"Timorous" Judges vs Bold Spirit Judges: Majaji wetu wanaangukia kundi gani?

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,386
73,980
Miaka ya nyuma taifa hili lilishuhudia majaji ambao walijitoa mhanga kutoa haki kadri ya sheria. Walitoa haki bila upendeleo, chuki wala kuogopa mamlaka zilizowazunguka. Walijulikana kama Bold spirits Judges.

Si wengi ingawa si hawa peke yao: Justice James Mwalusanya, Justice Mwesiumo, Justice Lugakingira, Katiti watakumbukwa daima milele ingawa tawala dhalimu zilizopita zilikataa kuwaenzi.

Kazi zao zimeshamiri katika vitabu vya Tanzania Law Reports kama precedents and judgments.

Je, Majaji wetu wa sasa unawaweka katika kundi gan kati ya "TIMOROUS" JUDGES VS "BOLD SPIRITS JUDGES"

images.jpg

Judge Mwalusanya

Hii ni quote kutoka Professor mmoja SA: Msikilize

The positive role that judges could play in Africa has been hampered by the increasing politicization of the judiciary, judicial corruption, lack of resources and judicial conservatism, according to Professor Charles Fombad of the Institute for International and Comparative Law in Africa at the University of Pretoria.

In a challenging address to the International Association of Judges’ Africa region conference in Cape Town, Fombad urged judges to take note that if these issues were not properly dealt with, the “reverse winds” of authoritarianism and the decline of good governance and constitutionalism, caused by politicians clinging to power, might prevail.

Huyu alikuwa ni Jaji pekee wa mahakama kuu ya Tanzania aliyokuwa anatoa kesi hukumu yake kama anafundisha vile. Usipoelewa hukumu za huyu jamaa bora uachane ma mambo ya sheria. Inasemekana hata Mahakama ya rufaa walikuwa wanapata tabu kupindua hukumu za huyu jamaa. alikuwa akisimamia haki, tena hata kama ni kinyume na serikali. Aliipiga chini serikali mara nyingi sana. So sad mahakama na serikali kwa ujumla wakamtupa mkono, hawakumpromote na alipostaafu hadi kufa alitelekezwa. Lakini atabaki legend kwenye mahakama ya tanzania na hadi leo hakuna jaji aliyemfikia.

Inasadikika n moja ya JAJIALIYEKUWA NA IQ KUBWA SANA TANZANIA mpaka wengine wakaa mua kumuita Lord Denning wa Tanzania.

Inasemekana Familia ya hawa jamaa (Mwalusanya) walijaaliwa uwezo mkubwa sana wa akili, huyu JAJI alikuwa na mdogo wake alisoma mpaka akaweuka kabisa akawa kichaa kabisaa na alikuwa akiamka na kuanza kutembea anahesabu hatua zake kwa kiingereza kwa wenyeji wa maeneo ya mabonde- tukuyu watakuwa mashahidi.

Historia fupi ya Jaji JAMES Mwalusanya

Full Name: *James Lewis Mwalusanya

Date of Birth: 8th September,1943

Place of Birth: Kililila village in Mbeya Region’s Rungwe District

Education: Tosamaganga Secondary School, 1960..

Cambridge School Certificate of Education Examination in 1962.. Tabora School (A Levels) between 1963 – 1964

University of E. Africa, Dar es Salaam College (Bachelor of Laws – LL.B), 1965-1969

Other Training: Compulsory National Service training at Makutupora Camp in Dodoma in 1970

Pupilage with Rweyongeza and Co. Advocates of Dodoma in 1998.

Career: Resident Magistrate Grade III in March, 1969..

Puisne Judge of the High Court of Tanzania in September, 1984.

Admitted as an Advocate of the High Court of Tanzania, in 1998NB: *He retired as a Judge of the High Court in 1997.

Important Publication:

Sheria ya Haki za Binadamu (1988); Upanuzi wa Demokrasia na Uimarishaji wa Haki za Binaadamu Katika Mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi Tanzania: Matumizi ya Katiba na Sheria Zilizopo ili Kudumisha Utulivu, Amani and Mshikamano (1993);

Utaratibu wa Sheria wa Kutatua Migogoro ya Kazi: Pale Mfanyakazi Anaapoachishwa Kazi, Kufukuzwa Kazi, Kupunguzwa Kazi, Kupewa Likizo Isiyo na Muda Maalum na bila Malipo au Kustaafishwa kwa Manufaa ya Umma (1993); and Usheria ya Mirathi: Maswali na Majibu Kuhusu Haki za Wajane (1993).



Death:

August 1, 2010.

Family:

A widow, Bumi, and five children (Mpokigwa Emmanuel, Anna Gulila, Paulina Nabwike, Enelesi Deodatha and Ernest).*If I could, I would have said,

REST IN PEACE JUDGE MWALUSANYA.
 
Ndo najua Leo kua kumbe yule tulikua tunamshangaa anatembea hatua flani afu analudi nyuma anaanza kutembea Tena akiwa anapita barabarani kakaake alikua mtu mzito serikalini .Mara ya mwisho kumuona alipita kijijini kwetu ijigha mwaka 2012(Sina uhakika)
 
Mijitu ya Mbeya Ina akili sana ndio maana CCM inapata kipindi kigumu sana huko, tofauti na Dodoma ambako njaa, ukame, umasikini na ujinga vimetamalaki
 
Ahsante mleta uzi. Mwalusanya alikuwa jaji wa aina yake ktk kizazi cha majaji wa enzi zake. Ule uandishi wake wa hukumu nao ulikuwa wa kipekee kabisa.
Kikubwa zaidi ni kusimamia maamuzi ya kuzingatia sheria bila kujali ni ys serikali ama la. Nadhani mawakili wa serikali enzi zake walipata shida sana. Maana kesi nyingi za serikali mara nyingi kama sio zote serikali ilikuwa inaangukia pua. Lakini kikubwa yule mzee unaposoma hukumu zake unaona alikuwa anasoma vitu vingi na sheria alikuwa anaijua vilivyo. Ni bahati mbaya hakufika Mahakama ya Rufaa. Lugakingira nae alikuwa vizuri mno na kiingereza chake kigumu. Mleta uzi umenikumbusha enzi hizo za kesi.
 
Back
Top Bottom