Airtel huduma yenu ya mteja kuomba atumiwe pesa ni nzuri lakini inachochea utapeli, rekebisheni wateja wanalizwa

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
370
1,446
Wakuu salaam,

Airtel kama mitandao mengine ina huduma inayokuwezesha kuomba kutumiwa pesa na mteja mwingine (kwa TiGO sijaona huduma hii), lakini kwa Airtel iko tofauti kiasi.

Kwa Airtel unaweza kutuma maombi hayo kwa mtu mwingine anayetumia Airtel pamoja na wateja wa mitandao mengine, yaani kama mimi ni mteja wa Airtel naweza kuomba unitumie pesa wewe mteja wa Vodacom au TiGO, hilo siyo tatizo, tatizo linakuja pale ambapo ujumbe huo unakwenda kama AirtelMoney, yaani ukipokea ujume pale juu inasoma kama AirtelMoney na kukwambia;

AirtelMoney

Hello, (jina la anayekuomba pesa) requested you to send money 1000000Tsh on their Airtel number (namba yake). Enjoy Sending Money for FREE with Airtel Money and other affordable services.


airtel.jpg

Ujumbe ukija hivi kama mtu usipokuwa makini unaweza kufikiri umetumiwa pesa, na hapa ndio matapeli wanatumia tobo hili.

Tapeli anakupigia simu anakwambia napiga simu kutoka Airtel, kuna mteja ametuma pesa kwako kimakosa hivyo wanaomba urudishe muamala huo, na walivyokuwa wajanja wanarequest hela ndogo tu kama vile elfu 50 ambayo ni rahisi mtu kuwa na kiasi hiko kwenye simu na hutaingia ugumu kurudisha muamala huo.

Najua mitandao inatoa elimu mtu akikosea kukutumia pesa usirudishe muamala huo bali aliyekosea ndio afanye reverse, tukichukulia uhalisia wa watanzania elimu hii inafikia watu wangapi? Ukichanganya na ule ubinadamu ambao Watanzania tuko nao mara nyingi mtu hatasita kutuma pesa hiyo.

Ukiangalia kwa haraka haraka unaona kweli ni ujumbe kutoka Airtel Money hivyo unatuma pesa bila wasiwasi. Jambo jingine ni kuwa lugha inayotumika ni kingereza pekee tofauti na mintando mingine kama Voda ambako ukitumiwa ombi kama hilo kwanza inakuja namba ya mteja halafu unawekewa kwa lugha mbili, hapa hata kwa mtu ambaye Kiingereza kinampa tabu naweza kuelewa kwa Kiswahili.

Airtel badilisheni namna huduma hii inafanyika, badala ya ujumbe kwenda kama Airtel Money iende namba ya muhusika akiwa anaomba salio, lakini pia wekeni kwa na tafsiri ya Kiswahili, ili hata ambao Kingereza kinawapa tabu waweze kuelewa kuwa hapa ni mtu mwenyewe anaomba kutumiwa pesa hii, na kwakuwa hayupo kwenye orodha yako ya namba moja kwa moja utaelewa huyu ni tapeli. Lakini pia elimu iwe ni endelevu, sio mkishafanya kipindi fulani basi ndio ntolee hiyo

Nilipowatafuta Airtel Huduma kwa Wateja hawakuonekana kushtuka, hivyo nikapigia mstari suala hili si geni kuripotiwa kwao, na watu wengi wameshakutana na utapeli wa aina hii lakini hawajachukua hatua kurekebisha.

Nakuwekea hapo chini jinsi mtu anaweza kutuma ombi kwako (si ili muanze kutapeli watu watu Wakuu, bali muwe wamakini na utapili wa aina hii na Airtel wabadilishe namna huduma hii inatolewa) wasije kukana kuwa siyo kweli.

photo_2_2024-07-09_08-28-19.jpg

photo_9_2024-07-09_08-28-19.jpg

photo_3_2024-07-09_08-28-19.jpg

photo_5_2024-07-09_08-28-19.jpg


photo_8_2024-07-09_08-28-19.jpg

pesa.jpg

photo_4_2024-07-09_08-28-19.jpg
airtel.jpg

Na hivi ndivyo ujumbe inavyoonekana kwa mteja Airtel au mtandao mwingine anapoombwa salio hilo
 

Attachments

  • photo_10_2024-07-09_08-28-19.jpg
    photo_10_2024-07-09_08-28-19.jpg
    47.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom