Timu yangu Simba na mashabiki wote

Mpira huchezwa hadharani. Kwa kweli leo UTO wamelimwaga biriani ambalo msimu uliopita tulikuwa tunalipiga na kwa sasa hatuwezi tena, ni ukweli ambao baadhi ya wana Simba hawapendi kuusikia, ni kwa sababu tuliuza hazina zetu mbili na kufifiza ile ndoto ya kwenda mpaka fainali ya CAF.
Ukisikiliza wachambuzi wengi huongelea jinsi kiwango chetu kilivyoshuka ukilinganisha na msimu uliopita. Cha kushangangaza kinachoongelewa ni pengo lao na simsikii mwana Simba yoyote akijigamba kwa bulungutu tulilolipata kwa kuwauza wale mabwana hodari kabisa na roho timu. Naona tutawaongelea kwa muda mrefu sana.
Kimpira, UTO wame-improve sana na upo uwezekano wakainua makwapa mwaka huu kama nasi uchezaji wetu ukiendelea kama ulivyo sasa hivi. Mimi ni mwanamichezo na nimeisha jipanga kisaikojia kwa matokeo yoyote. Nililipenda goli lao la pili na kunikumbusha kuwa hayo ndio yalikuwa magoli yetu yaliyokuwa yakitupa furaha misimu kadhaa iliyooita.
Kupanga ni kuchagua. Kuna mtu ataambulia bulungutu. Mwingine basi jipya na labda mwingine atainua kwapa baada miaka minne,
Who knows, time will tell.
 
Acha wanasimba watapike nyongo ni ujinga una striker bocco age 36 kagere 35 wawa beki35 then wanaanza first eleven unaona kabasa wanavo hangaika akili zinataka miili inakataa kwa nini wana simba wasitapike nyongo ? Nahao nimetolea mfano wapo wachezaji wengi ambao wako hoi Bini taabani.Na huo ndio udhaifu wa Management nzima ya Simba haikujipanga vyema wacha wana simba waseme ya moyoni
 
Simba tumesajili vibaya- wachezaji wote wapya- viwango vyao sio vizuri- na wale wa zamani wamechokai- Simba bado inahitaji- kiungo mkabaji- kiungo mshambuliaji- na mshambuliaji- bila kufanya hivyo- Mwaka huu tuta feli kabisa
 
Mimi natamani watu wa uto na wale Simba mguu nje ndani waendelee kuwavimbisha uto kuwa wanabeba ubingwa na kuwapa kila sifa ,hii Ina faida Sana kwa Simba.
Simba Mara nyingi anaanza kinyonge sana full presha Ila gari likiwaka linawaka kweli kweli wakat upande wa pili wakiendelea kujiaminisha watakuja pigwa na mbeya city pale sokoine au kule sumbawaga kwa wajera jera ndipo sasa presha itakuwa sehemu yao na msimu kuyoyoma hatmae muda wa kupewa lawama karia na marefa utawadia katika sehemu yake.

Unbeaten haijaanza huu msimu nadhan Ni neno lililozoeleka kwa Wana uto hasa mzunguko wa kwanza ,so sishangai kwa hizi kelele na Tambo za kila namna .

Mahesab mwisho wa msimu ,alafu nilitamani Simba hata huko shirikisho atoke mapema tu ili wajipange upya kupitia ligi kuu ,kusiwe na viporo vya mechi wanavyolalamikia kila kukicha Hawa uto .
 
Simba tumesajili vibaya- wachezaji wote wapya- viwango vyao sio vizuri- na wale wa zamani wamechokai- Simba bado inahitaji- kiungo mkabaji- kiungo mshambuliaji- na mshambuliaji- bila kufanya hivyo- Mwaka huu tuta feli kabisa
Nakubalina na wewe hapo kwa mshambuliaj pekee Ila sehem zingine pako poa tu sio kinyonge ni swala la muda tu.
Beki anzisha onyango na innonga au Kennedy na innonga Mambo ni bambam,

Pemben anzisha zimbwe ,kule weka mwenda ,kapombe awe anatokea sub , katikat Ni utitir wa viungo ni kocha tu anaamua aanze na kina Nan ,mrishaji kwa maana no kumi bwalya anatosha Sana Tena Sana , tatizo lipo pale mbele ,Mugalu ni mtu Ila Hana shabaha ,kibu ni mtu Ila Ana wenge Sana ,kagere na bocco wangepisha tu dirisha dogo
 
Simba bado ndio timu bora Tanzania.

Usitishwe na Utopolo wanakutana na timu mbovu. Ukitoa Simba timu bora Tanzania kwa sasa ni Polisi Tz, Biashara na Dodoma jiji.

Subiri uwaone wagosi wa kaya pira tutakalowachezea.
Ina ubora upi tena?
 
Nimekubali kwa gemu ya jana na azam.. utoh wameimarika mno. Ila kombe haliendi kwao.. litabaki unyamani
 
Mwamedi yupo pale kimaslahi aliona fursa saivi anawapiga hela
 
Bata fc acha tuendelee kujifariji
 
Baiskeli ya miti tu hiyo kwenye mipando itafahamika tu
#Nguvumoja
 
Muandiko wa kiume sana huu
 
Simba bado ndio timu bora Tanzania.

Usitishwe na Utopolo wanakutana na timu mbovu. Ukitoa Simba timu bora Tanzania kwa sasa ni Polisi Tz, Biashara na Dodoma jiji.

Subiri uwaone wagosi wa kaya pira tutakalowachezea.
Vp? Pira mlilowachezea
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…