Naomba kupata msaada wa ufafanuzi
- Tunachokijua
- Taarifa inayodai kuwa Kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Pape Thiaw amepeleka kombe la AFCON kwenye kambi ya Jeshi kwa ajili ya ulinzi, kama hatua inayoonekana msimamo wa Senegal kutoliachia taji hilo kwa Morocco, na kwamba kwasasa kombe hilo linalindwa na Vikosi vya Jeshi saa 24 ili Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF) isiweze kulipata si za Kweli.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo za Kidigitali umethibitisha kuwa Video hii si ya sasa, haihusiani na hukumu ya Kamati ya Rufaa ya CAF na imekuwepo Mtandaoni tangu Februari 8, 2026 wakati timu hiyo ilipokwenda kwenye mojawapo ya Kambi za jeshi kufurahia ushindi wao.
Video halisi ya tukio hili ya Feberuari 8, 2026 ipo hapa.