Tishio la Al-shabab kwa wakazi wa Kigamboni

Mughwira

Senior Member
Jun 10, 2008
109
34
Kama kweli taarifa za waziri wa mambo ya ndani ya nchi na za kamanda Kova hazikuwa za kuchakachua, zilizotiwa mafuta ya kisiasa ili kuhalalisha vyama vya siasa na wanaharakati wengine kutoandamana. Mimi naona kuna hatari zaidi kwa wakazi wa Kigamboni kuliko hata wale wapenzi wa maandamano au waandamanaji. Je polisi, usalama wa taifa nk wanachukulia kwa uzito upi msongamano wa wananchi kwenye vyumba vya kusubiria Panton upande wa Magogoni na Kigamboni? Kama kweli Al-Shabab wanapenda mikusanyiko kutekeleza azima yao?
Nawasilisha
 

Attachments

  • mv+magogoni+kivukoni[1].JPG
    mv+magogoni+kivukoni[1].JPG
    44.1 KB · Views: 92
Hao Al shabab hawawezi kusogea karibu na kivuko cha kigamboni hata siku moja, wanaogopa kuzama.
 
Back
Top Bottom