TIMUA TIMUA CHADEMA: Diwani CHADEMA asimamishwa miezi mitatu

TIMUA TIMUA CHADEMA: Diwani CHADEMA asimamishwa miezi mitatu

Moods, huyu muleta mada anapotosha jukwaa kwani anasema kuwa ni Timua Timua ya Chadema , huyu kaongea na Halimashauri yake kisa kuwaambia wananchi kuhusu makusanyo ya kodi ambayo yamekuwa yakifanywa na Halimashauri .

Mkuu hebu soma kiswahili ulichotumia.
 
makada wa chama hiki wengi ni wachumia tumbo, walikuwa wanatafuta kichaka cha kuficha njaa zao
:noidea:
Na sasa inakula kwao, wafujaji hawavumiliwi ni fukuza kwa kwenda mbele.

CHADEMA NI VEMA.
 
Ametimuliwa wapi sasa
kama ana utovu wa nidhamu na kukiuka taratibu za uendeshaji wa halmashauri ulitaka watu wamvumilie kwa kuwa ni Diwani
Hata wewe ukikiuka kwa makusudi taratibu za ofisi yako na kuwa na utovu wa nidhamu sidhani kama mwajiri wako atakuvumilia
na hii amesimamishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri na jua kwamba halmashauri ina kanunina haiendeshi tuu kama familia kuvumiliana
Ukikiuka taratibu unatimuliwa kwenye kikao au kusimamishwa

Haya unayoyasema hapa ni Lugha ya Kigeni kwa ccm, serikali za ccm, na idara zao zote.
 
Haya unayoyasema hapa ni Lugha ya Kigeni kwa ccm, serikali za ccm, na idara zao zote.

Mkuuu Sangarara kwao ni watakatifu sana na hawafanyi lolote
maana inaonekana diwani akihoji ulaji wa pesa za Halmashauri anasimamishwa kwa utovu wa nidhamu au akihoji utekelezaji wa miradi ya maendeleo wanamsimamisha
Ila hao wako hapa kusifia ujinga na kuona kuwa kilichofanyika ni halali kabisa
 
Last edited by a moderator:
Kati ya Lema na Zitto nani anatafuta umaarufu??

quote-many-have-been-the-wise-speeches-of-fools-though-not-so-many-as-the-foolish-speeches-of-wise-men-thomas-fuller-342993.jpg
 
Salaam wana Jukwaa.
Tunduma:
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma,
imemsimamisha Diwani wa Tunduma kupitia Chadema, Frank Mwakajoka kuhudhuria vikao kwa miezi mitatu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji huo, Elias Cheyo alithibitisha kufikiwa na uamuzi huo, na kwamba
hatahudhuria vikao vya Kamati ya Fedha vinavyofanyika kila mwezi mpaka Februari 2014


Cheyo alisema kuwa diwani huyo ambaye ni Mjumbe Kamati ya Fedha na Uongozi amekuwa na tabia ya utovu wa nidhamu kwa kukiuka makusudi za taratibu za uendeshaji wa halmashauri hiyo.

SOURCE: Mwananchi.

NKUU SINDE, Nduguyenu.

Mkuu umeshirikisha ubongo kweli? Timua timua chadema ina maana gani kama waliomsimamisha ni halmashauri ya mji?
 
Hili jukwaa limeanza kuboa, waleta madawa style hii wanafanya kwa bahati mbaya, uelewa mdogo au ni
kudharau jukwaa?
 
fukuza uozo huko, wanaolindana tutawaona tu! china ukifanya upuuzi wanakupiga shaba!
 
Inawezekana Prof. Muhongo alikuwa right kuwa watanzania ni wavivu wa kufikiri. Sasa tofauti ya kutimuliwa na kusimamishwa ni nini? Ni mamlaka gani imetumika kufikia huo uamuzi?? I feel sorry for JF's server(s).
 
Heading na content havina uhusiano. Yamkini ulikuwa na hoja ya msingi uliyotaka kusema, lakini umeshindwa kufanya hivyo.

Salaam wana Jukwaa.
Tunduma:
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma,
imemsimamisha Diwani wa Tunduma kupitia Chadema, Frank Mwakajoka kuhudhuria vikao kwa miezi mitatu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji huo, Elias Cheyo alithibitisha kufikiwa na uamuzi huo, na kwamba
hatahudhuria vikao vya Kamati ya Fedha vinavyofanyika kila mwezi mpaka Februari 2014


Cheyo alisema kuwa diwani huyo ambaye ni Mjumbe Kamati ya Fedha na Uongozi amekuwa na tabia ya utovu wa nidhamu kwa kukiuka makusudi za taratibu za uendeshaji wa halmashauri hiyo.

SOURCE: Mwananchi.

NKUU SINDE, Nduguyenu.
 
Mkuu umeshirikisha ubongo kweli? Timua timua chadema ina maana gani kama waliomsimamisha ni halmashauri ya mji?

Mkuu Mungi, hizi tetesi ninazomwagika huku mtaani mithili ya njugu, Kuwa Mmemsimamisha kazi Naibu katibu mkuu wa chama chenu ni za kweli?
 
Last edited by a moderator:
ushabiki acha.... heading ujumbe Huu.... content tofauti........, shame on you.
 
Katika uzi huu mimi ugomvi wangu no mods -- sijui wamekuwa vipi? Ukisoma habari yenyewe ni dhahiri kichwa cha habari kinapotosha kabisa, kama vile Chadema ndiyo wamemtimua diwani huyo. Mods walitakiwa kukirekebisha kichwa cha habari, kama vile wanavyofanya katika thread zingine.

Kwa kuachia kichwa hiki cha habari, Mods wanaendekeza ushabiki humu JF, hasa siku hizi.
 
Kubadeki! Hapo mtatiana shombo mpaka basi. Chadema heads for collapse

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom