TIGO ni mtandao mbovu kuliko yote Tanzania kwa sasa.

snipa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
4,301
1,793
Naamini hili wazo sio mimi tu binafsi ambaye ninalo, no ni watu wengi.
Sikuwahi jijengea mtizamo wakuamini hivi lakini kwa sasa Tz sioni mtandao mbovu kama TIGO, hakuna kabisa.
Bora mtandao uwe unakata afu unarudi, lakini sio unaona kabisa mtandao uko full afu kinachoendelea hakuna.
Hili jambo wanaliweza TIGO peke yao hakuna wengine sijaona kabisa.
Bora ningekuwa naishi kijijini huko au pembeni kidogo ya jiji lakini hapa hapatown wanapo promote 4G zao hizi bado matatizo kibao.

1- HUDUMA ZA INTERNET WANATOA USIKU
Mchana nimetumia sana hawa jamaa lakini kwenye simu kidogo wanafariji lakini sio kwenye PC, yaani chenga kabisa kama wanagawa bure vifurushi, mpaka mida ya usiku usiku hapo kidogo unaweza kuona speed inakuja kuja.

xcQMq7.png


WhatsApp nayo ni hai ile ile, picha ya 25KB inadownload kama 20GB

2- NAMBA HAIPATIKANI HATA IKIWA HEWANI
Hili swala kwa hawa jamaa ni lakawaida sana na imefikia hatua wamelizoea, wanachukulia kawaida tu binafsi nionavyo maana ni zaidi ya mara moja unaweza mpigia mtu na asipatikane, na baadae lawama zianze mwishowe ugomvi. (Tigo hapa wanaweza leta migogoro kwenye ndoa za watu, ni vyema hili liangaliwe sana)

3- TIGO PESA HAIRUDISHI SMS
Ni mara kadhaa hili nimeliona na lizoea, unaingiza hela kwa wakala na sms sipati, ila ukijaribu kununua salio inakubali, hapo ndipo ninapowezaga kuangalia salio, maana sio kama voda, wao voda unaweza mtumia mtu hela isiyo sahihi na ukajua salio lako la MPESA, ila Tigo hili swala hawana, na siwezi kuwalaumu ila nitakachowalaumu ni kutokupata sms baada ya transaction na wakala.

4- UONGO (UTAPELI)
Tigo kwao kuongea uongo wameona ni jambo la kawaida sana, nimepokea sms zao nyingi sana wakinibembeleza ninunue salio kwa Tigo Pesa na wataniludishia hela yangu ile ile kwenye Tgo pesa, lakini la hasha, hawafanyi hivi, huu ni utapeli na uongo uliopitiliza.

Halotel wamekuja juzi juzi tu hapa,na tukisema tuangalie uhalisia kabisa Halotel wako vizuri kwenye huda husika zinazotumika a watu wengi kwa sasa hasa internet.

@snipa
 
Naunga mkono hoja! mi nipo morogoro mjin kabisa mitaa ya misufi lakin mtandao unasumbua kama nipo sitimbi vile, co mm tu hata ma bro zangu nao pia mtandao majanga, kwel tigo biashara imewashinda
 
Hahahahaha Hadi Raha Mi nishaapa Silei Mtandao wa Simu Ni Kuhama Tu panapoeleweka.. Yaani Nikiwa Eneo fulani Tigo Inakubalika Naweka Tigo.. Nikiwa Mahali Tigo Wabovu Naweka Line Pembeni nachukua Inayopiga Mzigo Fresh
 
Nime download live soccer tv naangalia city kupitia bt1 raha sana na 4G LTE YA TTCL
 
Nime download live soccer tv naangalia city kupitia bt1 raha sana na 4G LTE YA TTCL
TTCL wako vizuri toka kitambo ila walikua wanazingua vocha zao kuzipata, now kidogo hizi changes zitawaboost sana, kama hawatafanya kama anavyofanyaga Mgema.
 
kwa wakazi wa Dar mimi naona haina maana tena ya kutumia 3G wakati same Bundle inayotumika kwenye 3G inaweza tumika kwenye 4G
Modem zao za 4G zilikua bei yakutupa kabisa hivo opting for 4G kwa Upande wa internet ingekuondolea kero moja wapo kati ya hizo ulizozitaja
 
kwa simu kuwa hewani halafu haipatikani ni jambo la kawaida kabisa kwa huo mtandao. unapiga simu haipatikani illa kwa kuwa unajua tatizo lao ukirudia tena inaita.
 
Line za TTCL zinapatikanaje wakuu?je vifurushi vyao unaweza kununua kama tunavyonunua vya airtel na tigo kupitia airtel money au tg pesa?
 
Mimi nashangaa mtandao unakata hata kama nilikuwa sehemu ambayo mnara unasoma full-kweli tiGO majanga!!!

Labda mitambo imechakaaa
 
Back
Top Bottom