jitwangabalogi
JF-Expert Member
- Aug 8, 2018
- 329
- 387
kweli mkuu, maana ki uhalisia mtu ukiwa ndotoni ni ngumu sana kujua kama unaota(bali utaona kila kitu kipo katika uhalisia wake,kuanzia mazingira,watu,na shughuli zote zinazoendelea zipo kawaida kama haya maisha yetu ya jf,bali utofauti utakaokuwepo ni swala mda na wakati, kuhusu mda ni kwamba kila kitu kinafanyika/kutendeka papo kwa hapo, ama kufumba na kufumbua, kwa mfano ukiwa ndotoni labda ukawaza kwenda mahali tofauti na hapo ulipo utajikuta mda huohuo umefika mahali ulipokusudia, haijawahi kukutokea!? na kuhusu swala la wakati kwenye ndoto huwa halipo unaweza ukajiona umezaliwa umekua umekufa kwa wakati huohuo,ama unaweza kuishi nyakati tofauti kwa kufumba na kufumbua, ) na kama itatokea ukafanya jambo au kitu kufanyika juu yako na ukaamini 100% sio la kweli au likaleta mshangao wa kutolielewa wala kufikirika ni lazima utashituka/kuamka, kwa mfano labda unaota unakimbizwa au unataka kufa nawe ukakinzana na hiyo hali je hujikuti umeshituka ghafla usingizini!?Duuh! swali gumu ni hilo sasa je, yapi ni maisha halisi?
Kwa mtazamo na fikra zangu maisha halisi yapo katikati ya maisha haya tuliyonayo hapa jf na maisha ya ndotoni, leo usiku ukilala au kwa wakati wako wowote utakaoamua kulala ile hali itakayokuwepo katikati baada ya kuuacha huu uhalisia wa jf na kabla hujaingia ndotoni mi ndio fikra zangu zinanituma hayo ndio maisha halisi