Tigo na Voda mnatuibia kwa kutulazimishia bando za Usiku

TENGEFU

Senior Member
Jan 25, 2017
138
206
Nimeingia kununua bando mitandao yote kwa mtandao wa Tigo kama kawaida kwa kupiga *147*00# na voda *149*01#. baada ya kubonyeza button ya mwisho nikapokea kifurushi cha mwezi lakini kimeandikwa kitakuwa kinatumika kuanzia saa 4 usiku hadi saa 11:59 asubuhi.

Huu ni wizi mkubwa kwa sababu mnafanya haya bila makubaliano na mteja AMBAYE LENGO NI KUNUNUA BANDO LA MASAA 24. Mbaya zaidi mnafanya hivi kwa kumtega mteja bila kumpa prio information kuwa ni bando la usiku.

Kifurushi hiki hiki ndicho tulichokuwa tunanunua kwa matumizi masaa 24. leo mnabadilisha bila kumpa taarifa mteja huu ni wizi mkubwa na itabidi wanasheria mtusaidie kuwachukulia hatua.

Kama walipata hasara kipindi cha uchaguzi siyo sisi tuliosababisha maana inaonekana wanataka kufidia hasara kwa migongo yetu.

ninao ushahidi na ninaandika kwa sababu nimenunua vifurushi vya jumla ya 20000 na vyote vnikalazimishwa nianze kutumia saa 4 usuki.

Huo muda huwa ni wa kulala na wao wanajua kwa kinachofanyika hapa ni uhuni na wizi.

Naomba mamlaka husika pia watusaidie ili turudishiwe hela zetu.
 
TCRA wako kimya, wakati tigo au voda wanabadilisha tu vifurushi na kuwaibia watanzania, mimi nailaumu sana sana TCRA.. yaani tigo, voda wanacheza sana na watanzania na kuwaibia kupitia data na vifurushi vingine vya kupiga..
 
Tigo wana bando za kipumbavu kwa sasa, muda wowote from now naweza kuwahama.

Mwanzo walikua na offer za gb1 na dakika 100 kwa muda wa siku 3. Kwa sasa Wameziondoa dakika, na wamebakiza mb tu.
 
Tigo wana bando za kipumbavu kwa sasa, muda wowote from now naweza kuwahama.

Mwanzo walikua na offer za gb1 na dakika 100 kwa muda wa siku 3. Kwa sasa Wameziondoa dakika, na wamebakiza mb tu.
Ndio kulimia meno kwenyewe kama ulikua hujui
 
Back
Top Bottom