wa karibu.

Wajumbe kadhaa wa Baraza la masheikh Taifa wanajiandaa kutumia katiba ya Bakwata kumuengua mufti katika nafasi yake ya umufti kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Wakati wajumbe wengine kumi wa halmashauri kuu ya Bakwata Taifa wakijiandaa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na Imani na mufti katika kikao kijacho ili kutoa nafasi ya mufti kujiuzulu kabla hawajatoa taarifa za siri za ubadhilifu mkuu wanaoujua wajumbe hao dhidi ya mufti.

Wakati huo huo viongozi wa Bakwata toka mikoa mitano, wanajiandalia kujiuzulu kutokana na kuchoshwa kwao na vitendo vya mufti Zuberi. Vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na mufti Zuberi kuingiza Bakwata kwa miaka miwili sasa bila muelekeo wowote, huku vitendo vya ubadhirifu, ubinafsishaji wa mali za bakwata na ubabaishaji kushika kasi na ndugu wa mufti kupewa kipaumbele bila kuzingatia katiba ya Bakwata.

Updates:

Masheikh watatu ambao ni wajumbe wa baraza la ulamaa taifa Bakwata,wakishirikiana na sheikh mkuu wa dar es salaam,sheikh mkuu wa tabora,pamoja na kiongozi mwandamizi wa zamani wa Bakwata ndio wanasuka mpango wa kumuondoa mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi.

Mpango huo ulioandali kwa umakini mkubwa,huenda ukamfanya mufti Zuberi kuwa ni mufti wa kwanza kuenguliwa katika historia ya bakwata na kupelekea mufti kwa mara ya kwanza kutoka Rufiji.

Mpango ambao ulikuwa utekelezwe wakati Mufti Zuberi akiwa yupo Morocco,ambao kwa sasa utatekelezwa wakati wowote.

Nitaendelea kuwapa update!!!
 
The Bourne

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
1,077
2,000
Uchaguzi ungekua unasimamia misingi ya dini Zuberi asingepenya, sisi pia madokta na ma prof. wapo wenye elimu zote lakini sababu ni tawi la chama viongozi watakua wakina Alhad, mwenzako anaokota uchafu na kuweka kwenye pipa wewe unaselfika,
Kwa wenzetu utasikia dokta nani , dokta nani ndio viongozi
 
Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,543
2,000
Mufti wa mwisho alikuwa ni marehemu Hemed bin Jumaa bin Hemed. Hawa wengine wote waliofuata hakuna hata mmoja aliyewahi kuenea kwenye kile kiti.

Akaja Marehemu Simba ndiyo kabisaa, akaboronga boronga kabla ya kwenda zake. Zaidi akaishia kufumaniwa na wake zake huko hijjah akizini na hawara walipokwenda kuhiji mecca
 
Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
3,483
2,000
Mufti wawisho alikua ni marehemu Hemed bin Jumaa bin Hemed. Hawa wengine wote waliofuata hakuna hata mmoja aliyewahi kuenea kwenye kile kiti. Akaja Marehemu Simba ndiyo kabisaa, akaboronga boronga kabla ya kwenda zake. Zaidi akaishia kufumaniwa na wake zake huko hijjah akizini na hawara walipokwenda kuhiji mecca

duuu
 
kwabwina

Senior Member
May 29, 2016
128
250
Mufti wa mwisho alikuwa ni marehemu Hemed bin Jumaa bin Hemed. Hawa wengine wote waliofuata hakuna hata mmoja aliyewahi kuenea kwenye kile kiti.

Akaja Marehemu Simba ndiyo kabisaa, akaboronga boronga kabla ya kwenda zake. Zaidi akaishia kufumaniwa na wake zake huko hijjah akizini na hawara walipokwenda kuhiji mecca
Dah Hatar mkuu kiongoz wa dini kuwa na makandokando Kama hayo
 
SeliSelina

JF-Expert Member
Jun 27, 2014
223
500
Muogope mungu sana,
Unamsingizia maiti huogopi wewe,
Kosa kumsingizia alokuwa hai, jee huyu alokuwa maiti jee?

Vipi utamuomba msamahan wakati hayupo tena, usiwe unafanya mambo kwa kufurahisha nafsi au kwa ajili ya chuki ni hatari zaidi.

Na hatari zaidi ya kuwa ulipomsingizia ni pahali patakatifu ambapo waislam wote wanakutana kutimiza nguzo ya tano pamoja na kumuomba allaah awasamehe madhambi yao.

Leo unakuja kusema ya kuwa mufti kazini! Hata angekuwa si mufti, mtu yoyote yule hauwezi kumsemea kosa hilo.

Jee wajua ya kuwa katika uislam kumsingizia mtu zinaa, adhabu yake ni kupigwa fimbo thamanini?

Laiti hukumu ya allaah ingekuwa inatumika basi wewe sasa hivi ni kuhukumiwa fimbo hizo, na bora zaidi kupata hiyo hukumu kuliko adhabu ambayo allaah atakutia katika maisha yako yote ya hapa duniani na kaburini na mpaka kukufuliwa.

Kwa hili huna msamaha mpaka umuombe mwenyewe samahani, sasa sijui umejitayarisha vipi kusimama mbele ya allaah na kumpa hoja ya kuwa kwa nini ulisema hivi, na pia sijui ulomsingizia hata hiyo siku ya siku atakuwa mwenye kukusamehe.

Note:
Mufti simba simjui namsikia tuu, ila nimesema haya kwa yoyote yule anaemsingizia mtu uongo, uwe wowote ule, ajitayarishe makaazi yake motoni

Mufti wa mwisho alikuwa ni marehemu Hemed bin Jumaa bin Hemed. Hawa wengine wote waliofuata hakuna hata mmoja aliyewahi kuenea kwenye kile kiti.

Akaja Marehemu Simba ndiyo kabisaa, akaboronga boronga kabla ya kwenda zake. Zaidi akaishia kufumaniwa na wake zake huko hijjah akizini na hawara walipokwenda kuhiji mecca
 
bdo

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,772
2,000
MUOGOPE MUNGU SANA,
UNAMSINGIZIA MAITI HUOGOPI WEWE,
KOSA KUMSINGIZIA ALOKUWA HAI, JEE HUYU ALOKUWA MAITI JEE?
VIPI UTAMUOMBA MSAMAHAN WAKATI HAYUPO TENA, USIWE UNAFANYA MAMBO KWA KUFURAHISHA NAFSI AU KWA AJILI YA CHUKI NI HATARI ZAIDI.
NA HATARI ZAIDI YA KUWA ULIPOMSINGIZIA NI PAHALI PATAKATIFU AMBAPO WAISLAM WOTE WANAKUTANA KUTIMIZA NGUZO YA TANO PAMOJA NA KUMUOMBA ALLAAH AWASAMEHE MADHAMBI YAO.
LEO UNAKUJA KUSEMA YA KUWA MUFTI KAZINI! HATA ANGEKUWA SI MUFTI, MTU YOYOTE YULE HAUWEZI KUMSEMEA KOSA HILO.
JEE WAJUA YA KUWA KATIKA UISLAM KUMSINGIZIA MTU ZINAA, ADHABU YAKE NI KUPIGWA FIMBO THAMANINI?
LAITI HUKUMU YA ALLAAH INGEKUWA INATUMIKA BASI WEWE SASA HIVI NI KUHUKUMIWA FIMBO HIZO, NA BORA ZAIDI KUPATA HIYO HUKUMU KULIKO ADHABU AMBAYO ALLAAH ATAKUTIA KATIKA MAISHA YAKO YOTE YA HAPA DUNIANI NA KABURINI NA MPAKA KUKUFULIWA.
KWA HILI HUNA MSAMAHA MPAKA UMUOMBE MWENYEWE SAMAHANI, SASA SIJUI UMEJITAYARISHA VIPI KUSIMAMA MBELE YA ALLAAH NA KUMPA HOJA YA KUWA KWA NINI ULISEMA HIVI, NA PIA SIJUI ULOMSINGIZIA HATA HIYO SIKU YA SIKU ATAKUWA MWENYE KUKUSAMEHE.
NOTE:
MUFTI SIMBA SIMJUI NAMSIKIA TUU, ILA NIMESEMA HAYA KWA YOYOTE YULE ANAEMSINGIZIA MTU UONGO, UWE WOWOTE ULE, AJITAYARISHE MAKAAZI YAKE MOTONI
Mimi napita tu! Ila wewe una uhakika gani kama kilichosemwa ni uongo ama ukweli? Na wewe unaelekea katika mkumbo wa kusingizia kama si kusema uongo.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
MUOGOPE MUNGU SANA,
UNAMSINGIZIA MAITI HUOGOPI WEWE,
KOSA KUMSINGIZIA ALOKUWA HAI, JEE HUYU ALOKUWA MAITI JEE?
VIPI UTAMUOMBA MSAMAHAN WAKATI HAYUPO TENA, USIWE UNAFANYA MAMBO KWA KUFURAHISHA NAFSI AU KWA AJILI YA CHUKI NI HATARI ZAIDI.
NA HATARI ZAIDI YA KUWA ULIPOMSINGIZIA NI PAHALI PATAKATIFU AMBAPO WAISLAM WOTE WANAKUTANA KUTIMIZA NGUZO YA TANO PAMOJA NA KUMUOMBA ALLAAH AWASAMEHE MADHAMBI YAO.
LEO UNAKUJA KUSEMA YA KUWA MUFTI KAZINI! HATA ANGEKUWA SI MUFTI, MTU YOYOTE YULE HAUWEZI KUMSEMEA KOSA HILO.
JEE WAJUA YA KUWA KATIKA UISLAM KUMSINGIZIA MTU ZINAA, ADHABU YAKE NI KUPIGWA FIMBO THAMANINI?
LAITI HUKUMU YA ALLAAH INGEKUWA INATUMIKA BASI WEWE SASA HIVI NI KUHUKUMIWA FIMBO HIZO, NA BORA ZAIDI KUPATA HIYO HUKUMU KULIKO ADHABU AMBAYO ALLAAH ATAKUTIA KATIKA MAISHA YAKO YOTE YA HAPA DUNIANI NA KABURINI NA MPAKA KUKUFULIWA.
KWA HILI HUNA MSAMAHA MPAKA UMUOMBE MWENYEWE SAMAHANI, SASA SIJUI UMEJITAYARISHA VIPI KUSIMAMA MBELE YA ALLAAH NA KUMPA HOJA YA KUWA KWA NINI ULISEMA HIVI, NA PIA SIJUI ULOMSINGIZIA HATA HIYO SIKU YA SIKU ATAKUWA MWENYE KUKUSAMEHE.
NOTE:
MUFTI SIMBA SIMJUI NAMSIKIA TUU, ILA NIMESEMA HAYA KWA YOYOTE YULE ANAEMSINGIZIA MTU UONGO, UWE WOWOTE ULE, AJITAYARISHE MAKAAZI YAKE MOTONI
Herufi ndogo zingefikisha ujumbe ulioukusudia bila kukalfisha nafsi za watu kwa miherufi mikubwa.

Naona kama uswaiba wa mkuu wa mkoa na sheikh wa mkoa unataka kufanya mambo yasiyotarajiwa yakawa bayana.
"wakimalizana na upinzani wanahamia kwenu" Tundu Lissu.
 
Sueky

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
320
250
Mufti wa mwisho alikuwa ni marehemu Hemed bin Jumaa bin Hemed. Hawa wengine wote waliofuata hakuna hata mmoja aliyewahi kuenea kwenye kile kiti.

Akaja Marehemu Simba ndiyo kabisaa, akaboronga boronga kabla ya kwenda zake. Zaidi akaishia kufumaniwa na wake zake huko hijjah akizini na hawara walipokwenda kuhiji mecca
mmmh Kwanini akusomewa Albadli huko uko???
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom