Time Travel Kwenye Ndoto

Kapyepye Mfyambuzi

JF-Expert Member
Jun 18, 2020
542
918
(It's true my self)

Habari wakuu,
Husikeni na mada tajwa hapo juu. Baada ya kuamka muda huu nimeona sio vibaya Ku share nanyi ndoto yangu. Najua humu Tuna wasomi na wataalamu wa mambo mbalimbali. Naomba mchango wa mawazo / maono/ Tafsiri zenu juu ya ndoto yangu hii.

Niende mmoja kwa moja kwenye Mada.

Jana usiku nimechelewa Sana kulala na nilikuwa Nina uchovu mwingi sana. Nimelala ya pata kama vile Saa 7:30 ambapo Sio kawaida yangu.
,,,Jinsi nilivyo lala na kuanzia kuota sikumbuki,, nimekuja tu kupata Ufahamu kuwa nipo mwaka 1973 (mwaka ambapo bado hata sijazaliwa). Na nilijua tu bila kuambiwa na mtu kuwa huu ni mwaka 1973, kwa kujiridhisha nikawauliza tena watu wawili waliokua karibu yangu kuwa eti jamani huu ni mwaka gani wakaniambia tena kwa kunishangaa, we vipi, umeshapoteza kumbukumbu? Tumeingia mwaka 1973 - 72 tumeiacha wiki mbili zilizopita.

Chaajabu nilikuwa sijui wala sitambui kama naota nilikuwa najua nipo kwenye uhalisia ila kilichonishangaza zaidi nilikuwa nikiwaona watu am so sasa hivi ni watu wazima/ wengine wazee/ wengine walishakufa namaeneo na mitaa (ambayo haina hata lami kwa sasa ina lami na imejengeka) naishangaa Sana na kujiuliza kuwa hawa watu mbona kama nilishawahi kuwaona some where ila sikumbuki nibwapi! Hizi Barabara zenye vumbi na mitaa mingine haina hata nyumba nyingi nikiiona naikumbuka najiuliza hii mitaa mbona kama nilishawahi kuiona hapo kabla ila sikumbuki ni wapii,,!?

Ghafla nilianza kuwaona watu kwenye uhalisia wa maisha yao ya enzi zilee...!!
Nilianza kutembea kwenye mitaa mbalimbali nikianza kuyafananisha maeneo ambayo kama nayakumbuka vile ila sijui niliwahi kuyaona wapi. Nakumbuka katika tembea tembea nikakutana na Jamaa mmoja ni jirani yangu (sasa hivi ni mbaba mtu mzima) maeneo ya nyumbani kwake anayoishi, ila chaajabu eti amerudi ujanani, nikamsalimia kwa kumchangamkia ila alikuwa ananishangaa kuwa nimemjuaje wakati yeye hanijui na hanikumbuki kwa kuwa nilimtaja na jina kabisa kwenye salamu. Nilimuuliza unamjua fulani (jinalangu- ambae ndio Mimi) akasema mbona simjui? Na wakati huku kwenye uhalisia ni jamaa yangu na tunapigaga nae stori

Nili experience mazingira mengi ambayo sijawai yaona na siwezi yaelezea yote. Ila picha zilivyo kuwa zinaonekana zingine ni kama kwenye mfano wa negative photograph.

Naombeni msaada wakuu hiyo ni ndoto ya aina gani? Na inavyjumbe gani?
(Tambua nilikuwa sikumbuki kwamba nimo kwenye ndoto au hapa naota Hapana, nilipo shtuka tu ndio nikajua kumbe nilikuwa naota!)

Msaada wakuu
Mshana Jr Rakims Undava King msafiri.razaro MziziMkavu na wengineo
 
Siku moja nilipata kusoma kisa hiki mahali;
hiyo siku kulikuwa na vyura watano wamekaa juu ya gogo ambalo linaelea juu ya maji, basi chura wa kwanza akawaambia wenzie 'sijawahi kuona jinsi tunavyokwenda kwa ulaini juu ya maji haya', lakini chura wa pili akamkata kauli na kumwambia 'sisi hatuendi bali tumetulia juu ya hili gogo ambalo ndilo linajongea kwa ulaini juu ya maji haya', kabla ya kumalizia kauli yake chura wa tatu naye akampinga kauli yake kwa kumwambia 'si kweli ya kwamba hili gogo linajongea juu ya maji bali hili gogo lipo pale pale na kinachojongea ni haya maji yaliyo ndani ya mto huu',chura wa nne nae akadakia kwa juu na kusema 'sio kama maji haya yaliyo ndani ya mto huu yanajongea bali ni akili zenu ndizo ambazo zinajongea', basi bwana ukazuka mzozo mkubwa zaidi wa ule wa simba na yanga nusra ya hawa vyura kupigana kwa kila mmoja kutetea hoja yake, lakini kulikuwa na chura mwingine ambaye amekaa pembeni kimya ambaye hakutoa hoja wala kwenye mabishano yale hakushiriki, baada ya wale vyura wanne kushindwa kufikia muafaka ikabidi wamuulize yule chura wa tano ambaye alikuwa kimya kwa mda wote ili yeye ndio atoe suluhisho la chura yupi hoja yake ndio ina mashiko... baada ya kutulia kwa sekunde arobaini naye aliwaambia "sio sisi tunaojongea,wala gogo,wala maji,wala akili zetu bali kila kitu kipo palepale na hakuna kinachoenda wala kinachorudi" basi wale vyura wanne walijawa na hasira juu ya maneno yale ya chura wa tano, basi wakamkamata wakampiga kisha wakamtumbukiza mtoni!
 
Ndoto inaweza tokana na mambo mengi;

Mfano wewe ulichoka na ukachelewa kulala kunaweza kukufanya ulale usingizi mzito unaokupeka kwenye kuota.

Tafsiri ya Ndoto unaweza kuifanya kwa kuangalia matendo yaliyojitokeza kwenye hiyo ndoto. Kwa maelezo ya ndoto yako, umeota mambo ya miaka ya nyuma hii ni ndoto inayohusu watu wenye mamlaka. Inawezekana Baba yako au Babu yako ambaye sasa hayupo Duniani enzi za uhai wake aliwahi kukwambia ufanye kitu fulani na wewe hukukifanya. Anaweza kukutokea kwenye ndoto kwa staili kama hiyo kwa muonekano wa mtu mwingine ili akukumbushe utimize yale maagizo yake ya siku za nyuma.

Vitu vingine vya kuvifuatilia ni mwisho wa hiyo ndoto iliishaje?. Kulikuwa na matukio ya wewe kufurahi au kuumia?.

Ndoto mbaya ni zile tukio la mwisho labda uling'atwa na Nyoka au ulitumbukia shimoni au ulikuwa unalia gafla ukashtuka na kuamka au ulikuwa unaota unapaa angani ghafla ukaanza kudondoka ukaanguka hadi chini na kuumia sana au unaota unakimbizwa na Simba kisha akakupata na kukufanya kitoweo.

Tafsiri ndoto yako kwa kuangalia yale matukio ya mwisho ya kwenye ndoto
 
Shukrani Sana mkuu GEMBESON Kwenye ndoto hiyo sikuwa na huzuni bali nilikuwa ninafuraha ya aina yake haijawahi tokea, nili-enjoy sana, mpaka nafikia hatua ya kushtuka usingizini nilijikuta ni mwenye furaha hali ya kuwa sijapata Siri yoyote kwenye ndoto hiyo. Nilichokikumbuka ni kuwa nimeota/ Kuya experience maisha ya miaka ya nyuma yalikuwaje kupitia kwenye ndoto.
Huenda ikawa Kuna Siri lakini kumbukumbu imefuta sikumbuki zingine zimefutika
 
Poa. Ndoto zenye kuisha kwa matukio ya furaha kama hii yako hazina shida.

Kama unaishi Mikoani au uko mbali na wazazi wako, ni wazi unakumbushwa kuwakumbuka wazazi wako ndio sababu ya kuota mazingira ya siku za nyuma pamoja na kuota upo na mtu aliyekuwa kijana siku za nyuma.
 
Siku moja nilipata kusoma kisa hiki mahali;
hiyo siku kulikuwa na vyura watano wamekaa juu ya gogo ambalo linaelea juu ya maji, basi chura wa kwanza akawaambia wenzie 'sijawahi kuona jinsi tunavyokwenda kwa ulaini juu ya maji haya', lakini chura wa pili akamkata kauli na kumwambia 'sisi hatuendi bali tumetulia juu ya hili gogo ambalo ndilo linajongea kwa ulaini juu ya maji haya', kabla ya kumalizia kauli yake chura wa tatu naye akampinga kauli yake kwa kumwambia 'si kweli ya kwamba hili gogo linajongea juu ya maji bali hili gogo lipo pale pale na kinachojongea ni haya maji yaliyo ndani ya mto huu',chura wa nne nae akadakia kwa juu na kusema 'sio kama maji haya yaliyo ndani ya mto huu yanajongea bali ni akili zenu ndizo ambazo zinajongea', basi bwana ukazuka mzozo mkubwa zaidi wa ule wa simba na yanga nusra ya hawa vyura kupigana kwa kila mmoja kutetea hoja yake, lakini kulikuwa na chura mwingine ambaye amekaa pembeni kimya ambaye hakutoa hoja wala kwenye mabishano yale hakushiriki, baada ya wale vyura wanne kushindwa kufikia muafaka ikabidi wamuulize yule chura wa tano ambaye alikuwa kimya kwa mda wote ili yeye ndio atoe suluhisho la chura yupi hoja yake ndio ina mashiko... baada ya kutulia kwa sekunde arobaini naye aliwaambia "sio sisi tunaojongea,wala gogo,wala maji,wala akili zetu bali kila kitu kipo palepale na hakuna kinachoenda wala kinachorudi" basi wale vyura wanne walijawa na hasira juu ya maneno yale ya chura wa tano, basi wakamkamata wakampiga kisha wakamtumbukiza mtoni!
Inafikrisha sana
 
...na huo ndio mwanzo wa kuutafuta ukweli kama yeye ni binadamu anayeishi mwaka 1973 ambapo sasa akilala anaota yupo mwaka 2021, au yeye ni binadamu anayeishi mwaka 2021 ambapo akilala anaota yupo 1973!?...
Dah!
Hapo mkuu jitwangabalogi umenifikirisha tena, inamaana kwenye ulimwengu wa roho naweza kuwa bado nipo 1973? japokuwa nilikuwa bado kuzaliwa! wakati kwenye ulimwengu wa mwili nipo 2021!!
Hii inawezekana kweli!?
 
Ulimwengu wa roho ni upi na ulimwengu wa mwili ni upi!? kama unamaanisha ukiwa ndotoni ndio ulimwengu wa roho pia ukumbuke hata pia mwili unakua nao, na ndio maana ndotoni tunazaliwa,tunakula,tunasoma,tunaoa na kuolewa,tunapigana,tunasali/swali,tunauana,tunarogana,tunapata ajali na hata pia tunakufa,(hivyo mwili na roho vyote hata ndotoni tunavyo) je huu unaouona ni ulimwengu wa mwili unatofauti wowote na huo ulimwengu wa roho!?
hizi ishu za kiroho mi mwenyewe huwa zinanichanganya sana na mda mwingine majibu nakosa...tuchukulie tu mfano wa ndoto yako "wewe hapa tunavyochati jf kwa mtazamo wako na watu wote nami pia nikiwemo tupo mwaka 2021, je unaweza kweli kumuaminisha mtu wa hapa jf ya kwamba tupo mwaka 1973!?...la hasha bali utaoneka we ni kichaa,umechanganyikiwa, au unaota sivyo!? lakini je ukilala na usingizini ukaota upo mazingira ya mwaka 1973 wewe pamoja na wale wote waliokukuzunguka katika maisha yako ya ndotoni je unaweza kuwashawishi mpo mwaka 2021!? la hasha nao wataona wewe ni mwehu au upo ndotoni unaota. swali sasa ni je? yapi ni maisha yako halisi!? hapa tunapochat jf ni uhalisia wako au unaota!? au je ni yale mazingira 1973 ni uhalisia wako au upo ndotoni...
 
Duuh! swali gumu ni hilo sasa je, yapi ni maisha halisi?

Similar Discussions

Back
Top Bottom