Geita: Mawasiliano kwa mtandao wa tiGO ni changamoto

Twin Tower

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
2,133
2,986
Nimekuwa mtumiaji wa huu mtandao kwa zaidi ya miaka 18 (nikibadirisha chip mara moja tu kuendana na mahitaji ya mabadiriko ya teknolojia) sasa enzi hizo buzzy ni bomba na ile longa longa ukikesha huku ukihangaika kupata laini… enzi hizo mabibo hostel vijana usiku ndo ulikuwa muda wa story
Ndi ndi ndi aaaa , e bwana eee.

Lakini kwa takribani zaidi ya wiki sasa mawasiliano ya tigo yamekuwa hafifu sana, scratch nyingi, mikoromo ya kutosha, hata kupiga simu hadi itoke ni kujitafuta sana.

Kama ndiyo maboresho mnayofanya baada ya kubadirisha jina la MIC, huu mtandao sasa tunaenda kuuhama.

Nimejaribu kuwatafuta kupitia namba yao ya huduma kwa wateja bila mafanikio yeyote ile.

Sisi kama wateja hamuwezi kuwa mnatufanyia haya mambo ya huduma za hovyo, bando likiwa juu tuendelee kuwachukulia poa.
 
dah!! ila hata wewe ni mvumilivu na mstahimilivu sana. Yaani hata hujastuka wale vijana wanaosajili lini mitaani na vispeaker huwa hawaitaji Tigo coz ni changamoto
 
Habari Niko Geita wilaya ya bukombe kata ya bugelenga, niko huku karibu mwaka sasa na kumekua na changamoto iliyokosa utatuzi kwa muda mrefu sasa (nimeikuta)

Eneo nililopo tuna MNARA wa tiGO lakini chakushangaza mnara huu ni kama haufanyi kazi. Muda wote simu huandika EMERGENCY na ikitokea ikasoma mtandao hakuna mawasiliano yeyote yanayoweza kufanyika

Tumejaribu kuwatafuta wahusika wa tiGO bila mafanikio, naamini kupitia jamii forums kilio chetu kitakwenda kusikika.

Eneo mnara ulipo pana umeme lakini chakushangaza mnara unatumia solar.. Hivyo likiingia giza kidogo mawaziliano hupotea.

Siku zote wakazi wa eneo hili hatuwasiliani nyakati za usiku kwakua huwa mtandao umeshuka.. Na mchana mtandao huwa hafifu mnoo.

Ombi
Wahusika waje kuboresha mnara tupate mawasiliano ya uhakika saa 24

Pili
Wahusika wa tiGO waje kuboresha mnara huu.. Kwan tunaamini unatumia technology ya zamani sanaa (line katika smartphone huonesha 2G) Waje watufungie 4G ili tupate internet anbayo hatuipati kwa muda mrefu sasa

Tatu
Kwakua eneo ulipo mnara umepita umeme waje wafunge na umeme ili tuwe tunapata mawasiliana hata nyakati za mawingu na nyakati za usiku.

Jamii forums naamini mnakwenda kutusaidia kutatua changamoto hii. Ahsante

Screenshot_2023-10-26-12-03-40-52.png
16985331238551670781028.jpg
 
Back
Top Bottom