TiGo nivushe mmeiba pesa yangu

nxon

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,162
406
Habari !

Naitwa Nickson Kimambo naishi Morogoro mjini ni mtumiaji wa mtandao wa TIGO TANZANIA. no zangu ni 0717693927

Jana tarehe 26 december 2020 nilijiunga na kifurushi cha internet cha wiki kwa tsh 3000/- kwa njia ya tigo pesa, baada ya hapo nikaletewa sms kuwa kifurushi changu cha internet kimedadilishwa kuwa salio la kawaida ili kiweza kulipia mkopo wa tigo nivushe.

Kwa kumbukumbu zangu sijawahi kuomba mkopo wa tigo nivushe hata siku moja pia hawakunipa taarifa kuwa nilikopa shilingi ngapi na nimelipa shilingi ngapi? ila pesa yangu imekatwa.

Leo tar 27 december2020 nimepiga simu huduma kwa wateja kuomba ufafanuzi kwa nn pesa yangu ikatwe wakati sijawahi kukopa kigo nivushe? Muhudumu akajibu kuwa nilikopa tar 7 november 2020, wakati sio kweli kwamba nilikopa.

Nikamuuliza swali marejesho ya mkopo huwa ni siku ngapi? akajibu ni siku 3, nikamuuliza tena iwaje nikatwe tareh 26 december 2020? akaijibu nilikuwa siweki salio, wakati sio kweli naweka salio karibu kila wiki najiunga na vifurushi vya wiki.

Hivyo naomba muongozo wa suala hili
 
Nakumbuka nipo Moro town kama 2012 kama sijakosea sikua hata na mia ya nauli nikatumiwa 5000 Kwa tigo pesa

Aisee nilitapeliwa sikuipata iyo 5000 mpaka kesho toka apo sikuwahi kutumia tigo pesa

Na laini nikajaga kutupa.
 
Tigo Pesa Ni wezi sana, Waliwahi kunikata 32,000 kwenye simu kuwa heti nimejiunga kifurushi kupitia facebook wakatihuo nilikuwa siko hata sehemu naweza kutumia internet na nilikuwa nina kama miezi miwili sijaingia Fb, na fata facebook activity ilikuwa haionyeshi kuwa nilinunua salio..

Nilihangaika kupiga simu huduma kwa wateja wanarukaruka tu hakuna majibu yakueleweka sijawahi kuipata hiyo hela hadi leo. TIGO NI WEZI
 
Back
Top Bottom